Skip to main content

Posts

Showing posts from December 7, 2018

USHAURI KWA WATOTO WA KIKE #MSIPOTEE KABLA YA KUTIMIZA MAKUSUDI MAALIMU

JINSI BINTI ANAVYO WEZA KUEPUKA KUCHEZEWA NA KUPOTEZA NDOTO ZAKE KIMAISHA  Wakati watu wawili mwanamke na mwanaume wanapokuwa kwenye kilele cha mapenzi, ni rahisi sana kila mmoja kuchunga kauli zake na kuongea yale ambayo yatamvutia mpenzi wake ili kila mmoja awe na mvuto kwa mwenzake na hivyo kuwa karibu zaidi. Hata hivyo watu wengi (hususan wanawake) wanashindwa kung'amua kwamba, katika mapenzi kila mmoja ana lake moyoni, na ni vigumu kujua mwenzako anawaza nini juu yako. Katika mahusiano mara nyingi wanawake ndio huumizwa kwa sababu wakati mwingine mwanaume anapomtaka mwanamke humpa matarajio makubwa kuhusu hatima yao ili kumvuta, lakini kumbe analo lake moyoni na hapo ndipo mwanamke hujikuta akijitolea kwa hali na mali akijua kwamba, mwenzake amempenda na wataoana wakati kumbe mwenzie wala hana mpango huo. Ni vyema kama mwanamke akiamua kujiingiza kwenye uhusiano, basi awe na uhusiano na mwanaume ambaye anaonekana dhahiri kuwa ni muoaji na si wa kumchezea tu, na kuingia mit...