USIRUHUSU WATU KUTUMIA HISTORIA YAKO KUKUNYANYASA! Kuna mambo mengi ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma, kuna hatua nyingi ulipitia, zipo nzuri zipo mbaya, kuna mambo mengi ambayo unatamani kuyasahau katika maisha yako lakini huwezi, kuna mambo mengi unatamani kuyabadilisha katika maisha yako lakini huwezi. Yameshatokea na ni sehemu ya maisha yako, haya tunayaita historia, si sehemu tena ya maisha yako, wewe ni mtu mpya, huwezi kubadilisha historia lakini usijihukumu au kuruhusu watu kukuhukumu kutokana na historia yako. Ulikua Malaya kweli, ulikua mwizi kweli, umetoka katika familia ya kimasikini, ulikua mshamba, ulikua unadanga, ulikua marioo na chochote kile ambacho ulikua, kama umeshapita katika hali yoyote mbaya na sasa hauko huko cha kufanya ni kuangalia historia na kumshukuru Mungu hauko kule tena. Acha kujihukumu, acha kujisikia vibaya na kubwa kabisa usiruhusu watu kukufanya ujisikie vibaya. Anaweza kuwa mume au mke, wanaweza kuwa majirani au ndugu, watataka kukudharau k...
Karibu tuzungumze hapa ndipo kituo chako bora cha maarifa ,karibu useme, niseme, waseme na sisi tunasema 2018. ni sehemu pekee ya kila mmoja kutoa maoni yake na uwelewa wake juu ya kuelimisha jamii. ukiwa unachochote cha kutaka kutushirikisha kupitia jukwaa hili la wana jamii, usisite kututumia baraua pepe kwenda kwa bahatimagweiga467@gmail.com au wasiliana nasi kwa simu namba 0757472165, 0659991953. huduma zetu ni masaa 24