Skip to main content

Posts

Showing posts from November 10, 2021

UPANGILIO WA CHANJO KWA VIFRANGA.

MPANGILIO SAHIHI WA CHANJO KWA VIFARANGA CHOTARA NA KIENYEJI ............................................. Vifaranga ili wakuwe vyema na kusitawi ni lazima wazingatiwe katika chanjo na chakula bora.   Chanjo humsaidia kifaranga kujikinga na magonjwa hatari ambayo hayana dawa kama vile mdondo,  mahebe  ,  Gumboro na ugonjwa wa ndui.  Haya ni magonjwa ambayo yakitokea Katika shamba huweza kuleta vifo na hasara kubwa kwa mfugaji.   Magonjwa haya huwa yana chanjo na sio dawa hivyo mfugaji anapaswa kuzingatia ratiba za chanjo kwa usahihi     *RATIBA ZA CHANJO*  SIKU 1.    MAREK'S SIKU 7.    NEWCASTLE SIKU 14.    GUMBORO SIKU 21   NEWCASTLE SIKU 28   GUMBORO SIKU 35     NDUI Katika hizo chanjo , chanjo mbili hutolewa kwenye bawa ambazo ni chanjo ya marekes  na  chanjo ya ndui.  Chanjo zilizobakia huchanganywa katika maji Kwa maelekezo sahihi ya kitaalamu....

USIMAMIZI WA KUKU WANAO TAGA.

 SABABU ZA KUJIENDESHA KIHASARA KATIKA UFUGAJI Ufugaji ili ukuletee matokeo chanya inakutaka mfugaji utumie akili nyingi na mbinu sitahiki . Kuliko matumizi mengi ya pesa akili kidogo  ( maarifa ) Nimewahi kusema huko nyuma Kwamba kabla hujaweka pesa zako kwenye tasinia ya ufugaji inakuhitaji kwanza uwekeze kwenye upatikanaji wa Elimu sahihi kuhusu ufugaji.  Kinyume cha hapo ni kuhatarisha mtaji wako. Wapo watu wanaingia kwenye tasinia hi ya ufugaji kwa sababu wanapesa.  Ukweli usiopingika ni kwamba pesa haiwezi kuzuia kuku kufa isipokuwa maarifa sahihi ya ufugaji ndio yatakusaidia kujua 👇 ✔️ Anaumwa nini  ✔️Atumie dawa gani  ✔️Kwa nini Anaumwa  ✔️ dozi sahihi kwa ugonjwa alionao  ✔️Ataweza kupona?  ✔️Anaweza kuambukiza wengine  ✔️Ni magonjwa yatokanayo na ukosefu wa chanjo au mazingira wanayoishi? ? Ukisema unafuga kwa sababu unapesa itakusaidia kuzuia magonjwa kwa kununua madawa sio kweli kwa sababu kuna kipindi inafikia kuku wanagoma...