Skip to main content

JINSI IMANI YA ELIMU INAVYO WATIA WATU UMASIKINI



Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.

📚 Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏡 na 🚗 magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!). Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.

Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.

1.Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli. Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.

2. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha. Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Sasa nisikilize:- Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninataka uelewe jambo hili: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani. Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.

Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHUMBA

Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba; Jambo la kwanza –    Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu 2Wakorinto 3:17  ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’. Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya. Kum...

ZINGATIA HAYA UNAPOKUWA MBALI NA MWENZI WAKO

KAMA UKO MBALI NA MPENZI WAKO ZINGATIA HAYA Kama unaishi mbali na mpenzi wako kwanza kabisa unatakiwa kukubali kua mko mbali, huwezi na wala hutakiwi kucontrol kile anachokifanya kule, acha kufuatilia anafanya nini huko, yuko na nani na mambo kama hayo, kwa kfuupi wivu weka pembeni kwani ukiendekeza utachanganyikiwa. Kuna mambo mengi atayafanya mazuri na mabaya lakini kama hakuonyeshei basi huna haja ya kuyafukunyua. Jambo la pili ni mawasiliano haya ni muhimu na anapokupigia simu au unapompigia tumieni muda wenu vizuri kwa kuongelea kuhusu mapenzi na si kila siku “Mbona hukupokea simu yangu? Mbona nilikuona online hukujibu SMS zangu? Kulalamika sijui nimesikia hivi? Nimesikia vile!” Atakuvumilia kwa muda kisha itaboa na atakua anakwepa kuzungumza nawe na mwisho mapenzi yatakufa. Hata kama mnaongea dakika tano zifanyeni ziwe tamu zihusu mapenzi na si kuzozana mpaka mtu akitaka kupiga simu anawaza hivi nikiongea naye si kelele tu, hakuna mtu anapenda kupigia simu mtu aliyenuna....

VITU VYA MSINGI VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUDUMISHA UPENDO KATIKA MAHUSIANO

Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.” Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi. Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea, yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana. 1. Uaminifu Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote. Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako. Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano. Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli...