Skip to main content

WANAWAKE WENGI HUFUNGA NA KUOMBA WANAUME WA NAMNA HII.



Ndugu zangu, nimeongea kuhusu baraka na heri ya kuwa na mwanamke wa pekee pia ni vizuri kwa wakina dada na wanawake kutambua kuwa nao wanatamani sana kuwa na mume wa namna hii. Hii pia ni namna moja ya sisi wanaume kujidai katika ndoa zetu. Mke huyu ana heri anapompata mume wa namna hii:
1️⃣ Mume anayemjua Mungu na anaishi maisha ya kumpendaza Mungu.
2️⃣ Mume anayetambua kuwa yeye ni baba wa familia, mume wa ndoa na mlinzi wa familia.
3️⃣ Mume anayejua kuwa mke wake anatakiwa kusikiliza na siyo kukaripia na kugombezwa kama mtoto na wakati mwengine kutamkiwa maneno makali mbele ya watoto.
4️⃣ Mume ambaye ana uwezo wa kujishusa pale anapofanya kosa, anapoumiza hisia za mke wake.
5️⃣ Mume ambaye anatambua ulimwengu wa mwanamke na anatambua mahitaji ya mke wake.
6️⃣ Mume ambaye anashirikisha mambo ya familia na ndoa kwa mke wake na wanapanga mipango mbalimbali ya familia kwa pamoja.
7️⃣ Mume ambaye anatambua kuwa ni wajibu wake kuwa na muda wa pekee wa kuwa na mke wake, kama vile outing au wenye uwezo basi mtoko wa kwenda mahali na kupumzika angalau hata mara moja kwa miezi kadhaa au kwa mwaka.
8️⃣ Mume ambaye anakumbuka siku maalum za mke wake na kumuenzi, kumpetipeti mke wake kama mtoto au "baby". hili ni la muhimu sana kwa wanawake.
9️⃣ Mume anayetambua kuwa ana wajibu wa kumsaidia mke wake hata kazi ndogo-ndogo za nyumbani muda unaporuhusu.
🔟 Mume ambaye anatambua malezi siyo kazi ya mke wake peke yake, bali kwa pamoja wanasimama imara kulea watoto.
1️⃣1️⃣ Mume ambaye anajivuania kuwa na mke wake na siyo kuona hata shida kumtambulisha au kuongozana naye.
1️⃣2️⃣ Mume ambaye ana nia ya maendeleo na katika maendeleo anajua mke wake ni nguzo muhimu ya wao kufikia malengo ya familia.
1️⃣3️⃣ Mume ambaye habadiliki kutokana na pesa nyingi anazopata, bado ni mwaminifu kwa mke wake na muwazi kwa kila jambo.
1️⃣4️⃣ Mume ambaye anampenda mke wake akiwa ni maskini na hata kama ni tajiri anatambua yote hayo ni baraka zao pamoja.
1️⃣5️⃣ Mume ambaye anafurahia mafanikio ya mke wake na pia kumtia moyo mke wake anapokutana na changamoto, zinakuwa zao wote.
1️⃣6️⃣ Mume ambaye kipato chake siyo siri yake, hana account za siri, kw sabau chochote anachopata anafahamu ni kwa ajili yao kwa pamoja katika familia.
1️⃣7️⃣ Mume anayetambua kuwa mapenzi na mahaba katika ndoa yanahitaji maandalizi mazuri hasa kumwanadaa mkewe na siyo kukurupuka na kumrukia na akimaliza shida zake anageuka pembeni kulala.
1️⃣8️⃣ Mume ambaye anatambua kuwa anaweza kujifunza na kuelemisha mambo mbalimbali na mke wake, siyo kumdharua kwa kila jambo. Mume ambaye anaona mazuri kwa mke wake, na pia kumsifia mke wake. Wanawake wanapenda kusifiwa na kutambuliwa

Mungu nijaalie mke mwema.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...