Skip to main content

Bwana Yesu asifiwe nipende kukukaribisha tena katika somo langu jipya la jinsi ya kutambua kusudi la Mungu ndani yako. Moja ya maswali yanayowatatiza watu wengi duniani na wameshindwa kujua ni wao kutambua makusudi ya wao kuishi katika dunia hii. Wengi wamekua wakiishi katika maisha ambayo sio yao halisi bali wamekua wakiishi kwa kuiga iga maisha ya wengine jambo ambalo ni janga kubwa kwa mkristo kua hivyo. Ila nipende kukutia moyo usikate tamaa kwa maswali uliyonayo hebu fatana nami katika somo hili mwanzo hadi mwisho na nina Imani kua utapata kitu kikubwa cha kukusaidia.

NINI MAANA YA KUSUDI??
Watu wengi wameshindwa kuelewa maana halisi ya maisha yao jambo liliwapekea kuishi maisha ya wengine. Ngoja nikupe maana halisi ya kusudi

KUSUDI ~ Ni wazo au lengo lililowekwa ndani ya akili yako ili liwe kama malengo ambayo kwa hayo yataweza kuongoza maishani ili kutimiza lile ambalo Mungu ameweka katika maisha yako.


Hebu tuangalie Zaidi katika Biblia inasema nini juu ya kusudi la Mungu katika maisha ya mwanadamu aliyemuumba


Yeremia 1:4;10 4  Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5  Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Na ule mstari wa 10 10  angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.

Mungu anamwambia Yeremia kabla sijakuumba nalikujua kwa maana nyingine Mungu anajaribu kumwambia Yeremia kwamba nalitambua kabisa nilichokua nafanya pindi nilipokuumba. Ukiendelea ule mstari wa kumi hapo juu Mungu anamwambia maana halisi yay eye kumuumba yaani kusudi lake ni nini hasa kwa kumwambia Yeremia kwamba amemuweka kua nabii wa mataifa hivyo kusudi kubwa la Yeremia kuwepo duniani yamegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kusudi la kwanza Mungu anamwambia amemuweka kua nabii juu ya mataifa na kusudi la pili amewekwa kua juu ya mataifa na kazi yake halisi ni kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.

Lakini nikwambie siri kubwa iliyofichika hapa Mungu kabla hajamweka Yeremia kua nabii wake kwa mataifa kulishakua na kusudi ambalo Mungu alilokwisha kuliweka kabla ambalo aliliona kabisa halitaweza kufanikiwa pasipo kumuumba mtu ili alitimize.

Hivyo basi tambua kabisa kabla Mungu hajakuleta hapa duniani alikwisha kuumba kusudi lako ili uweze kuishi kwalo. Yaani wewe kuishi kwako sio kwa sababu ya kitu kingine ila unaishi duniani kutokana na kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako. Kwa maana nyingine ni kama hakuna kusudi hakuna mtu pia, maana Mungu hawezi kumuumba mtu bila kuweka kazi yake kabla ya kumuumba

KUWEPO KWAKO NI KWAAJILI YA KUSUDI AMBALO MUNGU ALILIUMBA HATA KABLA YAKO WEWE KUUMBWA; PASIPO KUSUDI HAKUNA MTU.
                                                     (No purpose no man)

Nipende pia kukwambia kua Mungu alimpa Yeremia uwezo hata kabla hajazaliwa ili aziangushe falme na huu uwezo si kwa ajili ya Yeremia ila ni kwaajili ya kusudi la Mungu. Jifunze hapa kuwa upo uwezo ulionao juu ya maisha yako si kwa sababu Mungu alikupa ili uwe wako ila ni kwaajili ya kusudi lake kwa maana Mungu hawezi kumpa mtu kusudi pasipo kumpa uwezo na mamlaka juu ya falme na mazingira anayoishi



TAMBUA NDANI YA KUSUDI LAKO UPO UWEZO NA MAMLAKA YA KUAMURU NA KUBADILISHA MAZINGIRA PINZANI JUU YA MAISHA YAKO NA HII SI KWA SABABU YA WEWE MWENYEWE ILA NI KWAAJILI YA KUSUDI LAKE MUNGU MWENYEWE.


