Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2018

LAZIMA KUCHAGUA KUNYAMAZA.

                              MITHALI 11:12  Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. MITHALI 17:28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu. Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba tunataka kuongea kila wakati, tunataka kujibu kila tunachokisikia, kila tunachokiona tunataka kukisemea kitu. Kuna wakati tunasikia na kukutana na mambo ambayo kiuhalisia moyo unagoma kabisa kunyamaza, unatamani ujibu, unatamani uwaambie watu yale umefanyiwa, unatamani uelezee vile umeumizwa lakini kumbe si kila jambo linatakiwa kuongelewa. Si kila ukionacho unatakiwa kukisemea kitu. Si kila usikiacho/uambiwacho ni lazima ujibu. Si kila ufanyiwacho ni lazima umwambie kila mtu. MUHUBIRI 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; I...

KABULA YA KUTAFUTA MCHUMBA ZINGATIA MAMBO HAYA.

by   Lameck & Faustina Mtaka USIHARAKISHE . Usiharakishe na kukurupuka kutafuta mchumba kabla ya wakati muafaka.Pengine unaweza kujiuliza ni wakati upi ni muafaka kutafuta au kuwa na mchumba?ni wakati unapokuwa umekomaa kiroho, kiakili na kimwili umejitambua kikamilifu ulikotoka, mahali ulipo na unapokwenda na umetathimini kwa makini mipango na ratiba yako ya sasa na ya baadaye ndipo waweza kuchukua hatua hii mhimu katika maisha. Wengi wamepuuzia hili na kukurupuka kutafuta mchumba bila kujitathmini na kuishia kwenye uasherati na usaliti vilivyowaletea huzuni na majuto badala ya furaha na ndoa takatifu. Biblia inasema  “ Ni nani katika ninyi Kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kumalizia asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi watu wote waonao wakaanza kumdhihaki…….” (Luka 14:28-30).   USITAFUTE MCHUMBA KWA MSUKUMO KUTOKA NJE. Usitafute mchumba Kwa kuangalizia, kushawishiwa, kuiga au kusuk...

USHAURI KWA MABINTI

Moja  ya taswira ya kutambua kesho ya mwanamke yeyote katika ndoa yake ni kutambua msimamo wa awali. wapo mabinti ambao  wamepoteza waenzi wao kwa kushindwa kuwa na msimamo katika mahusiano yao. kwa maana nyingine tunasema wanavumishwa na wimbi la watu wakupita na ambao hwana mpango wowote wa kukuaa nao kimahusiano. tathimini inaonyesha kwamba asilimia kubwa ya wanawake ambao hawajaolewa na hawatarajii kuolewa wamekumbwa na tatizo hilo kutokana na kukoswa msimamo kipindi cha ubinti wao.    Jambo la kutambua ni kwamba unaposhindwa kuwa na msimamo lazima hadhi yako itashuka na kujikuta unakuwa mtu wakimatumizi katika upande wa wanaume. ipo haja ya kubadilika kama watoto wakike ili kuweza kutoa taswira chanya ya kesho. wanaume wanachohitaji kwa sasa ni umakini na msimamo wa mwanamke na siyo urembo wa mwanamke. japo kwa sasa wamebakia wanaume wachache wanaotumia kauli ya kwamba sura ndio kila kitu.  kuna misingi maalumu amabayo unatakiwa kuitambua kama binti ili k...