Skip to main content

NUKUU KUELEKEA MWAKA MPYA

Binti yoyote  utambue kuwa kuna tofauti ya kuolewa na kujioa mwenyewe, sasa usiwe na haraka mpaka ukafikia hatua ya kuamua kujioa  maana huko ndani Jasho litakutoka, Mungu Anaweza asikupe ndizi moja Leo lakini kesho akakupa mkungu mzima wa ndizi hivyo kikubwa ni kuwa na subira na imani kwa Mungu, mfano kuchangia mahari au kujilipia mahari sio jukumu lako,  kuolewa na mtu asiye na Kazi au shughuli ya kufanya halafu weee ndio umhudumie kwa kuwa una kipato na umri unaenda na wenzio wameolewa Hilo pia hapana Hilo sio jukumu lako pia wewe ndio wa kuhudumiwa na kutunzwa pale msaada wako unapohitajika sawa ndio maana ukaitwa msaidizi na sio kichwa, kuolewa tu ilimradi na wewe umetoa gundu kuwa na mimi niliwahi Vaa shera kama wengine mnavyosema hata kama unajua kuwa mwanaume hakupendi ila una mimba yake na wazazi wamelazimisha ili usiwatie aibu Nyumbani wakati unajua kabisa ndoa yako itakuwa na mtikisiko mana mume hana upendo na wewe hivyo yajayo unayajua hilo pia sio kwakuwa kuna watu walipata mimba lakini baadaye wakaja kuolewa na mtu  mwingine mwenye upendo hivyo sio Mwisho wa maisha  , na vitu vingine utajiongeza, kuna mtu atakuwa kanielewa hapo, maana  2019 hiyo inakuja usiseme sikukuambia Japo vijana wengi wa mteremko hawataipenda hii najua ila ndio ukweli wenyewe huo

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...