Skip to main content

Posts

Showing posts from December 25, 2018

USHAURI WA WADAU WA JUKWAA LETU LA TUJENGANE MEDIA

Imeandikwa na mwanamke ambaye ameachika kwa mume wake na sasa anaishi peke yake na kulea mtoto Nimeandika kwenu  ili muweze kuelewa kuwa wakati mwingine ni vema kuwathamini Wenza wetu. Nina miaka 32, Mimi na mume wangu tulikuwa kwenye mahusiano kwa Muda wa miaka 6 na tulikuwa marafiki kabla hatujaoana, nilimsubiri mume wangu mpaka alipomaliza chuo, baadaye wazazi wakafahamiana na sisi tukafunga  ndoa na sasa tuna mtoto wa miaka 7.mume wangu Alikuwa ni mtu wa kukasirika haraka  lakini hayo yote yalianza baada ya mimi mwenyewe kutaka kumuonyesha kuwa hawezi kunitawala. Kila mara tulipogombana kidogo tu nilichukua mizigo yangu na kwenda kwetu kuelezea,dada yangu anachukua simu na kuanza kumpigia simu mume wangu na kumgombeza, na nilikuwa nikimtishia kuwa kama vipi nipe talaka yangu, huku Moyoni kiukweli simaanishi kweli kutaka talaka, nilikuwa naleta tu ufahari na kutaka kutoonekana nimeshindwa au Nina shida naye sana, siku moja kwa matendo yangu nilisababisha mpaka akan...

NUKUU KUELEKEA MWAKA MPYA

Binti yoyote  utambue kuwa kuna tofauti ya kuolewa na kujioa mwenyewe, sasa usiwe na haraka mpaka ukafikia hatua ya kuamua kujioa  maana huko ndani Jasho litakutoka, Mungu Anaweza asikupe ndizi moja Leo lakini kesho akakupa mkungu mzima wa ndizi hivyo kikubwa ni kuwa na subira na imani kwa Mungu, mfano kuchangia mahari au kujilipia mahari sio jukumu lako,  kuolewa na mtu asiye na Kazi au shughuli ya kufanya halafu weee ndio umhudumie kwa kuwa una kipato na umri unaenda na wenzio wameolewa Hilo pia hapana Hilo sio jukumu lako pia wewe ndio wa kuhudumiwa na kutunzwa pale msaada wako unapohitajika sawa ndio maana ukaitwa msaidizi na sio kichwa, kuolewa tu ilimradi na wewe umetoa gundu kuwa na mimi niliwahi Vaa shera kama wengine mnavyosema hata kama unajua kuwa mwanaume hakupendi ila una mimba yake na wazazi wamelazimisha ili usiwatie aibu Nyumbani wakati unajua kabisa ndoa yako itakuwa na mtikisiko mana mume hana upendo na wewe hivyo yajayo unayajua hilo pia sio kwakuwa kun...