Skip to main content

Posts

Showing posts from June 28, 2018
Harusi ya Kana 1   Yn 1:43  Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.  2 Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.  3 Hata divai ilipowaishia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.  4 Yn 19:26; Mt 12:48; Mk 1:24 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.  5 Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni.  6 Mk 7:3,4  Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kunawa, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.  7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza mpaka juu.  8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa sherehe. Wakapeleka.  9 Naye mkuu wa sherehe alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa sherehe alimwita bwana arusi,  10 akamwambia, Kila mtu kwanza huand...

USHUHUDA WA YOHANA MBATIZAJI

Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji 19   Lk 3:15,16  Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?  20 Mdo 13:25  Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.  21 Kum 18:15,18; Mal 4:5; Mt 17:10; Yn 6:14; 7:40  Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.  22 Basi wakamwambia, U nani? Na tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wanenaje juu yako mwenyewe?  23 Isa 40:3; Mt 3:3; Mk 1:3; Lk 3:4 Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.  24 Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo.  25 Mt 21:25  Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?  26 Mt 3:11; Mk 1:7,8  Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi....

sulemani mwana wa daudi

    Methali za Sulemani +  mwana wa Daudi, +  mfalme wa Israeli: +   2   Ili mtu ajifunze *  hekima +  na nidhamu; Ili aelewe maneno ya hekima;   3   Ili apate nidhamu +  inayoleta ufahamu, Uadilifu, +  busara, * +  na unyoofu; *   4   Ili kumfanya mjinga awe mwerevu; + Ili kumpa kijana ujuzi na uwezo wa kufikiri. +   5   Mtu mwenye hekima husikiliza na kujifunza zaidi; + Mtu mwenye uelewaji hupata mwelekezo stadi * +   6   Ili kuelewa methali na fumbo, * Maneno ya wenye hekima na vitendawili vyao. +   7   Kumwogopa *  Yehova ndio mwanzo wa ujuzi. + Ni wapumbavu tu wanaodharau hekima na nidhamu. +   8   Mwanangu, sikiliza nidhamu ya baba yako, + Wala usiyaache mafundisho *  ya mama yako. +   9   Ni shada linalovutia kwenye kichwa chako + Na pambo maridadi shingoni mwako. + 10   Mwanangu, watenda dhambi wa...