Skip to main content

USIMAMIZI WA KUKU WANAO TAGA.

 SABABU ZA KUJIENDESHA KIHASARA KATIKA UFUGAJI

Ufugaji ili ukuletee matokeo chanya inakutaka mfugaji utumie akili nyingi na mbinu sitahiki . Kuliko matumizi mengi ya pesa akili kidogo  ( maarifa )

Nimewahi kusema huko nyuma Kwamba kabla hujaweka pesa zako kwenye tasinia ya ufugaji inakuhitaji kwanza uwekeze kwenye upatikanaji wa Elimu sahihi kuhusu ufugaji.  Kinyume cha hapo ni kuhatarisha mtaji wako.

Wapo watu wanaingia kwenye tasinia hi ya ufugaji kwa sababu wanapesa.  Ukweli usiopingika ni kwamba pesa haiwezi kuzuia kuku kufa isipokuwa maarifa sahihi ya ufugaji ndio yatakusaidia kujua 👇

✔️ Anaumwa nini 

✔️Atumie dawa gani 

✔️Kwa nini Anaumwa 

✔️ dozi sahihi kwa ugonjwa alionao 

✔️Ataweza kupona? 

✔️Anaweza kuambukiza wengine 

✔️Ni magonjwa yatokanayo na ukosefu wa chanjo au mazingira wanayoishi? ?

Ukisema unafuga kwa sababu unapesa itakusaidia kuzuia magonjwa kwa kununua madawa sio kweli kwa sababu kuna kipindi inafikia kuku wanagoma dawa zote za ugonjwa husika.  Mwisho wa siku itabidi wafe kisha kupata hasara.  Tafuta maarifa sahihi kabla ya kuingia huku

Hebu Twende kwenye maada lengwa kuhusu sababu zinazopelekea mfugaji kujiendesha kihasara Bila kupata faida.  Wapo wafugaji wanafurahi kuwa na kuku wengi kwa maana ya Namba Lakini hawampi faida sitahiki 

Kuchakachua chakula.....  hi hupelekea kuku kutaga chini ya kiwango na kusababisha mfugaji kupata mayai ambayo yanatosha kurudisha garama za chakula kwa siku au kwa wiki.   Muda mwingine hata kuku kushindwa kujirisha wenyewe na kupelekea mfugaji kuchukua pesa binafsi kwajili ya kulisha kuku. 

Kuku anapoanza kutaga inabidi mfugaji kuwa makini kuona kama kuku wako wanakupa faida.  

 Nitajuaje napata faida? ???

Hesabu za Kujua kama unajiendesha kihasara unaweza kubaini kupitia kiwango cha makusanyo ya mayai kwa wiki Kisha unatoa garama za chakula na mahitaji yanayo wahusu kuku. 

 Mfano

Una kuku 100 matetea  na kwa siku unapata trey 3 kwa maana asilimia 90.

Kwahiyo ni 3 ×12000=36000/= kwa siku.  

Kwa wiki ni 36000×7= 252,000/= kwa wiki 

Baada ya kupata hiyo pesa unatoa garama ya chakula kwa wiki husika.  Kinachobaki ndio faida yako wewe kwa wiki.  

By experience kuku 100 wanaotaga inatakiwa watumie 87.5kg kwa wiki . Hapa sitaweza kutoa total kwa sababu garama zipo tofauti kulingana na Eneo alipo mfugaji.  Ukiona kwa wiki nzima wanarudisha pesa yao ya chakula unapaswa kujua kwamba unawahudumia kuku ili waendelee kuwepo nyumbani. 

Kutobaini magonjwa kwa wakati.  Hi ni changamoto kubwa kwa sababu itakupelekea kuku washuke kiutagaji au kuacha kabisa kwa muda huku wewe ukitumia garama binafisi kukabiliana na tatizo. Hapa kuna garama mbili madawa +chakula na baada ya kupona itabidi mfugaji uingie mfukoni sana kuwarejesha kwenye hali yao ya awali.  Njia rahisi hapa ni kutumia muda wako  vyema kukagua kuku kabla ugonjwa haujafikia hali mbaya. 

 Matumizi ya dawa yasio sahihi kulingana na shughuli anayofanya kuku au rika.  Kuku anayetaga lazima apewe dawa ambazo hazitaathiri mfumo wake wa utagaji.  Hapa inatakiwa kushaurina na watalamu husika.  Endapo dawa zitatumika Bila kuzingatia utaratibu sahihi ni lazima utagaji ushuke na kujikuta unajiendesha kihasara. 

 Mabanda kuwa machafu.  Hi itakuletea magonjwa mara kwa mara na kujikuta kuku wanaishi kwa madawa kila siku.  

By Magweiga

📞+255757472165

📞+255786155188

Tutaendelea kuangazia somo hili kwa upana hapo kesho Mungu akitujalia uhaI.  :"

Karibu kwa uhitaji wa vifaranga wa kroila wa siku kwa shilingi 1500/=Vifaranga Hawa hupatikana kila wiki .


Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...