Skip to main content

USHAURI KWA WATOTO WA KIKE #MSIPOTEE KABLA YA KUTIMIZA MAKUSUDI MAALIMU

JINSI BINTI ANAVYO WEZA KUEPUKA KUCHEZEWA NA KUPOTEZA NDOTO ZAKE KIMAISHA 

Wakati watu wawili mwanamke na mwanaume wanapokuwa kwenye kilele cha mapenzi, ni rahisi sana kila mmoja kuchunga kauli zake na kuongea yale ambayo yatamvutia mpenzi wake ili kila mmoja awe na mvuto kwa mwenzake na hivyo kuwa karibu zaidi. Hata hivyo watu wengi (hususan wanawake) wanashindwa kung'amua kwamba, katika mapenzi kila mmoja ana lake moyoni, na ni vigumu kujua mwenzako anawaza nini juu yako.
Katika mahusiano mara nyingi wanawake ndio huumizwa kwa sababu wakati mwingine mwanaume anapomtaka mwanamke humpa matarajio makubwa kuhusu hatima yao ili kumvuta, lakini kumbe analo lake moyoni na hapo ndipo mwanamke hujikuta akijitolea kwa hali na mali akijua kwamba, mwenzake amempenda na wataoana wakati kumbe mwenzie wala hana mpango huo.
Ni vyema kama mwanamke akiamua kujiingiza kwenye uhusiano, basi awe na uhusiano na mwanaume ambaye anaonekana dhahiri kuwa ni muoaji na si wa kumchezea tu, na kuingia mitini. Unaweza kujiuliza kuwa utamjuaje mwanaume muoaji na yule ambaye si muoaji bali wa kukuchezea tu.
Hapa chini nitaeleza baadhi ya mambo muhimu yatakayomuwezesha mwanamke kujua kama mwanaume aliye naye ni muoaji au anamchezea tu:
   1. Katika mazungumzo yenu ya kawaida jaribu kuzungumzia kuhusu maisha ya ndoa ili kuangalia kama yeye anayachukulia vipi. Wanawake wengi hukwepa kuzungumzia maisha ya ndoa na wapenzi wao kwa kuhofia kwamba wataonekana wanajipigia debe ili waolewe, lakini hili ni jambo muhimu sana kulijadili.
Kwa nini?
Kwa sababu ni muhimu kwa wapenzi waliopendana na kuaminiana kukaa na kujadili kuhusu matarajio ya kila mmoja ili kujua kama wako kwenye mustakabali mmoja au la. Kwa kujadili kuhusu jambo hilo kutawawezesha kujiwekea malengo ya namna ya kufikia matarajio yao. Iwapo mwanaume ataonekana kutovutiwa na mazungumzo hayo, basi hapo mwanamke ajue kwamba anachezewa na kama akiendelea na uhusiano huo, basi ajue kwamba, amekubali kuchezewa.
   2. Katu usijiaminishe kwamba kila mwanaume utakayekutana naye na kukutongoza na kukuahidi kukuoa kuwa huenda akawa ndiye mtarajiwa. Wanawake wengi wamekuwa na hamu kubwa ya kutaka kuolewa na wanayatamani sana maisha ya ndoa. Wanaamini kwamba kila mwanaume atakayemualika kuwa na mtoko naye hususan wa chakula cha mchana au usiku ndiye mtarajiwa. Lakini jambo ambalo wanawake wengi hawalijui ni kwamba si kila mwanaume anayevutiwa na yeye ni muoaji. Ni kujidanganya tu, si wote wenye nia thabiti ya kutaka kuoa. Kwao jambo la muhimu ni kutaka kuonja na kuacha.
     3. Ni vyema ukaangalia matendo yake zaidi kuliko maneno yake.
. Hii ni muhimu sana. Mwanaume anaweza kukwambia kwamba wewe ndiye chaguo lake atakayekuoa, na anaweza hata kukupeleka kwa Sonara au duka la kuuza pete za uchumba za dhahabu na kukununulia pete ya uchumba ya gharama, lakini kama hataanza kuchukua hatua muhimu za kukutambulisha kwao kwa ajili ya kupata Baraka za wazazi wake au kujitambulisha kwenu kwa ajili ya kupata Baraka za wazazi wako,Basi ujue kwamba hayo ni maneno matupu na katu hayavunji mfupa Hapo ujue kwamba huna chako bali unachezewa na iwapo utaendelea na uhusiano huo, basi umekubali kuchezewa.
   4. Kama mwanaume akiwa mkweli na kukueleza kwamba anakupenda lakini hana mpango wa kuoa hivi karibuni, usilazimishe kujenga uhusiano naye kwa nia ya kutaka kumshawishi ili akuoe. Kama kuna mambo ambayo mnaendana na umevutiwa kuwa naye karibu, si vibaya kujenga naye urafiki wa kawaida usiohusisha mapenzi. Lakini ni vyema kuwa makini kwani wakati mwingine urafiki wa kawaida na mwanaume unaweza kukufikisha mahali ambapo hukutarajia.
    5. Tengeneza aina ya maisha yatakayokutambulisha jinsi ulivyo na matarajio yako pamoja na msimamo wako kuhusu mahusiano. Hiyo itakufanya kujenga uzingativu kwenye matarajio yako na haitakuwa rahisi kwako kwenda kinyume na malengo uliyojiwekea hasa pale atakapojitokeza mwanaume atakayetaka kujenga mahusiano na wewe.
Ni vyema wanawake wakijua kwamba, ni rahisi kuingia katika mitego ya wanaume wakware. Kama hutaki kujiingiza kwenye uhusiano utakaokuumiza na kukusababishia maumivu makali moyoni, basi ni vyema kujua aina ya uhusiano ulionao na huyo mpenzi wako. Usikubali kabisa mtu kuchezea maisha yako.

   Imeandaliwa na bahati magweiga 
   Simu namba  0757472165
    Tigo simu namba 0659991953

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHUMBA

Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba; Jambo la kwanza –    Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu 2Wakorinto 3:17  ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’. Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya. Kum...

VITU VYA MSINGI VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUDUMISHA UPENDO KATIKA MAHUSIANO

Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.” Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi. Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea, yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana. 1. Uaminifu Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote. Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako. Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano. Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli...

ZINGATIA HAYA UNAPOKUWA MBALI NA MWENZI WAKO

KAMA UKO MBALI NA MPENZI WAKO ZINGATIA HAYA Kama unaishi mbali na mpenzi wako kwanza kabisa unatakiwa kukubali kua mko mbali, huwezi na wala hutakiwi kucontrol kile anachokifanya kule, acha kufuatilia anafanya nini huko, yuko na nani na mambo kama hayo, kwa kfuupi wivu weka pembeni kwani ukiendekeza utachanganyikiwa. Kuna mambo mengi atayafanya mazuri na mabaya lakini kama hakuonyeshei basi huna haja ya kuyafukunyua. Jambo la pili ni mawasiliano haya ni muhimu na anapokupigia simu au unapompigia tumieni muda wenu vizuri kwa kuongelea kuhusu mapenzi na si kila siku “Mbona hukupokea simu yangu? Mbona nilikuona online hukujibu SMS zangu? Kulalamika sijui nimesikia hivi? Nimesikia vile!” Atakuvumilia kwa muda kisha itaboa na atakua anakwepa kuzungumza nawe na mwisho mapenzi yatakufa. Hata kama mnaongea dakika tano zifanyeni ziwe tamu zihusu mapenzi na si kuzozana mpaka mtu akitaka kupiga simu anawaza hivi nikiongea naye si kelele tu, hakuna mtu anapenda kupigia simu mtu aliyenuna....