Ndugu zangu, nimeongea kuhusu baraka na heri ya kuwa na mwanamke wa pekee pia ni vizuri kwa wakina dada na wanawake kutambua kuwa nao wanatamani sana kuwa na mume wa namna hii. Hii pia ni namna moja ya sisi wanaume kujidai katika ndoa zetu. Mke huyu ana heri anapompata mume wa namna hii: 1️⃣ Mume anayemjua Mungu na anaishi maisha ya kumpendaza Mungu. 2️⃣ Mume anayetambua kuwa yeye ni baba wa familia, mume wa ndoa na mlinzi wa familia. 3️⃣ Mume anayejua kuwa mke wake anatakiwa kusikiliza na siyo kukaripia na kugombezwa kama mtoto na wakati mwengine kutamkiwa maneno makali mbele ya watoto. 4️⃣ Mume ambaye ana uwezo wa kujishusa pale anapofanya kosa, anapoumiza hisia za mke wake. 5️⃣ Mume ambaye anatambua ulimwengu wa mwanamke na anatambua mahitaji ya mke wake. 6️⃣ Mume ambaye anashirikisha mambo ya familia na ndoa kwa mke wake na wanapanga mipango mbalimbali ya familia kwa pamoja. 7️⃣ Mume ambaye anatambua kuwa ni wajibu wake kuwa na muda wa pekee wa kuwa na mke wake, kama vile ...
Karibu tuzungumze hapa ndipo kituo chako bora cha maarifa ,karibu useme, niseme, waseme na sisi tunasema 2018. ni sehemu pekee ya kila mmoja kutoa maoni yake na uwelewa wake juu ya kuelimisha jamii. ukiwa unachochote cha kutaka kutushirikisha kupitia jukwaa hili la wana jamii, usisite kututumia baraua pepe kwenda kwa bahatimagweiga467@gmail.com au wasiliana nasi kwa simu namba 0757472165, 0659991953. huduma zetu ni masaa 24