Skip to main content

MAHITAJI MUHIMU KABLA YA KUWEKA VIFARANGA BANDANI.

 MAHITAJI  MUHIMU KABLA YA KUWEKA VIFARANGA BANDANI :

Unapotaka kuanza ufugaji wowote wa kuku lazima uwe na mahitaji muhimu ya kusaidia muradi wako ukuwe vyema na kuepukana na changamoto.  

Miongoni mwa mambo muhimu ni kama vile. 

1. Banda kulingana na idadi ya vifaranga unavyotaka kuweka.  Usizidishe vifaranga katika banda moja ili kuepusha ukuaji hafifu na matatizo mengine kama vile kudonoana.  Hakikisha banda limezingatia kanuni zote za ujenzi ikiwemo 

✔️uelekeo wa upepo 

✔️upauwaji wa paa

✔️uelekeo wa maji yani lisiwe katika mkondo wa maji 

✔️Hewa iingie na kutoka kwa usahihi ili kuzuia mambukizi zaidi ya magonjwa pale yanapokuwa yametokea. 

2.  Vyombo vya chakula na maji kulingana na Idadi sahihi ya vifaranga.  Kwa mfano vifaranga 100 wanahitaji Vyombo 3 vya maji na vitatu vya chakula ndani ya siku 30 mpaka 45

3. Vyungu joto au taa za umeme za kulelea vifaranga 

4. vitaru vya kulelea vifaranga endapo banda ni kubwa.  Unaweza kutengeneza buruda ili kusaidia kuzuia upotevu wa joto bandani na usambaaji wake. 

5.Dawa  za kuanzishia  ( Neoxchick )

6. Glucose . endapo vifaranga watakuwa wametoka umbali mrefu wanatakiwa kupewa glucose kwa masaa 3 ili kuwaongezea nguvu na kuchangamka kwajili ya kuanza kula.  

 Katika mchanganuo huu hakuna sehemu nimetaja madawa yenye mlengo wa kutibu magonjwa.  Sio rahisi kuzungumzia madawa kwa sababu huwezi kufahamu vifaranga wataumwa nini na watatumia dawa zipi na watapona baada ya muda gani.  

Kuna wakati vifaranga wanaumwa na kujikuta wametumia dawa zaidi ya 3 kwenye ugonjwa mmoja kulingana na ukubwa wa tatizo.  

Jambo la muhimu ni usimamzi bora na kufuata sharia zote za ufugaji.

Pia Elimu dhidi ya utambuzi wa magonjwa na kinga dhidi ya magonjwa ni muhimu zaidi kuwa nayo.  

Jenga utaratibu wa kukagua maendeleo ya vifaranga wako Mara kwa Mara ili ubaini changamoto zikiwa katika hali ya kawaida ambayo Unaweza kukabiliana nayo.  

Niwatakie ufugaji mwema na siku njema. 

 By  Bahati magweiga. 

Wasiliana Nami kwa huduma zetu za vifaranga wa siku 1 aina ya kroila.  

 0757472165 

0786155188

E-mail bahatichacha698@gmail.com 

Pia Tunatoa mafunzo ya kutotolesha vifaranga kwa kutumia mabox ambayo huduma hiyo hufanyika online kwa garama nafuu kabisa.  Tupo kibaha pwani.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...