by Lameck & Faustina Mtaka USIHARAKISHE . Usiharakishe na kukurupuka kutafuta mchumba kabla ya wakati muafaka.Pengine unaweza kujiuliza ni wakati upi ni muafaka kutafuta au kuwa na mchumba?ni wakati unapokuwa umekomaa kiroho, kiakili na kimwili umejitambua kikamilifu ulikotoka, mahali ulipo na unapokwenda na umetathimini kwa makini mipango na ratiba yako ya sasa na ya baadaye ndipo waweza kuchukua hatua hii mhimu katika maisha. Wengi wamepuuzia hili na kukurupuka kutafuta mchumba bila kujitathmini na kuishia kwenye uasherati na usaliti vilivyowaletea huzuni na majuto badala ya furaha na ndoa takatifu. Biblia inasema “ Ni nani katika ninyi Kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kumalizia asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi watu wote waonao wakaanza kumdhihaki…….” (Luka 14:28-30). USITAFUTE MCHUMBA KWA MSUKUMO KUTOKA NJE. Usitafute mchumba Kwa kuangalizia, kushawishiwa, kuiga au kusuk...
Karibu tuzungumze hapa ndipo kituo chako bora cha maarifa ,karibu useme, niseme, waseme na sisi tunasema 2018. ni sehemu pekee ya kila mmoja kutoa maoni yake na uwelewa wake juu ya kuelimisha jamii. ukiwa unachochote cha kutaka kutushirikisha kupitia jukwaa hili la wana jamii, usisite kututumia baraua pepe kwenda kwa bahatimagweiga467@gmail.com au wasiliana nasi kwa simu namba 0757472165, 0659991953. huduma zetu ni masaa 24