Leo ningependa tuangalie kidogo kuhusu vita ya kimawazo Siku moja nikiwa nimelala, naliota ufalme wa Mungu na ule wa Shetani upo katika vita. Kila upande ulikuwa unafanya bidii kuhakikisha mawazo/matakwa yake yanatekelezwa kupitia mtu. Naam niliota kuna kitu Mungu anataka kizaliwe duniani kupitia mtu na Shetani naye akawa akipinga kile cha Mungu kwa kuleta cha kwake kizaliwe kupitia mtu huyo huyo. Baada ya kutafakari ndoto ile ndipo nikapata ujumbe huu, sasa endelea kujifunza. Kwanza ni vizuri ukafahamu kwamba, ikiwa Mungu ana mawazo ya amani juu yako(Yeremia 29:11), basi, Shetani pia ana mawazo ya uharibifu juu yako. Na hii ina maana kila siku mwanadamu atakutana na vita ya nini atekeleze katika ufahamu wake, naam hii ndiyo vita ya mawazo. Mungu atapigana kuhakikisha mawazo yake juu yako yanafanikiwa na Shetani naye atapigana kuhakikisha mawazo yake kupitia wewe yanafanikiwa. Kumbuka kwamba Mungu anapotaka kufanya jambo lolote chini ya jua anatumia njia ya kuweka wazo ndani y...
Karibu tuzungumze hapa ndipo kituo chako bora cha maarifa ,karibu useme, niseme, waseme na sisi tunasema 2018. ni sehemu pekee ya kila mmoja kutoa maoni yake na uwelewa wake juu ya kuelimisha jamii. ukiwa unachochote cha kutaka kutushirikisha kupitia jukwaa hili la wana jamii, usisite kututumia baraua pepe kwenda kwa bahatimagweiga467@gmail.com au wasiliana nasi kwa simu namba 0757472165, 0659991953. huduma zetu ni masaa 24