Skip to main content

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

 MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI 

Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa. 

Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida 

Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%%

Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.  

Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia.

Ukweli ni kwamba itafika sehemu utaona kama ufugaji unakuonea vile kumbe sio kweli bali ni matamaa yako tu mfugaji.   Kwa hesabu za haraka kuku 100 kroila wakiwa watagaji wazuri na wanao simamiwa vyema watakupa 252,000/=  kwa wiki ila usiache kukumbuka kwamba wanaweza kutaga chini ya kiwango. 

Kama mfugaji utakuwa unategemea kuku 100 uliowakuza kwa shida ndio waendeshe 200  vipi siku ikitokea wameshindwa kutaga inavyotakiwa? Kuna wakati wanashuka utagaji bila tatizo lolote Jeee!  Unaweza kumudu hawa 200? . 

Asilimia 99% ya wafugaji wanaofuga kwa Tamaa  huwa hatuoni faida kabisa.  Kwa sababu Tunaamini Katika wingi na sio Katika ufanisi. 

 Ukiona kroila nipe

Ukiona sasso nipe

Ukiona tanbro  nipe hata 10 

Ukiona Malawi unasema nikichukua hata 20  sio mbaya.

Unajikuta mfugaji una aina zote za kuku pale nyumbani japo wachache wachache lakini hawaendani 

✔️umri, 

✔️ ukuaji tofauti 

✔️ulishaji wao tofauti 

✔️utagaji wao tofauti 

Lengo hapo ni nini kama sio Tamaa? 

Kwa nini usitumie hiyo pesa kuendesha kuku wa aina moja ili wakuwe vyema wakuletee matokeo? ????

Wafugaji wenye Malengo huwezi kukuta anafuga mbegu zote za kuku kwa pamoja bali huchagua ilio bora zaidi na kuiboresha ili apate matokeo ya haraka. 

Ufugaji mpaka ufikie faida sio jambo jepesi kama wengi tunavyo chukulia.  Inahitaji akili, umakini, mtaji na muda.

O786155188

 ushauri wangu

✔️ punguza Tamaa na ridhika na ulichonacho kwanza hadi kikuletee matokeo.  Kuingiza vifaranga wapya bila mtaji kwa kutegemea kuku 100 wawendeshe ni kutafuta *stress* 

✔️Fuga kwa Malengo 

✔️Chagua kitu ambacho unataka kuku wakusaidie kutimiza Katika safari ya maisha yako Kisha weka kidogo kidogo kutimiza hicho kitu. 

http://www.tujenganemedia.blogspot.com

 Inaweza kuwa ni kiwanja au ujenzi wa nyumba nk.  Kama kuku watakujengea nyumba, au kukupa kiwanja nk lazima uhamasike kila uwonapo kitu hicho. 

✔️jifanyie Tathimini kama unasonga mbele na uchukue hatua zaidi.  

✔️Tumia sana watu wanaofanya vitu kwa vitendo zaidi ya wahamasishaji. Hawa wanaweza kukuingiza kwenye mtego ambao mwisho wa siku utakufanya uchukie ndoto zako.  

✔️Chagua watu sahihi wa kujifunza kutoka kwao kuhusu ufugaji wako 

✔️ kuwa na msimamo Katika kile unachoamini kuhusu ufugaji wako ili muradi kiwe sahihi. 

By Magweiga 

📞+255757472165

📞+255786155188

bahatimagweiga467@gmail.com 

✔️vifaranga 

✔️Mayai

✔️kuku 

Vyote vinapatikana kwetu 24 hrs.  Wasiliana nasi kupitia hizo namba hapo juu.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...