Skip to main content

Posts

Showing posts from July 15, 2018
Bwana Yesu asifiwe nipende kukukaribisha tena katika somo langu jipya la jinsi ya kutambua kusudi la Mungu ndani yako. Moja ya maswali yanayowatatiza watu wengi duniani na wameshindwa kujua ni wao kutambua makusudi ya wao kuishi katika dunia hii. Wengi wamekua wakiishi katika maisha ambayo sio yao halisi bali wamekua wakiishi kwa kuiga iga maisha ya wengine jambo ambalo ni janga kubwa kwa mkristo kua hivyo. Ila nipende kukutia moyo usikate tamaa kwa maswali uliyonayo hebu fatana nami katika somo hili mwanzo hadi mwisho na nina Imani kua utapata kitu kikubwa cha kukusaidia. NINI MAANA YA KUSUDI?? Watu wengi wameshindwa kuelewa maana halisi ya maisha yao jambo liliwapekea kuishi maisha ya wengine. Ngoja nikupe maana halisi ya kusudi KUSUDI  ~ Ni wazo au lengo lililowekwa ndani ya akili yako ili liwe kama malengo ambayo kwa hayo yataweza kuongoza maishani ili kutimiza lile ambalo Mungu ameweka katika maisha yako. Hebu tuangalie Zaidi katika Biblia inasema nini juu ...