USIHARAKISHE.
Usiharakishe na kukurupuka kutafuta mchumba kabla ya wakati muafaka.Pengine unaweza kujiuliza ni wakati upi ni muafaka kutafuta au kuwa na mchumba?ni wakati unapokuwa umekomaa kiroho, kiakili na kimwili umejitambua kikamilifu ulikotoka, mahali ulipo na unapokwenda na umetathimini kwa makini mipango na ratiba yako ya sasa na ya baadaye ndipo waweza kuchukua hatua hii mhimu katika maisha.
Wengi wamepuuzia hili na kukurupuka kutafuta mchumba bila kujitathmini na kuishia kwenye uasherati na usaliti vilivyowaletea huzuni na majuto badala ya furaha na ndoa takatifu. Biblia inasema “Ni nani katika ninyi Kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kumalizia asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi watu wote waonao wakaanza kumdhihaki…….” (Luka 14:28-30).
USITAFUTE MCHUMBA KWA MSUKUMO KUTOKA NJE.
Usitafute mchumba Kwa kuangalizia, kushawishiwa, kuiga au kusukumwa na ndugu, marafiki au washiriki wenzako, suala la kutafuta mchumba linapaswa kutoka ndani yako baada ya kujithamini na kuona kuwa ni wakati mwafaka na kupata sababu za msingi za kupata mchumba hatimaye kufunga ndoa.
USITAFUTIWE MCHUMBA.
Vijana wa kiume na wa kike wanatakiwa kuwa makini sana katika suala hili, yakupasa uwe na orodha yako ya sifa unazozitaka, cha msingi zisipingane na neno la MUNGU, hizo zitakuongoza katika kutafuta mke au mme utayempenda na kumfurahia, fanya maamuzi ambayo hutakuwa na sababu ya kumfurahia mwingine.
Ushauri wa ndugu, jamaa, marafiki na vio
ngozi wa kanisa unafaa kuzingatiwa kwa makini,lakini maamuzi ya mwisho yatoke kwa mhusika ambaye ataambatana na huyo mwenzi maisha yote, wengi wametafutiwa na kuishia kulaumu na kuvunja uchumba na hata ndoa.
USIFANYE UCHUMBA WA SIRI.
Uhusiano kati ya kijana wa kiume na wa kike
waliopendana, waliokubalian kuoana huitwa uchumba baada ya vijana hao waliokubaliana kuwajulisha wazazi wa pande zote mbili na ikibidi viongozi wa kanisa. Kuendesha mahusiano ya siri siri kunafananishwa na Nabii sawa na dhambi ya wizi, kuiba upendo wa msichana, kwa kweli kitendo hiki hakikubaliki kabisa na si chema kwa binti mwenyewe, kwa wazazi na hata mbele za MUNGU “mvulana ampendaye msichana …. Bila kujulikan kwa wazazi wa msichana hafanyi tendo jema kwa msichana mwenyewe wala kwa wazazi wake. Kwa kweli hata hafanyi kitendo chema cha kikristo madhara ya uchumba wa siri ni pamoja na kuvunja uhusiano wenu na MUNGU, kukosa ushauri wa wazazi na viongozi wacha MUNGU, kufasiriwa vibaya na watu wanaowaona na kujiingiza katika vitendo viovu vya uasherati kwa urahisi. Hivyo mara baada ya kukubaliana, ni muhimu kutoa taarifa kwa wazazi na uongozi wa kanisa.
USIWE NA WACHUMBA WENGI.
“Ajifanyiae rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe……..” (Mithali 18:24). Utafiti unaonyesha kuwa vijana wengi wa kiume na wa kike wakristo huwa na wachumba wengi kwasababu kwa sababu zifuatazo, kwanza kutokuwa na uhakika kuwa yupi mchumba wa kweli, pili ni kutaka kupata umaarufu, tatu ni tamaa na nne ni kutaka vya bure na tano ni kukurupuka. Hiyo siyo tabia njema kwa kijana mkristo, kuwa na wachumba wengi kuna madhara makubwa. mfano kuwa mdanganyifu ili kuwaridhisha wote, kusababisha ugomvi na hata kuuana miongoni mwa wa wapenzi wako, wakigundua wote waweza kukuacha, lakini pia ni kuwapotezea muda wengine.Mungu hapendezwi na mwenendo huo hata kidogo,uovu huu usipoachwa, utajitokeza tena katika maisha ya ndoa baada ya harusi muombe MUNGU kwa imani uwe naye mmoja tu kwa wakati na inaposhindikana, tulia mwombe MUNGU naye atatuongoza mahali sahihi.
