Skip to main content

USHAURI KWA MABINTI

Moja  ya taswira ya kutambua kesho ya mwanamke yeyote katika ndoa yake ni kutambua msimamo wa awali. wapo mabinti ambao  wamepoteza waenzi wao kwa kushindwa kuwa na msimamo katika mahusiano yao. kwa maana nyingine tunasema wanavumishwa na wimbi la watu wakupita na ambao hwana mpango wowote wa kukuaa nao kimahusiano. tathimini inaonyesha kwamba asilimia kubwa ya wanawake ambao hawajaolewa na hawatarajii kuolewa wamekumbwa na tatizo hilo kutokana na kukoswa msimamo kipindi cha ubinti wao. 
  Jambo la kutambua ni kwamba unaposhindwa kuwa na msimamo lazima hadhi yako itashuka na kujikuta unakuwa mtu wakimatumizi katika upande wa wanaume. ipo haja ya kubadilika kama watoto wakike ili kuweza kutoa taswira chanya ya kesho. wanaume wanachohitaji kwa sasa ni umakini na msimamo wa mwanamke na siyo urembo wa mwanamke. japo kwa sasa wamebakia wanaume wachache wanaotumia kauli ya kwamba sura ndio kila kitu. 
kuna misingi maalumu amabayo unatakiwa kuitambua kama binti ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuwa mwanamke mwenye maono na mwenye kuonyesha taswira ya badaye.

TAZAMA HAPA KAMA UNA SIFA ZIFUATAZO  BASI UTAKUWA MKE MWEMA WA  BADAYE.

MKE MWEMA HUJAWA NA HEKIMA.

Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi vizuri – Ukali, maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida. Wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mwanaume anaempenda anacheka na mwanamke ni Kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata mpaka marafiki wanatambua kuwa hali ni mbaya. Mwanamke anaepiga kelele na mgomvi bibilia imemwita mwanamke mpumbavu. “Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.” (MIT. 9:13)
Ni vizuri kutofanya jambo kwa hasira na kuiruhusu hekima kukutawala
UVIVU SIO SEHEMU YA MAISHA YAKE.
Kuna wanawake ambao ni wavivu kupita kiasi hawawezi fanya jambo lolote wenyewe lazima kumtegemea dada wa kazi. Kila kitu huwa wanakua na sababu utasikia sipigi deki sababu kiuno kina mshituko, sifui nguo kucha zangu ni laini zinakatika, neno la Mungu linasemaje juu ya wanawake wa namna hii?
“Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu.” (MIT. 22:13)
Hawakosi sababu kwa kile wanachotakiwa kufanya,ili uwe mwanamke/mke mwema jifunze kujibiidisha na uache uvivu.

NI MSAFI, ANAYEJUA KUPANGILIA MAVAZI YAKE

Kuna wanawake ambao wanaamini wanaume wanaangalia tabia tuu. Sio kweli. Lazima avutiwe na wewe kwanza maana tabia haionekani kwa nje ni kitu cha ndani,so mwonekano wako ndio unaoweza kumfanya kutaka kujua tabia yako. Mwanamke/mke mwema anajua avae nini kwa wakati gani na anajua namna yakupangilia rangi za mavazi yake ili kuonekana akiwa na mvuto, Mwanaume anapomwangalia mwanamke anapata picha hata ya watoto wake watakavokua wanavalishwa. Sio tu mavazi hata mwili- ni vizuri kuwa msafi wa mwili sio kijasho cha hatari au harufu isiyo kuwa ya kawaida, kumbuka Mungu ndo anaangalia moyo ila mwanadamu anaangalia nje kwanza moyo badae kwa hiyo usafi wa mazingira na mwili ni jambo muhimu. “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.”(1 TIM. 4:12)

ANATIMIZA MAHITAJI YA NDOA KWA MUME WAKE

Sulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku.” Kuna wanawake wavivu kwa swala hili, pia kuna wanaopenda kulipiza visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki nzima mama anapanda kitandani huku amevaa “KOMBATI” utafikiri ni askari anaenda vitani. Wanaume ni sawa na mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa. Fanya makosa yote, lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya ndoa, hilo ni kosa la Jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Mungu.

