Skip to main content

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake)

MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI. 

Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji. 

Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.  

 Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa.

kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment

1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea 

✔️ Typhoid 

✔️Mafua 

✔️ coccidiosis 

✔️kipindu pindu cha kuku

 Haya yote ni magonjwa ni magonjwa ambayo yanamlengo wa kimazingira. Ni magonjwa ambayo husababishwa na

✔️ uchafu wa mabanda, 

✔️vyombo vya maji, 

✔️️mabanda kuwa mabichi muda mrefu,  

✔️Uchanganywaji wa kuku wasio endana umri,  ✔️Mzunguko hafifu wa hewa bandani, 

✔️chakula kuwa kichafu na kilicho chini ya kiwango,  

✔️Kutokuwa na vitendea kazi maalum kwa banda husika,  

✔️usimamizi usiokuwa endelevu,  

✔️Matumizi ya dozi yasioweza kupona kwa kuku jambo ambalo hupelekea kudumu kwa magonjwa muda mrefu bandani na hatimaye kupelekea vifo, 

✔️ Kuchelewa kubaini ugonjwa ukiwa kwenye stage za mwanzo. 

Pia yapo magonjwa yenye mlengo wa chanjo kama vile  

Newcastle disease,  gumboro, 

marekes,  

IB  nk.  Haya ni magonjwa ambayo mfugaji anapaswa kutumia chanjo kuwakinga kuku wake. 

 Hapa napo kumekuwepo na changamoto kuwa ya Nani amfunge paka kengere?* magonjwa Haya yakitokea huwa kuna kusingiziana  Kati ya muuzaji na mfugaji.  

Mfugaji anasema chanjo aliwapa labda aliponunua ndio kuna kasoro lakini pia muuzaji hutetea kwa nguvu zote  ubora wa chanjo zake. 

Anayepata hasara kubwa ni mfugaji.  Utakuta kapoteza kuku *1000*  kwa magonjwa Haya yenye mlengo wa chanjo.  

Hapa ni kuhakikisha unazingatia mambo muhimu wakati wa kutoa chanjo,  kabla na baada ya chanjo.   Chagua chanzo sahihi cha  uchukuaji wa chanjo. 

 2 .Tamaa. ni miongoni mwa mambo yanayo kwamisha wafugaji wengi na kujikuta wanapata hasara kuwa.  Unakuta mfugaji mtaji wake ni kuhudumia kuku 100 ndani ya miezi 5 alafu mfugaji huyo anaingiza vifaranga 500.  Kinachotokea hapa ni mtaji kukatika na kujikuta umeingia kwenye janga la kudumaza kuku. 

Wingi si hoja. Unaweza ukawa na kuku 500  dhaifu,  hawana afya,  wamekonda na hata kuwauza ni changamoto. Lakini mwanzako akawa na kuku 200 wenye kiwango na afya nzuri.  Huwezi kumfikia hata kidogo.  

0757472165

NB: Maisha ni kupanga  na kupanga ni kuchagua

Fuga unachokimudu na utaifurahia kazi hi ya ufugaji.  Utapata matokeo mazuri na ya kufurahisha.   

0786155188

Ili tufanye vyema kwenye miradi yetu na kupata matokeo lazima Tuzingatie 

✔️ Usafi wa mabanda 

✔️Usafi wa vyombo 

✔️Chanjo 

✔️ Chakula bora . Epuka kujichanganyia hovyo chakula.  Tumia formula zinazoleta matokeo chanya.  Usiwe mwepesi wa kuchakachua chakula ukidhani unakwepa garama.  Watakudai huko mbeleni. 

✔️ Vitamin +minerals 

✔️Mbegu bora . Chagua Mbegu inayoweza kukua kwa haraka na kupata mwitikio +++

✔️Bajeti sahihi . Usiweke kuku ambao haujui namna ya kufika nao kwenye lengo.  

✔️ Usimamizi binafsi . Fuatilia kwa ukaribu kwani wewe ndio uliyebeba maono ya miradi yako.  Fuatilia kujua kama pesa yako itarejea au laa! 

✔️ Nia ya kufanya 

✔️Elimu ya ufugaji.  Usiache kuendelea kujifunza, . Hakuna aliyewahi  kumaliza kusoma 

 By Magweiga

 Magweiga poultry investment

Wauzaji wa vifaranga, kuku, mayai nk. . 

📞+255786155188

📞+255757472165


Comments

Popular posts from this blog

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...