Skip to main content

USHAURI WA WADAU WA JUKWAA LETU LA TUJENGANE MEDIA

Imeandikwa na mwanamke ambaye ameachika kwa mume wake na sasa anaishi peke yake na kulea mtoto

Nimeandika kwenu  ili muweze kuelewa kuwa wakati mwingine ni vema kuwathamini Wenza wetu.

Nina miaka 32, Mimi na mume wangu tulikuwa kwenye mahusiano kwa Muda wa miaka 6 na tulikuwa marafiki kabla hatujaoana, nilimsubiri mume wangu mpaka alipomaliza chuo, baadaye wazazi wakafahamiana na sisi tukafunga  ndoa na sasa tuna mtoto wa miaka 7.mume wangu Alikuwa ni mtu wa kukasirika haraka  lakini hayo yote yalianza baada ya mimi mwenyewe kutaka kumuonyesha kuwa hawezi kunitawala. Kila mara tulipogombana kidogo tu nilichukua mizigo yangu na kwenda kwetu kuelezea,dada yangu anachukua simu na kuanza kumpigia simu mume wangu na kumgombeza, na nilikuwa nikimtishia kuwa kama vipi nipe talaka yangu, huku Moyoni kiukweli simaanishi kweli kutaka talaka, nilikuwa naleta tu ufahari na kutaka kutoonekana nimeshindwa au Nina shida naye sana, siku moja kwa matendo yangu nilisababisha mpaka akanipiga sana na kunifungia nje, nikaenda kwetu kama kawaida na familia yangu wakampeleka polisi, na kila wakati ilikuwa inaonekana kama  mimi ndio ninaonewa na kuteswa na mume wangu ila ukweli mimi ndio niliyekuwa namnyanyasa mume wangu kihisia.wakamkamata na kumuweka ndani na mimi nikaambwa sana na ndugu Zake kuwa nifute kesi aachiwe. Baadaye nikajifikiria kuwa mm ndio Nina makosa mume wangu hakuwa mgomvi kabisa nilimsukumia mume wangu ukutani mpaka akaanguka Chini na bado aliamka na kuomba msamaha. Nikafuta kesi na tukayamaliza,  baada ya miezi 3 Nikafunga vilago vyangu na kuondoka tena sababu ya kitu kidogo tu ambacho tungeweza kukimaliza na kumuacha peke yake, baada ya siku 2 nilipata simu kuwa mume wangu yupo hospitali, familia yangu ikaniambia kuwa nisiende kumuona itaonekana kama nambembelezaa na dada zangu wakahisi anajifanyisha ugonjwa, na wakati wote huo watu walikuwa wananionea Huruma kama vile ninateseka kwenye ndoa yangu, alikaa hospitali wiki nzima na baada ya kutoka nilipokea  barua ya kutaka kuachana, nilitaka kukata ila sababu ya kiburi changu kitakatifu nikajua  atabadili mawazo tu na kunibembeleza, nikampigia simu na kusema bora tuachane maana hata mimi naona kama niko Jehanamu.

Tulipokutana mahakamani nikataka kumkomesha nikaiambia mahakama kuwa nataka tugawane kila kitu tulichochuma wote na kwa mshangao wa Ajabu na yeye akaiambia mahakama kuwa chochote ninachotaka nipewe tu anachotaka yeye ni kuachana tu . tuliachana mwaka 2009 mwezi wa 6,  sasa hivi mume wangu ameoa mwanamke mwingine na mimi nipo tu nimeharibikiwa na ndugu zangu wamenigeuka na kunicheka na sasa  ninaishi kwa kutegemea hela za mtoto za matumizi anazopewa mwanangu na baba yake, najua nimepoteza ndoa yangu mwenyewe,

 Nipo hapa kukuambia wewe mwanamke uliyeolewa kuwa makini sana na ushauri unaopewa,  usiruhusu  ndugu au wazazi  hata marafiki  waingilie ndoa yako, sasa hivi hata wadogo zangu ndio Wanaheshimika zaidi kuliko mimi, wote waliokuwa wananipa moyo niachane na mume wangu walikuwa wananijaza upepo kinafiki na sasa Wamenikimbia na kuniacha peke yangu naangaika.

Share ujumbe huu kama umekubariki ili kunusuru ndoa Zingine, Mara nyingine huwa sio makosa ya mwanaume bali ni ujinga wetu na kiburi..hivyo kuna cha kujifunza kama mwanamke

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...