Skip to main content

Posts

Showing posts from November 16, 2018

JINSI IMANI YA ELIMU INAVYO WATIA WATU UMASIKINI

Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa. 📚 Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏡 na 🚗 magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!). Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana. Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga. 1.Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe...

MSAADA UTOKAO KWA MUNGU JUU NA ALIYE HAI

MIAKA 2,000 hivi iliyopita, Paulo, mwandikaji wa Biblia alimfafanua Yehova kuwa “Mungu anayetoa uvumilivu na faraja.” ( Waroma 15:5 ) Kwa kuwa Biblia inatuhakikishia kwamba Yehova habadiliki kadiri wakati unavyopita, tunaweza kuwa na hakika kwamba bado Mungu anawafariji wale wanaomtumikia. ( Yakobo 1:17 ) Kwa kweli, Biblia inafunua kwamba Yehova anawafariji kwa njia mbalimbali wale walio na uhitaji. Ni njia gani hizo? Mungu anawatia nguvu wale wanaomwomba msaada kupitia sala. Pia, Mungu anawachochea Wakristo wa kweli kuwafariji waamini wenzao. Na Yehova ameweka katika Neno lake, Biblia, masimulizi yenye kutia moyo ambayo yanawatia nguvu hasa wale wanaoomboleza kifo cha mtoto. Acheni tuchunguze aina hizo tatu za faraja, moja baada ya nyingine. “Yehova Mwenyewe Akasikia” Mfalme Daudi aliandika hivi kuhusu Muumba wetu, Yehova: “Mtegemeeni nyakati zote. Mimineni moyo wenu mbele zake. Mungu ni kimbilio letu.” ( Zaburi 62:8 ) Kwa nini Daudi alikuwa na uhakika huo katika Yehova? Daudi alia...

USICHUKULIE CHUKI KWA KILA MTU

Ikiwa jamii inayokuzunguka itajinua na kukuongelea wewe katika maeneo tofauti na mienendo tofauti , ni lazima uchukue nafasi ya kujitathimini upya na kufanya toba za kila wakati juu ya hayo. wanadamu wakati mwingine huwa na taarifa za ishara ya kuharibikiwa kwako pia  mungu huwatumia wao kukufikishia ujumbe juu ya kukutaka ubadilike na uendane na kile ambacho yeye alikusudia ufanye hapa duniani. sio kwamba kila mwanadamu nayekwandama kutokna na mienendo yako anakutakia mabaya bali wengine huwa na nia njema. hupaswi kuchukia badala yake unapaswa kujielimisha juu ya hayo na kuwatumia kama wajuzaji wako.          ...................................