Ngoja nikwambie kitu tambua kwamba mazingira unayoishi hata kabla hujazaliwa Mungu alishapanga uwepo hapo ili kufanikisha mpango wake mahali hapo.wengi wamekua wakiogopa mazingira wanayoishi kwa kuyaona ni magumu nipende tu kukwambia kwamba kukimbia mazingira unayoyaishi sasa sio njia ya wewe kufanikiwa  bali ni kukimbia kusudi na majukumu ambayo Mungu alikuumbia kwayo.

Mungu alifahamu kabisa mazingira ambayo atakuweka kwamba utakutana na falme na ngome za adui, anaelewa mapepo, vita ambavyo utapambana navyo, mapepo ambayo utambana nayo lakini nikwambie kabisa ni lazima ushinde iwapo utajifunza kuishi na kukaa ndani ya kusudi la Mungu haijalishi majaribu ni makali kiasi gani ila mwenye kusudi unao upako ndani yake hata kabla yay eye kuumbwa maana lilianza kwanza kusudi la Mungu ndani yake hata kabla yake, hivyo ndani yako ipo nguvu na uwezo ambao una uwezo wa kutosha kupambana na kila aina ya changamoto unazopitia.



Hebu anza kujiangalia sasa kwa upya tena katika maisha yako, vitu vinavyokuzunguka, vita pamoja na mapambano ya Ibilisi unayokumbana nayo kila siku hayataweza kukushinda ila utayashinda wewe, hayataweza kukumaliza bali utayamaliza wewe kwa sababu upo kwenye kusudi lake.


JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LAKO
pamoja na yote hayo niliyokufundisha apo awali hayataweza kukusaidia vizuri kama hadi sasa hujajua kusudi la Mungu juu ya maisha yako. Tunapokuja katika swala la kutambua kusudi lako sio kazi rahisi sana, wengi wetu wamekua wakifanya kila aina ya huduma lakini bado wanaona wanapwaya, wengine wamejaribu kufanya biashara lakini bado wanapwaya, kila wanachojaribu kukifanya katika maisha yao wanaona bado kuna kitu kinawadai  ambacho bado wanatakiwa kukifanya (kusudi) lakini pamoja na jitihada zao zote bado wameshindwa kujua ni nini hicho ambacho kimekosekana kwao


wengine wanaona kupata pesa pamoja na mafanikio ndio kujua kusudi lako kwenye maisha yako kitu ambacho si sahihi. Ngoja nikwambie pesa na mafanikio ni matokeo ya ujira baada ya mtu kufanya kazi Fulani aliyopewa. Hivyo huna haja ya kujisumbua sana juu ya hayo hebu anza sasa kutimiza kusudi lake kwanza ndani yako alafu utaona kama mungu hatalipia kusudi lake


KAMA UKITUMIKA KWA UAMINIFU JUU YA KUSUDI LA MUNGU KWAKO BASI KUA TAYARI KWA MAFANIKIO MAANA KUSUDI LA MUNGU KWAKO LINALIPA KWA YULE ALIYELITAMBUA NA KULIISHI.


Ili uweze kujua upo ndani ya kusudi la Mungu ni lazima kiwango cha Amani yako kiendane na kiwango cha kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako.
Ngoja nikwambie kwamba lipo jambo umewahi kulifikiria kulifanya au tayari umekwishalifanya na ukasikia Amani ndani ya moyo wako hata kama unaliona kama dogo tambua kua hilo ndilo kusudi la Mungu kwako, na uwe na uhakika si kwamba Mungu atakupa Amani peke yake bali atakupa pia uwezo, nguvu na mamlaka ya kuweza kupambana na mazingira unayoyapitia na hajalishi ni magumu kiasi gani lakini ni lazima utayashinda maana Mungu hakuumba kusudi ndani yako ili lishindwe.


