Skip to main content

UPANGILIO WA CHANJO KWA VIFRANGA.

MPANGILIO SAHIHI WA CHANJO KWA VIFARANGA CHOTARA NA KIENYEJI
.............................................
Vifaranga ili wakuwe vyema na kusitawi ni lazima wazingatiwe katika chanjo na chakula bora.  
Chanjo humsaidia kifaranga kujikinga na magonjwa hatari ambayo hayana dawa kama vile mdondo,  mahebe  ,  Gumboro na ugonjwa wa ndui. 
Haya ni magonjwa ambayo yakitokea Katika shamba huweza kuleta vifo na hasara kubwa kwa mfugaji.  
Magonjwa haya huwa yana chanjo na sio dawa hivyo mfugaji anapaswa kuzingatia ratiba za chanjo kwa usahihi 
   *RATIBA ZA CHANJO* 

SIKU 1.    MAREK'S
SIKU 7.    NEWCASTLE
SIKU 14.    GUMBORO
SIKU 21   NEWCASTLE
SIKU 28   GUMBORO
SIKU 35     NDUI

Katika hizo chanjo , chanjo mbili hutolewa kwenye bawa ambazo ni chanjo ya marekes  na  chanjo ya ndui. 
Chanjo zilizobakia huchanganywa katika maji Kwa maelekezo sahihi ya kitaalamu.  
✔️Chanjo hutakiwa kuhifadhiwa Katika sehemu ya ubaridi na kusiwe na changamoto za ukatikaji wa umeme kwa Muda mrefu zaidi.  
✔️Chanjo inatakiwa ikaguliwe tarehe ya kuisha matumizi ili kuwepuka vifo kwa kuku au vifaranga.  
✔️Chanjo ifunguliwe vizuri kulingana na maelekezo ya kitaalamu . Epuka chanjo kukutana na mionzi ya jua Kwa muda mrefu kabla ya kuchanganywa na maji. 
✔️ chanjo nyingi hutumika kwa muda wa masaa 2 baada ya hapo inatikwa kutupwa mbali na mazingira ya kuku. 
✔️ Chanjo zinunuliwe kutoka Kwa wasambazaji wa kuaminika na wenye historia nzuri Katika uuzaji wa madawa na chanjo.  Kuna badhi ya wasambazaji hawazingatii sheria za utunzaji wa chanjo na kusababisha hasara kwa wafugaji. 
✔️ Kuku wagonjwa / vifaranga wasipewe chanjo badala yake watibiwe kwanza wapone kisha ndio wapewe chanjo. 
✔️ chunguza vifaranga kwa makini siku 3 kabla ya chanjo ili kubaini kama kuna ugonjwa wowote. 
✔️ vifaranga wasipewe chanjo wakati wa Jua kali.  Inapendekezwa asubhi /jioni. 
✔️ chanjo ya Newcastle irudiwe kila baada ya miezi 3 . Hakikisha unaandika tarehe uliowapa chanjo na siku ya kurdia.  Hi itakusaidia kutovukisha chanjo kwa muda mrefu.  
   By Mqagweiga
Wasiliana nami kwa uhitaji wa huduma za vifaranga,  ushauri,  mayai,  kuku,  ujenzi wa mabanda bora kupitia namba 
📞 +255757472165
📞+256786155188
E-mail bahatichacha698@gmailcom
Niwatakie ufugaji mwema

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...