Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2019
Moja ya kitu ambacho kinakimbiza wateja dukani kwako ni kupokea mteja huku umekaa. Kinaua mood ya wateja wengi sana. Mteja ni kama mgeni,a napokuja dukani kwako uchangamfu wako ndiyo utamfanya kununua. Hembu jiulize umeenda kwa rafiki yako, umefika anakukaribisha anakuacha sebuleni anaenda kupiga stori nnje na watu wengine utaruudi? Sasa una duka mteja anakuja umekaa, anaulizia kitu flani umekaa unamuonyeshea kwa mkono tu au unamuambia ingia uangalie! Ndugu yangu labda kama unauza Oxygen kwamba nisiponunua nitakufa sirudi. Mteja akija kwako kwanza nyanyuka huku ukimkaribisha, akiulizia nguo flani nenda ishike, hata kama hutaki kuishusha lakini mgeukie muulize ni saizi gani, kama ni sahani muulize unataka rangi gani na chochote kile. Unaponyanyuka kuna mambo mawili yanatokea, kwanza anahisi unamhehsimu, anaanza kujiona kuwa kumbe na yeye ni wa muhimu anaheshimiwa, lakini pili anaanza kuona aibu, anaona kuwa huyu nisiponunua nitakua nimemsumbua. Lakini pia kuna kitu cha tatu kinatokea ...
Mke au binti unayetarajia kuolewa lazima utambue kuwa mume wako anapokuoa pia Ana wazazi wake kama wewe na Ana ndugu zake Kama wewe, imekuwa kawaida kwa mke kutaka au kupenda na kufurahia pale Ambapo mume Wake kama Ana uwezo Kusaidia ndugu zake na wazazi wake lakini linapokuja suala La mume kutaka Kuwasaidia ndugu zake wengi huwa tunakasirika na hapo ndiyo tunaanza wengine kuonyesha rangi zetu halisi na makucha yeti, labda niwaulize kwani Kuna ubaya Gani mume akisaidia ndugu zake au wazazi wake na mbona kwenu mkisaidiwa hukatai na uwezo upo, wengine tunaenda Mbali zaidi mpaka mnachonganisha ndugu na mume wako au mume wako na wazazi wake wakati wewe ndiyo unatakiwa kuwa kiunganishi mzuri kwa ndugu wa mume wako  na wazazi tena wakati mwingine hata ukiona mume wako Anajisahau sana na kuwa bize na mambo ya familia tu ni muhimu kumkumbusha kuhusu kuwakumbuka wazazi hata kwa kuwatembelea hata kama wazazi wana uwezo pia wapelekeeni hata zawadi yoyote mtapata Baraka za wazazi pia, hata kam...
USIRUHUSU WATU KUTUMIA HISTORIA YAKO KUKUNYANYASA! Kuna mambo mengi ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma, kuna hatua nyingi ulipitia, zipo nzuri zipo mbaya, kuna mambo mengi ambayo unatamani kuyasahau katika maisha yako lakini huwezi, kuna mambo mengi unatamani kuyabadilisha katika maisha yako lakini huwezi. Yameshatokea na ni sehemu ya maisha yako, haya tunayaita historia, si sehemu tena ya maisha yako, wewe ni mtu mpya, huwezi kubadilisha historia lakini usijihukumu au kuruhusu watu kukuhukumu kutokana na historia yako. Ulikua Malaya kweli, ulikua mwizi kweli, umetoka katika familia ya kimasikini, ulikua mshamba, ulikua unadanga, ulikua marioo na chochote kile ambacho ulikua, kama umeshapita katika hali yoyote mbaya na sasa hauko huko cha kufanya ni kuangalia historia na kumshukuru Mungu hauko kule tena. Acha kujihukumu, acha kujisikia vibaya na kubwa kabisa usiruhusu watu kukufanya ujisikie vibaya. Anaweza kuwa mume au mke, wanaweza kuwa majirani au ndugu, watataka kukudharau k...

MAMBO YANAYO CHUKIZA WANAUME KATIKA FAMILIA

Moja ya vitu ambavyo vinakera wanaume wengi ni kurudi nyumbani, unataka kuingia ndani unakuta mlangoni kumejaa wanawake, sijui majirani sijui mashoga zake mkeo wanapiga stori. Wengine wametandika na mkeka kabisa wanaongea kana bila wasiwasi wowote. Yaani ili kuingia ndani nilazima upite katikati yao. Unaingia ndani, labda mke alikupokea au hata hakukupokea lakini anatoka nnje kuendeleea na mazungumzo. Lakini pia umewahi kurudi nyumbani, umeamua ukapumzike mara hodi, mara sijui naomba hiki, mara kile mara kile. Hamkai mkapumua washakuja kuangalia TV, sijui kuna tamthilia. TV yako lakini huwezi hata kuangalia kwa uhuru, shoga yake kashikilia romoti. Mwisho wa wiki ndiyo kabisa, rafiki zake ni kujazana hapo nyumbani, wengine washenzi kabisa wanaingia na jikoni kupika. Yaani wanajifanya kupendana sana (Wale ambao wanashona na sare kabisa) wanakuja wanakaa wanapiga stori, kupika na kucheka kila saa! Mwanaume unaamua tu kulala ndani au kujifanya una ubize kzaini. Ndiyo hicho kitu k...