KUSUDI LAKO LINATEGEMEANA SANA NA KIWANGO CHA AMANI UNAYOISIKIA MOYONI MWAKO NA KWA LOLOTE UNALOLIFANYA KWENYE MAISHA YAKO


Je unasikia Amani kiasi gani unapofanya ilo unalolifanya sasa? Kama kiwango cha Amani yako ni kidogo kwa unalolifanya sasa au hapo nyuma basi tambua bado hujatambua kusudi la Mungu ndani yako. Anza kubadilisha sasa ilo unalolifanya sasa ambalo linakunyima Amani na fanya kile ambacho unapata Amani moyoni mwako n ahata kama kwa mazingira ya nje watu wanaweza kuliona ni dogo we jitahidi kulifanya maana katika hilo Mungu ataanza kukubariki katika hilo.



Nipende tu kukwambia zipo hatua kuu mbili ili mwanadamu aweze kufikia makusudi ya Mungu kwenye maisha yake ambayo ni kama ifuatavyo;

1.      Ni lazima mwanadamu ampokee Yesu maishani mwake kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Ilo ndilo jambo kuu muhimu zaid katika maisha ya kila mwanadamu kwasababu unapompokea Yesu kwenye maisha yako huo ndio mwanzo wa wewe kutambua kusudi lako kwa maana Yesu ndiye aliyetuumba pamoja na Mungu baba (Mwanzo 1:26) sasa endapo tutarudi kwake kwa njia ya toba tutafungua mlango wa yeye kuingia ndani ya maisha yetu na kuanza kutufundisha nini kusudi lake katika maisha yetu. Kumbuka wewe hukujiumba wewe ila Mungu ndiye aliyekuumba na hakukuumba tu ila alikupa kazi na makusudi yaw ewe kuwepo ila kitu ambacho kimekupotezea kusudi lako ni dhambi unazofanya, hivyo basi hatua ya mwanzo ya wewe kutambua kusudi ni wewe kurudi kwa Mungu kwa njia ya toba ili Mungu aweze tena kukuonesha kusudi lako katika maisha yako ni lipi hasa.


Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHUMBA

Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba; Jambo la kwanza –    Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu 2Wakorinto 3:17  ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’. Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya. Kum...

VITU VYA MSINGI VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUDUMISHA UPENDO KATIKA MAHUSIANO

Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.” Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi. Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea, yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana. 1. Uaminifu Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote. Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako. Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano. Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli...

ZINGATIA HAYA UNAPOKUWA MBALI NA MWENZI WAKO

KAMA UKO MBALI NA MPENZI WAKO ZINGATIA HAYA Kama unaishi mbali na mpenzi wako kwanza kabisa unatakiwa kukubali kua mko mbali, huwezi na wala hutakiwi kucontrol kile anachokifanya kule, acha kufuatilia anafanya nini huko, yuko na nani na mambo kama hayo, kwa kfuupi wivu weka pembeni kwani ukiendekeza utachanganyikiwa. Kuna mambo mengi atayafanya mazuri na mabaya lakini kama hakuonyeshei basi huna haja ya kuyafukunyua. Jambo la pili ni mawasiliano haya ni muhimu na anapokupigia simu au unapompigia tumieni muda wenu vizuri kwa kuongelea kuhusu mapenzi na si kila siku “Mbona hukupokea simu yangu? Mbona nilikuona online hukujibu SMS zangu? Kulalamika sijui nimesikia hivi? Nimesikia vile!” Atakuvumilia kwa muda kisha itaboa na atakua anakwepa kuzungumza nawe na mwisho mapenzi yatakufa. Hata kama mnaongea dakika tano zifanyeni ziwe tamu zihusu mapenzi na si kuzozana mpaka mtu akitaka kupiga simu anawaza hivi nikiongea naye si kelele tu, hakuna mtu anapenda kupigia simu mtu aliyenuna....