Skip to main content
Moja ya kitu ambacho kinakimbiza wateja dukani kwako ni kupokea mteja huku umekaa. Kinaua mood ya wateja wengi sana. Mteja ni kama mgeni,a napokuja dukani kwako uchangamfu wako ndiyo utamfanya kununua. Hembu jiulize umeenda kwa rafiki yako, umefika anakukaribisha anakuacha sebuleni anaenda kupiga stori nnje na watu wengine utaruudi?
Sasa una duka mteja anakuja umekaa, anaulizia kitu flani umekaa unamuonyeshea kwa mkono tu au unamuambia ingia uangalie! Ndugu yangu labda kama unauza Oxygen kwamba nisiponunua nitakufa sirudi. Mteja akija kwako kwanza nyanyuka huku ukimkaribisha, akiulizia nguo flani nenda ishike, hata kama hutaki kuishusha lakini mgeukie muulize ni saizi gani, kama ni sahani muulize unataka rangi gani na chochote kile.
Unaponyanyuka kuna mambo mawili yanatokea, kwanza anahisi unamhehsimu, anaanza kujiona kuwa kumbe na yeye ni wa muhimu anaheshimiwa, lakini pili anaanza kuona aibu, anaona kuwa huyu nisiponunua nitakua nimemsumbua. Lakini pia kuna kitu cha tatu kinatokea na hiki ni chamuhimu zaidi, unaponyanyuka unamlazimisha kukaa  dukani kwako kwa muda zaidi ili kuangalia vitu vingine.
Labda nikupe mfano tu, mteja kaja anaulizia una Lotion za Nivea, wewe huna kabisa, sasa kwa mtu ambaye hajui Biashara atasema sina akiwa kakaa anaendelea kuchezea simu yake akifuatilia sijui kama yale magari ni ya Zari au kakodi! Lakini kwa mfanyabiashara anajua kabisa kuwa hana Nivea ila atanyanyuka, ataenda kwenye shelfu la Lotion ataangalia kisha atasmea “Hizo zimetuishia ila tuna Nice and Lovely….”
Anageuka kidogo anamuangalia ngozi yake anauliza “Unapaka ya ngozi kavu au …” hapo mhusika hata kama haitaki lakini lazima akae kujibu lile swali kwakua umeuliza kistaarabu, ataangalia angalia na kutafuta kingine na hata asiponunua siku hiyo atarudi tena kwakua ulimuonyesha ukarimu. I;a mtu anakuja dukani, unakuta lijitu limenuna, au yuko bize na simu utafikiri kachanjiwa unaingia na kutoka hata hageuki halafu unaishia kusema “Huyu si mnunuaji?”
Yaani huwa nashangaa mtu mwingine analalamika wiki hajauza lakini anakuja huyo mtena mmoja anaacha kuweka simu pembeni akamhudumia unaacha kunyanyuka kumhudumia vizuri mpaka atamani kurudi tena! Kusimama mtena anapokuja kuna nguvu kubwa sana katika kumrudisha mteja, usijali ni wa namna gani simama tu hizo dakika tano ataona umemheshimu, fanya hivyo utanishukuru baadaye utakapotengeneza wateja wakudumu!

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...