Skip to main content

Posts

Showing posts from August 11, 2018

LAZIMA KUCHAGUA KUNYAMAZA.

                              MITHALI 11:12  Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. MITHALI 17:28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu. Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba tunataka kuongea kila wakati, tunataka kujibu kila tunachokisikia, kila tunachokiona tunataka kukisemea kitu. Kuna wakati tunasikia na kukutana na mambo ambayo kiuhalisia moyo unagoma kabisa kunyamaza, unatamani ujibu, unatamani uwaambie watu yale umefanyiwa, unatamani uelezee vile umeumizwa lakini kumbe si kila jambo linatakiwa kuongelewa. Si kila ukionacho unatakiwa kukisemea kitu. Si kila usikiacho/uambiwacho ni lazima ujibu. Si kila ufanyiwacho ni lazima umwambie kila mtu. MUHUBIRI 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; I...