Skip to main content
Mke au binti unayetarajia kuolewa lazima utambue kuwa mume wako anapokuoa pia Ana wazazi wake kama wewe na Ana ndugu zake Kama wewe, imekuwa kawaida kwa mke kutaka au kupenda na kufurahia pale Ambapo mume Wake kama Ana uwezo Kusaidia ndugu zake na wazazi wake lakini linapokuja suala La mume kutaka Kuwasaidia ndugu zake wengi huwa tunakasirika na hapo ndiyo tunaanza wengine kuonyesha rangi zetu halisi na makucha yeti, labda niwaulize kwani Kuna ubaya Gani mume akisaidia ndugu zake au wazazi wake na mbona kwenu mkisaidiwa hukatai na uwezo upo, wengine tunaenda Mbali zaidi mpaka mnachonganisha ndugu na mume wako au mume wako na wazazi wake wakati wewe ndiyo unatakiwa kuwa kiunganishi mzuri kwa ndugu wa mume wako  na wazazi tena wakati mwingine hata ukiona mume wako Anajisahau sana na kuwa bize na mambo ya familia tu ni muhimu kumkumbusha kuhusu kuwakumbuka wazazi hata kwa kuwatembelea hata kama wazazi wana uwezo pia wapelekeeni hata zawadi yoyote mtapata Baraka za wazazi pia, hata kama hupendi kukaa nao basi acha hata huko waliko awasaidie basi. Na hao unaowasaidi leo huwezi jua Watakuja kuwa nani na Watakuja kufanyika vipi kuwa msaada kwako au kwa watoto wako Maisha ni Mzunguko leo wewe unacho kesho hauna leo upo kesho haupo duniani. Yule ambaye leo hii unamfukuza hapo kwako au unamnyanyasa kesho ataweza kuwa mtu mwingine kabisa.

Kumbuka unapokuwa na roho mbaya kwa ndugu na hata wazazi wa mume wako Kuna mbegu mbaya Ambayo wewe kwa kujua au kutokujua unaipanda taratibu na itaota Ambayo itakuja kukugharimu siku moja kama sio kwako mwenyewe basi kwa watoto wako mwenyewe,

Na Ikumbukwe kuwa hata kama mtasaidia hao ndugu ni kwa muda tu na itakoma hata kama wanakaa hapo kwenu hawatakaa hapo milele Kuna kipindi nao Watakuwa na Maisha yao na nyumba zao na hata nyinyi hamtapungukiwa na kitu chochote kwakuwa hukuna lisilo na mwisho, kwa kuwa wakati mwingine Mungu analeta Baraka Ili uzitumie  na watu wengine pia kwa kufanya hivyo unakuwa unazuia mkondo wa Baraka kwenye nyumba yako na wengine baadaye mnashindwa hata kuwaendea hao ndugu kwa kuona aibu wanapokuwa wamefanikiwa mambo yanapowaendea kombo baadaye kwa sababu mkikumbuka mlivyowanyanyasa hao ndugu wa mume na kuwafanyia Roho mbaya lakini kwakuwa Mungu alikuwa na mpango mzuri na huyo ndugu hakukwama,  Usifikiri wewe ukiacha Kumsaidia huyo mtu atakufa au ndio itakuwa mwisho wake hapana Mungu atamuinulia mtu mwingine wa kumfikisha kwenye kanani yake. na wewe baadaye ikakuwia ngumu kwakuwa hukuwa umepanda mbegu njema.

Mimi mwenyewe hapa ni ushuhuda pia wa ninachokiongea Japo sitapenda kuongelea  hapa na nimepitia hayo pia hivyo naelewa  ilifika mahali nilikuwa napewa msaada kwa ajili ya Shule  na familia moja kwa kificho Ili mke asijue  nilikuwa ni lazima niende kazini kwa huyo baba au nikutane naye sehemu  au  akipata muda aje nyumbani kwetu kimya kimya Ili anipe hela ya ada au nauli  na kwakuwa kipindi hicho tulikuwa kwenye Mazingira magumu ya kuhitaji msaada, maana mke akijua  amani itatoweka nyumbani kwake kwa Kusaidia ndugu zake, na haya mambo bado kwenye nyumba zingine yanatokea hivyo tubadilike Wanawake Ili tupande mbegu njema na pia tujifunze katoka kwa wengine

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...