ANAJUA KUPIKA CHAKULA KITAMU CHENYE KUFURAHIWA NA FAMILIA.

Wanawake wengi hasa wa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula hotelini au kwa mama ntilie, kama umetoka bara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga NAZI kwenye chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, Mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, wanaume wanapenda chakula chenye ladha “Taste”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani. Ni hatari mwanamke kuwaza ndoa wakati hata chai ukipika unaunguza

ANATAMBUA KUWA WIVU NA HISIA MBAYA NI ADUI WA NDOA YAKE.

Usitoe siri za ndoa yenu kwa mashoga au ndugu zako. Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, Muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na Hekima ya kutunza ndoa kwa uadilifu na upendo, sio unaita watu nakuanza kusimulia madhaifu ya mumemo. “Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu. Hukaa mlangoni pa nyumba yake, Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka, Apate kuwaita wapitao njiani, Waendao moja kwa moja katika njia zao. Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili,” (MIT. 9:13-16)

ANA HOFU YA MUNGU SIYO YA MUME

Ni hatari sana kuwa na mwanamke mwenye hofu ya mwanaume na siyo ya Mungu. Hofu ya Mungu itamfanya asifanye vitu kwa kificho maana anauhakika Mungu anaona kila sehemu, Mwanamke mwenye hofu ya Mwanaume ni janga maana machoni kwa mwanaume ni mwema kama kondoo akitoka hapo ni mbuzi mwenye pembe kali. Wakati mwingine wanaume wamekua wakijitia moyo watawabadilisha hao wanawake. Kama hakubadilika mkiwa rafiki usitegemee atabadilika ndoani.Mke akiwa mcharuko uwezekano mkubwa wa watoto kuwa kama mama ni mkubwa maana ndo anakuwa nao muda mrefu

MWENYE MATUMIZI MAZURI YA PESA

Hili ni jambo la msingi sana na wanawake wengi huwa hawajui wanaume wengi huwatega katika huu mtego na kuwapima. Siku zote usitake kukomoa kwasababu anaekununulia ni mwingine na sio wewe, mtu katolewa labda chakula cha jioni ataanza kuagiza vitu alivyokua anaviona kwa tv bila hata kujua bei yake mradi halipi yeye, au kama ni shoping atahakikisha kanunua kila kitu alichokuwaga anawaza maishani bila kujali gharama kwa alie mtoa. Lakini pia hata kama ni kwa hela yako mwenyewe jifunze kuwa na akiba. Ni aibu sana mwanamke/msichana mwenye zaidi ya miaka 20 kutokua na akaunti/fedha ya akiba.

HUJISHUSHA NA KUOMBA MSAMAHA

Ugomvi mwingi kati ya mwanaume na mwanamke au mume na mke mara nyingi hutokana na wote kutaka kua juu hakuna aliyetayari kushuka. Kumbuka mwanamke ndio mlinzi wa ndoa. Wakati mwingine kushuka kwako ndio kunaweza pelekea mume/mwanaume naye kuona makosa yake lakini kutojishusha mara nyingi huleta magomvi ambayo mwishowe huleta aibu “Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.” (MIT. 11:2)

MWENYE MAWAZO YA KUENDELEZA FAMILIA.

Mwanamke mwenye upeo mpana wa kufikiri sio yule anaewaza namna ya kubadilisha ma dera, mwanamke mwema ni yule mwenye kukaa na kushauriana na mumewe juu ya mipango ya maendeleo na kumtia moyo mumewe juu ya mipango aliyonayo na sio kuwa kikwazo kwake na kumuonyesha kuwa hawezi kufikia malengo yake.



Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...