Skip to main content

Posts

Showing posts from November 12, 2021

MAHITAJI MUHIMU KABLA YA KUWEKA VIFARANGA BANDANI.

 MAHITAJI  MUHIMU KABLA YA KUWEKA VIFARANGA BANDANI : Unapotaka kuanza ufugaji wowote wa kuku lazima uwe na mahitaji muhimu ya kusaidia muradi wako ukuwe vyema na kuepukana na changamoto.   Miongoni mwa mambo muhimu ni kama vile.  1. Banda kulingana na idadi ya vifaranga unavyotaka kuweka.  Usizidishe vifaranga katika banda moja ili kuepusha ukuaji hafifu na matatizo mengine kama vile kudonoana.  Hakikisha banda limezingatia kanuni zote za ujenzi ikiwemo  ✔️uelekeo wa upepo  ✔️upauwaji wa paa ✔️uelekeo wa maji yani lisiwe katika mkondo wa maji  ✔️Hewa iingie na kutoka kwa usahihi ili kuzuia mambukizi zaidi ya magonjwa pale yanapokuwa yametokea.  2.  Vyombo vya chakula na maji kulingana na Idadi sahihi ya vifaranga.  Kwa mfano vifaranga 100 wanahitaji Vyombo 3 vya maji na vitatu vya chakula ndani ya siku 30 mpaka 45 3. Vyungu joto au taa za umeme za kulelea vifaranga  4. vitaru vya kulelea vifaranga endapo banda ni kub...