Skip to main content

HAKUNA NDOA ILIYOKAMILIKA ASILIMIA 1000%

Nataka kukuambia kuwa hakuna ndoa iliyo kamili yaani perfect, na kama kuna mtu Anakwambia kuwa ndoa yake ipo perfect ujue huyo ni muongo mkubwa vinginevyo kama hao watu waliooana ni mazombi kwa maana nyingine siyo Binadamu, hata kama ni ya mchungaji wako, shehe wako au hata askofu wako wa jimbo . hata hao mnaoona wanatupia mapicha picha na wake zao au waume zao kuonyesha kuwa wapo happy Haimaanishi kuwa ndio Muda wote asubuhi mpaka jioni,jumatatu mpaka jumapili, January mpaka December wao ni kucheka tu  hapana kiasi Kwamba ukaona kuwa ndoa yako haifai kabisa au upo kwenye Shimo, Kwenye ndoa watu kuna kukwazana, kupishana, hata kugombana kabisa wakati mwingine lakini  kikubwa tunachotofautiana wengi ni namna ya kushughulikia hayo matatizo yanapojitokeza na kuishia kuharibu ndoa zetu wenyewe



Katikati ya ndoa yenu nani mumemweka kama mhimili wenu ni Mungu au nani,? Wanaume kujaa ufahari kuwa mimi mwanaume Bwana siwezi omba msamaha, wanawake na wao husema Kwamba atanionaje huyu mimi labda nikimuanza kumuongelesha wakati yeye ndio Mwenye makosa,na wengi kutokuwa wakweli na kuamua kuyaongea matatizo yao hivyo kubaki na Vinyongo Moyoni mpaka kushindwa kusamehe. Tuachane na ujinga na tabia zinazohatarisha ndoa zetu, kumuanza mwenzio hata kama wewe sio mwenye makosa au kujipendekeza kwake ilimradi tu kunusuru na kuifanya ndoa Iendelee mbele  na  kuleta amani siyo Dhambi na siyo ujinga bali ni ujasiri na kujitambua zaidi.
   
      Bahati Magweiga
       Whatsapp : 0757472165
          Tigo           0659991953

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...