USIOMBE UCHUMBA KWA MAJARIBIO “KUUDHIHAKI MOYO”
‘Kudhihaki ni kosa ambalo halina upungufu wowote machoni pa MUNGU mtakatifu. Ingawa ni hivyo wengi huonyesha wasichana mapenzi na kuamsha upendo wao na baadaye wakaenda zao bila kujali Waliyonena na bila kufikiri maneno yao yatakuwa na matokea gani kwa yule msichana. Wanapokuwa wakitangatanga huko na huko huona sura mpya…. Na kuamsha mapenzi ya msichana mwingine hali kadhalika wakaenda na kumsahau pia. Vile vile wako wasichana wenye mienendo kama hiyo huu ni ouvu mbele za MUNGU, wengi wamejinyonga na kunywa sumu kwa sababu ya dhihaka za vijana ambao hawakua na dhamira ya dhati, waliotamka nakupenda kwa majaribio au kwa lugha inayotumiwa na vijana kujipima uzito, kisha wakaenda zao. Hebu kijana usiombe uchumba ikiwa huja dhamiria, wala usiombe uchumba bila kupenda au kwa kumsaidia msichana ama kumkubali kijana kwa kumsaidia au kwa majaribio, hiki si kitendo chema kabisa kwa anayetendewa na mbele za MUNGU.
USIWE MWONGO, MUELEZE UKWELI WOTE KUHUSU WEWE.
“Nao ulimi ni moto, ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi umewekwa katika viungo vyetu na ndio uutiao mwili wote unajisi; huuwasha moto mfululizo wa umbile nao huwashwa moto wa jehanamu” (Yakobo 3:6) kama kuna kitu kinachoweza kuteketeza uchumba wako ni uongo na usengenyaji. Vijana wengi hutafuta mchumba kwa uongo kwa kujipatia sifa au hadhi zisizo za kweli na kuficha baadhi ya mambo mhimu yanayowahusu, uwe wazi kwa mchumba wako au kijana anayetarajia awe mchumba wako.Ikiwa una mtoto au ulishawahi kuoa au kuolewa.Mueleze mipango au njozi zako za baadaye ili anapofanya maamuzi ya kuwa na wewe awe ameridhika na awe tayari kuwa na wewe jinsi ulivyo, huu ndio msingi wa upendo wa kweli.
EPUKA VITENDO VINAVYOWEZA KUTAFSIRIWA VIBAYA
Biblia inasema “sisi ni barua iliyoandikwa na kusomwa na watu wote”(2kor 3:2-3), kwa kuwa sisi ni barua ya MUNGU kwa watu wanao tuzunguka imetupasa kuepuka vitendo vyote vinavyoweza kutufanya tusomeke vibaya.Miongoni mwa vitendo hivyo ni kukaa mazingira ya kificho mfano gizani,chumbani au vichakani, watu wakiwaona wanawatafsiri vibaya na hivyo kuwazuia kumuona kristo katika maisha yenu,pamoja na hayo mazoea haya ndio chanzo kikubwa kuelekea katika uzinzi na uasherati .Kitendo kingine ni kuwa pamoja kila wakati ,ninyi sio mume na mke,huu sio wakati wake, kitendo hiki husababisha vijana kuzama katika mapenzi mazito kabla ya wakati,na hivyo huwa vipofu wa mapenzi,hiki nacho ni kichocheo kikubwa cha ngono kabla ya ndoa,kitendo kingine ni maongezi usiku wa manane, tabia hii haimpendezi mungu,saa za usiku ni saa za kumpumzika,kukesha usiku kucha kwa ajili ya maongezi kunadhuru afya yenu vilevile,madhara yake ni pamoja na kudhoofu ubongo,uchovu mwingi na hivyo kufanya hata ufanisi wa kazi zako upungue,pia kitendo hiki huamsha tama za mwili na mwisho kutumbukia katika zinaa na uasherati,na ukiwa unazungumza chumbani unakera wengine na wanakutafsiri vibaya.Tabia nyingine ni kutumia pesa au zawadi nyingi ili kuimarisha uchumba au kupata mchumba,kitendo hiki pia si mpango wa MUNGU,uchumba unapaswa kujengwa katika msingi wa upendo wa kweli na si vitu.Tabia hii husababisha upofu wa mapenzi hivyo mambo muhimu hupuuzwa na wengi hujitumbukiza katika uhusiano wa ndoa na watu wasiofaa.
