Skip to main content

Posts

Showing posts from April 29, 2019
Moja ya kitu ambacho kinakimbiza wateja dukani kwako ni kupokea mteja huku umekaa. Kinaua mood ya wateja wengi sana. Mteja ni kama mgeni,a napokuja dukani kwako uchangamfu wako ndiyo utamfanya kununua. Hembu jiulize umeenda kwa rafiki yako, umefika anakukaribisha anakuacha sebuleni anaenda kupiga stori nnje na watu wengine utaruudi? Sasa una duka mteja anakuja umekaa, anaulizia kitu flani umekaa unamuonyeshea kwa mkono tu au unamuambia ingia uangalie! Ndugu yangu labda kama unauza Oxygen kwamba nisiponunua nitakufa sirudi. Mteja akija kwako kwanza nyanyuka huku ukimkaribisha, akiulizia nguo flani nenda ishike, hata kama hutaki kuishusha lakini mgeukie muulize ni saizi gani, kama ni sahani muulize unataka rangi gani na chochote kile. Unaponyanyuka kuna mambo mawili yanatokea, kwanza anahisi unamhehsimu, anaanza kujiona kuwa kumbe na yeye ni wa muhimu anaheshimiwa, lakini pili anaanza kuona aibu, anaona kuwa huyu nisiponunua nitakua nimemsumbua. Lakini pia kuna kitu cha tatu kinatokea ...