Skip to main content

UTAJUAJE MTU ANAYE KUSARITI?

Kama mtu anachepuka au anakusariti lazima kutakuwa na dalili au viashiria  kadhaa kwake
Dalili za kujua mtu anaekusaliti
1. mwanandoa anayetoka nje ya ndoa hana muda wa kusikiliza familia ina tatizo au furaha gani. Anafafanua kuwa hiyo inatokana na muda wote kufikiria mambo ya familia nyingine hata kama ni ya mtu huko alikoanzisha uhusiano.
2. Kuchukia kushiriki tendo la ndoa
Anasema wengi wao hufanya mapenzi na wenza wao kwa kujilazimisha na wakati mwingine kulazimishwa kwa uwazi kabisa
3. mwenza anayetoka nje ya ndoa muda mwingi anakuwa mtu wa safari za ndani au za nje ya eneo analoishi.
4. anayechepuka anakuwa makini na simu zaidi ya kawaida, yupo radhi aende nayo bafuni, anakuwa makini asikamatwe anayochat kwenye simu.
5. kuchelewa kurudi nyumbani nk.
Tutaendelea kuangazia dalili mbalimbali za mtu anayekusariti
5. Kuongeza upendo ghafla: mwanaume anapoanza kutoka nje yandoa, kama ndoa yake haina vurugu , anaweza kuonesha upendo mkbwa hadi mkewe akashangaa na kujiuliza. Nafsi inamsuta mwanaume anajishtukia
6. Kuona kasoro nyingi za mke : kama mume anaanaza kuona kasoro nyingi za mkewe ambazo hapo nyuma alikuwa hazioni, basi ana lake jambo.
7. Mabadiliko ya kipato: Kuna wakati mabadiliko ya kipato yanaweza kuwa ni kiashirio cha mwanaume kutoka nje ya ndoa. Mwanaume anaweza kuwa na ajira ile ile au shughuli zilezile lakini ikaonekana kwamba kipato hakitoshi.
8 . Alama na harufu mpya: Kama mwanaume siyo makini sana, kupatikana kwa rangi ya mdomo kwenye shati au nguo zake za juu ni rahisi sana. lakini hata kama ni makini, harufu ya pafyumu tofauti na ile anayotumia mkewe inaweza kusikika sana kwenye nguo zake.
9. Mazungumzo ya simu: Kama mwanaume anaanza kuzungumza kwenye simu kwa kukatishakatisha au kusema tu,;nitakupigia baadae,' ama wakati mwingine kuonekana amebabaika baada ya kupokea simu, inaweza kuwa dalili. Kuna wakati anaweza kuwa anakata simu kila ikiita na kubadilika hata usoni kwa tahayari.
10. Mbele ya wanawake wengine: Tafiti nyingi zinaonesha kwamba, wanaume huchukua wanawake ambao wako karibu nao, au wamewazoea kwa njia ya kukutana mara kwa mara. Ni rahisi mwanaume kuwa na hawara ambaye ni jirani, mfanyakazi mwenzie, mshiriki wake kibiashara, rafiki wa familia, au hata mwanafunzi wake.Kwa hiyo mwanamke asijidanganye kwamba, kwa kuwa mwanamke fulani ni rafiki wa familia, ni jirani, ni mwanafunzi wa mumewe, hawezi kuwa na uhusiano naye, hapana. Kwa mwanaume, hao ni mawindo rahisi sana.

Tutaendelea badaye kidogo. Endelea kufuatilia makala zetu kila siku kwa mafunzo mbalimbali ya maisha
©Bahati Magweiga
Mshauri elekezi wa vijana na mahusiano
Simu namba 0757472165

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...