EPUKA ZINAA NA UASHERATI.
“Azinie na mwanamke hana akili kabisha (Mithali 6:32), Vijana wengi hudhani ngono kabla ya ndoa ni ujanja na huimarisha uhusiano wao.Lakini hiki ni kitendo kinacho haribu kabisha uhusiano wako na mwenzi wako na uhusiano wenu na mungu.Aidha uzinzi na uasherati unamadhara na hasara zake hasa kwa wasichana.Baadhi ya hasara wazipatazo wasichana ni kama zifuatazo:
Kupata mimba nje ya ndoa (mimba sizizotarajiawa), kukakataliwa na wachumba wao,kuharibu uwezakano wa kupata mchumbamwingine tena,vifo kwa sababu ya kujaribu kutoa mimba walizo pata bila ya kutegemea,kupoteza heshima katika jamii,kuvunja uhusiano wao na MUNGU n.k Sasa kwa nini usiepuke mambo haya kwa kuwa mwaminifu?
USICHUMBIE MTU WA IMANI TOFAUTI NA WEWE.
“Msifungiwe nira na wasioamini kwa jinsi isivyo kawaida” (2 kor 6:14),kuonana na kijana mwenye imani tofauti na wewe kunaleta migogoro mizito na isiyokoma katika maisha ya ndoa.Mungu amezuia jambo hili tangu zamani ,akawaelekeza waisraeli taifa lake teule wakati ule alisema “wale msioane nao, binti yako usimpe mwanawe mume, wala msimtwalie mwanao mume binti yake (kumb 7:2,3).Sababu yake Mungu anasema “kwa kuwa atamkengeusha mwanao asimfuate Mungu ili wapata kuabudu miungu mingine(kumb 7:4) Vijana wengi wameyapuuza maagizo haya mema na kuongozwa na tama za mioyo yao kama ilivyokuwa kwa Samsoni(waamuzi 14: ) wengine wakidai watawaongoa , huku ni kujidanganya ,Suleimani alikuwa na hekima kuliko watu wote wa wakati wake na wakati huu, alifanya kosa hilo hilo akitaka kuongoa mataifa yaliyomzunguka kwa kuoa binti zao lakini mwisho aliishia anguko kuu la kiroho na kugeukia miungu yao “Suleimani akawapenda wanawake wengi wageni nao wakaugeuza moyo” (1fal 11:)kama Suleimani alishindwa, vipi wewe?, anaweza kukubali ili kukuridhisha na kukupata wewe lakini kwa hakika huo sio uongofu wa moyoni na matokeo yake utayashuhudia baadaye.Ndoa zimegeuka kuwa mahabusu na jela ndogo,migawanyiko ya imani,malumbano yasio koma,ugomvi usio koma, kwa sababu watu wawili wenye itikadi na falsafa mbili tofauti waliunganishwa kwa ndoa bila ya kujali mausia ya neno la Mungu.Kijana ikiwa uliingia katika mausiano ya namna hii bila kujua au kwa kujua kwa neema ya yesu na hekima ya mbinguni vunja uhusiano huo mara moja
TUTAENDELEA..................................................................................
Comments
Post a Comment
asante kwa kuichagua tujengane media kuwa sehemu yako ya kujifunza