Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2019

UTAJUAJE MTU ANAYE KUSARITI?

Kama mtu anachepuka au anakusariti lazima kutakuwa na dalili au viashiria  kadhaa kwake Dalili za kujua mtu anaekusaliti 1. mwanandoa anayetoka nje ya ndoa hana muda wa kusikiliza familia ina tatizo au furaha gani. Anafafanua kuwa hiyo inatokana na muda wote kufikiria mambo ya familia nyingine hata kama ni ya mtu huko alikoanzisha uhusiano. 2. Kuchukia kushiriki tendo la ndoa Anasema wengi wao hufanya mapenzi na wenza wao kwa kujilazimisha na wakati mwingine kulazimishwa kwa uwazi kabisa 3. mwenza anayetoka nje ya ndoa muda mwingi anakuwa mtu wa safari za ndani au za nje ya eneo analoishi. 4. anayechepuka anakuwa makini na simu zaidi ya kawaida, yupo radhi aende nayo bafuni, anakuwa makini asikamatwe anayochat kwenye simu. 5. kuchelewa kurudi nyumbani nk. Tutaendelea kuangazia dalili mbalimbali za mtu anayekusariti 5. Kuongeza upendo ghafla: mwanaume anapoanza kutoka nje yandoa, kama ndoa yake haina vurugu , anaweza kuonesha upendo mkbwa hadi mkewe akashangaa na kujiuliza....

UNACHOTAKIWA KUFANYA BAADA YA KUSARITIWA / KUKATALIWA NA MWENZI WAKO

Watu wengi hukosea katika mahusiano  kwa kutokuwa  wavumilivu pale wanapoachwa au kusaritiwa.  Wengi huwahi sana kuingia kwenye mahusiano ikiwezekana siku moja baada ya kuachwa na mpenzi wake.  Ukweli ni kwamba huwezi kupatia katika mahusiano kama hujafanyia kazi sababu na changamoto zilizo mfanya huyo mwanaume au mwanamke akukimbie .wengi husema lengo ni kuziba magepu na kupunguza stresi lakini ukweli ni kwamba baada ya mchungu kuisha utarudia makosa yale yale  ya mwanzo.  Unachotakiwa kufanya baada ya kusaritiwa au kukataliwa na mpenzi wako ni........ 1. Jitathimini kwanza 2. Jifikirie kwa kina sana ili kubaini ukweli wa kusaritiwa au kukataliwa kwako. 3. Punguza jaziba na hasira zako kwani zinaweza kukufanya ukaumia zaid pale unapo ongea na aliyekusariti. 4. Punguza kumwambia kila mtu juu ya kuumizwa kwako 5. Jitahidi kusahau . Ukizingatia hayo itakuwa rahisi sana kufika mbali kimahusiano na kufanya chaguo sahihi la mwenzi wako. Ukiendelea kuingia...