Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.
James William (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake.
Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio. Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo (atttitude)
Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako.
Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia katika hisia, misimamo na mahusiano juu ya watu wanao kuzunguka.
1. MSIMAMO WAKO HUCHANGIA MAFANIKIO YAKO:
Neno msimamo ni muhimu sana katika nyanja yoyote ya mafanikio. Kwa mfano
Mtendaji yeyote kwenye kampuni anaweza kuwa mzuri bila kuwa na msimamo?
Mwanafunzi yeyote anaweza kuwa mzuri darasani bila kuwa na msimamo? , Mzazi., Mwalimu, mfanya biashara, mwajiri, mwajiriwa nk wanaweza kuwa na utaratibu mzuri wa sheria bila kuwa na msimamo? .
Kwahiyo kuwa na msimamo kwenye maisha yako kuna harakisha mafanikio yako mbele zaidi.
2: KUWA NA MSIMAMO KUTAKUSAIDIA KUTATUA MATATIZO (NYUMBANI NA KAZINI KWAKO)
Ukiwa na msimamo ni rahisi sana kuwepukana na musongo wa mawazo katika maeneo mbalimbali kama vile kwenye familia pamoja na maeneo unayofanyia kazi zako. Lazima tukubaliane kwamba sisi sote ni watu wa majukumu tunakwenda kujitafutia riziki na tunarudi nyumbani. Kinachotokea ni kwamba asilimia kubwa ya watu huchukua matatizo ya kazini na kurudi nayo nyumbabi na pia huchukua matatizo ya nyumbani na kwenda nayo kazini. Kinachotokea unapokuwa unahama na matatizo ni kwamba uzalishaji utapungua na musongo wa mawazo utaongezeka kazini kwako. Hivyo hivyo kwenye familia. Hiyo yote ukiwa na msimamo ni rahisi kujua namna ya kuvitatua.
VITU VITATU VINAVYO UNDA MISIMAMO YETU KATIKA MAISHA.
Misimamo yetu inatengenezwa na vitu vitatu
1. Ujuzi
2. Mazingira
3 Elimu
a) ujuzi : Tabia zetu zina badilika kutokana na ujuzi wa watu mbalimbali tunaokutana nao katika maisha yetu. Watu tunaokutana nao kila siku katika maisha huweza kubadili kabisa misimamo yetu kutoka chanya na kuwa hasi au kutoka hasi na kuelekea chanya. Hii inategemea sana na aina ya watu tunao changamana nao.
b) Mazingira : katika upande wa mazingira tunangalia maeneo kadhaa kama vile
- Mazingira ya kisiasa
- Mazingira ya kimira
- Mazingira ya kijamii
- Makundi hasi (peer pressure)
- Mazingira ya kidini nknow
Vyote hivyo vinaweza kuchangia kwa asilimia kubwa kwenye kujenga msimamo aidha msimamo hasi au chanya.
C) Elimu : Elimu zote mbili zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye kuunda msimamo wa maisha yetu. Hii inatokana na kuwepo kwa matumizi sahihi na ya siyo sahihi kielimu.
FAIDA ZA KUWA NA MSIMAMO CHANYA :
- Huongeza uzalishaji
- Husaidia kufanya vizuri kama timu moja na kufikia malengo yenu
- Hutatua matatizo
- Huongeza ubora
- Hukuza uhusiano
- Hufanya mtu kuwa sehemu ya mchango katika jamii
- Humfanya mtu aombe msamaha pale anapokuwa hayuko sahihi ili kumusaidia kuimarisha uzalishaji.
Kikubwa kinachowasumbua wengi ni kulalamika pasipo kuchukua mamzi magumu. Wengi wao hutumia kauli zifuatazo
- Hali ya uchumi ngumu
- Sina bahati ya kufanikiwe
- Mimi bado ni kijana
- Nishazeka muda umeniacha
- Sina Elimu ya kutosha
- Nimezaliwa kwenye familia masikini
- siko vizuri kwenye kuzitambua furusa zinazo kuja mbele yangu
- sina mtandao mzuri wa watu.
