Nataka kukuambia kuwa hakuna ndoa iliyo kamili yaani perfect, na kama kuna mtu Anakwambia kuwa ndoa yake ipo perfect ujue huyo ni muongo mkubwa vinginevyo kama hao watu waliooana ni mazombi kwa maana nyingine siyo Binadamu, hata kama ni ya mchungaji wako, shehe wako au hata askofu wako wa jimbo . hata hao mnaoona wanatupia mapicha picha na wake zao au waume zao kuonyesha kuwa wapo happy Haimaanishi kuwa ndio Muda wote asubuhi mpaka jioni,jumatatu mpaka jumapili, January mpaka December wao ni kucheka tu hapana kiasi Kwamba ukaona kuwa ndoa yako haifai kabisa au upo kwenye Shimo, Kwenye ndoa watu kuna kukwazana, kupishana, hata kugombana kabisa wakati mwingine lakini kikubwa tunachotofautiana wengi ni namna ya kushughulikia hayo matatizo yanapojitokeza na kuishia kuharibu ndoa zetu wenyewe Katikati ya ndoa yenu nani mumemweka kama mhimili wenu ni Mungu au nani,? Wanaume kujaa ufahari kuwa mimi mwanaume Bwana siwezi omba msamaha, wanawake na wao husema Kwamba atanionaje ...
Karibu tuzungumze hapa ndipo kituo chako bora cha maarifa ,karibu useme, niseme, waseme na sisi tunasema 2018. ni sehemu pekee ya kila mmoja kutoa maoni yake na uwelewa wake juu ya kuelimisha jamii. ukiwa unachochote cha kutaka kutushirikisha kupitia jukwaa hili la wana jamii, usisite kututumia baraua pepe kwenda kwa bahatimagweiga467@gmail.com au wasiliana nasi kwa simu namba 0757472165, 0659991953. huduma zetu ni masaa 24