- sina familia
Napenda niunganishe makala hii hapa chini hasa kwa wanawake kama sehemu ya kujitambua :
USHAURI WA BURE KATIKA UPANDE WA WANAWAKE ( JITAMBUENI )
Mara nyingi wanawake ni watu Ambao wanapenda Sana mambo ya mitandao kuliko akina baba, na wakati mwingine wanajisahau sana kiasi Kwamba kupitia post Zao mtu anaweza jua maisha yako Bila hata kuja Nyumbani kwako kuishi na kuona,
Wakati mwingine hata kitendo cha wewe kutupia mapicha na kuonyesha labda kuwa uko sehemu fulani labda na mumeo au mkeo mnakula good time, au upo likizo sehemu fulani, au umesafiri na ndege hii na kubadili ndege nyingine, au mafanikio ya watoto wako kwenye mitandao, au Muda mrefu umekuwa Ukitafuta mtoto na umepata ujauzito unatupia picha hata mtoto hajazaliwa, unatupia mapicha ya matanuzi yako na vitu vyako kama Magari, Nyumba nakadhalika na mara nyingine wengi wetu huwa tunasahau kubadili maneno ya status yako hii ni kwa wanawake na wanaume.
Nataka nikwambie kitu kuwa kuna watu wapo kimya kimya lakini Wana mafanikio ya hatari na huwezi kuona wamejionyesha onyesha my dear na sikuambii kuwa kwa kufanya hivyo wewe unavyofanya mitandaoni kuwa Labda ni Dhambi kwa Mungu aaaaaah ila unatakiwa utambue kuwa
1.Mara nyingi ni wachache sana watakaofurahi kweli na wewe
2.Comment nyingi nzuri utakazokuwa unapata kutoka kwa watu ni fake tupu ila tu laiti ingeingia ndani ya mioyo yao uone ndio ungeamini
3.Kwa kufanya hivyo jua kuwa kuna watu wataanza kukuonea wivu na kuongeza maadui na macho ya kishetani na wengine hata uchawi yatakuwa Juu yako na familia yako,
Hivyo wanawake Mungu atusaidie na tuwe makini na vitu vya kupost mitandaoni ili visije kuwa chanzo cha hazuni zetu baadaye, maana Kuna watu wengine wanatafuta mashambulizi, hivyo wote tuwe makini na mitandao na tubadilike maana shetani unajiinua sana kuvuruga maisha ya watu na familia za watu kupitia mitandao maana anajua ndio kwenye opportunity.
Tujifunze hili pia maana Kuna watu Wanaweza wasinielewe labda wakaelewa kupitia hii
Ndugu zangu wapendwa nawaomba sana msichukulie kwa wepesi jambo hili... Unapobadilisha Picha yako ya dp usisahau kubadilisha na maneno ya status yako... Ikiwezekana unapobadilisha Fanya vyote kwa pamoja hapo hapo. Rafiki yetu mmoja ametuambia kwenye group jingine kuwa kuna sokomoko limetokea nyumbani kwake na moto wake hauzimiki leo ni wiki ya tatu na mwisho wake haujajulikana bado... Sokomoko hilo lilianza hivi... Jamaa aliweka Picha ya gari lake la zamani na kuweka maneno ya status "Baya kama nini, hata kuliangalia linatia kinyaa" kwa bahati mbaya au nzuri mke wake wakati huo wote simu yake Ilikuwa inasumbua hivyo hakuweza kuingia watsap. Baada ya kama wiki akaweka Picha ya mkewe alafu akasahau kuondoa maneno ya status iliyokuwa na Picha ya ile gari... Shetani anavyojua kuyapanga mambo, simu ya mkewe ikatengemaa akarudi hewani na kukuta Picha yake kwenye profile ya mumewe na maneno yale... Mpaka leo nyumba haijatulia kama mvua za Dar... Habari hii ni ya kweli na usiidharau fanyia kazi..
Share na wenzio kama umevutiwa na makala hii.

Comments
Post a Comment
asante kwa kuichagua tujengane media kuwa sehemu yako ya kujifunza