Skip to main content

SIMLIZI YA KWELI YA WANANDOA WAWILI MARRY NA JOSEPH



Mkasa wa kweli wa  wanandoa fulani  ambao mpaka Mwisho wa simulizi hii kila mwanandoa ukiweza kupata Muda wa kusoma utajifunza kitu. Usiwe Mvivu wa kusoma mkasa huu

  JE NANI ALAUMIWE KATI YA JOSEPH
NA MARRY?
Ongozana nami mpaka mwisho wa simulizi.

1.Sehemu ya Kwanza

Joseph Alimuoa marry Kati ya mabint waTatu aliowahi kuwa nao,  marry Alikuwa mzuri sana hata  wa sura kiasi Kwamba Joseph akavutiwa naye Bila kujua uzuri wa mke ni tabia  na sio sura wala shepu,lakini Joseph Alikuwa amekufa ameoza kwa marry, Maisha ya ndoa yakaanza wakiwa hawana kitu yaani wote ndio Wanaanza from zero,  walikaa Muda kidogo Bila kupata watoto baadaye Mungu akawasaidia wakapata mtoto na familia ikaongezeka,  Joseph Alikuwa ni mtoto wa kwanza kwao na Alikuwa ametoka familia ya Kimaskini sana na marry pia hivyo hivyo tena kwao na marry ndio kulikuwa zaidi

 Baada ya miaka kazaa Mke akaanza kabadilika tabia mke akaanza kuwa Mchoyo ndugu wakija Nyumbani anakasirika yaani hata ndugu anapopakua chakula anaangalia chakula,  ikitokea Umefika kama umechelewa Muda walipokuwa wanakula ukakuta kimeisha basi ndugu atahesabu nyota,  na sio kuwa chakula hakipo hapana kipo ila mgeni ataanzia wapi kuomba kupikiwa,  Basi mume wake akawa anaumia  tu kuona ndugu Zake wananyanyaswa,  mume Alikuwa ni mtu Mwenye upendo sana,  mkarimu,  Mwenye Huruma na roho nzuri kwa watu wote haijalishi ni ndugu au Laa,

 baada ya miaka kazaa Mungu akafungua njia mume akapandishwa cheo akawa bosi mkubwa wa kampuni fulani,  wakati wote huo mke yeye ni mama wa Nyumbani,  Maisha yakawa mazuri mnoooo wakatoka kwenye umaskini wakawa kwenye status mpya ya Maisha,  mume akawajengea Nyumba mpya wakwe Zake,  akaanza kuwa saidia ndugu wa mke wake wa sioenda shule na wa sio na shughuli ya kufanya wakatafutiwa cha kufanya, Maisha yakawa mazuri wakasahau shida kabisa,  mume Alikuwa anamuhudumia kwa kila kitu,  mpaka ndugu Zake na wazazi wa mke Alikuwa anahudumia,  kiufupi mke Alikuwa Amepata mume ambaye kila mwanamke angemtamani  awe ndio wake, watu wakajua kuwa basi na mke atabadlika labda roho ya umaskini ilikuwa inamsumbua sasa wa me Barikiwa atabadlika, yaani Pamoja na yote mke akawa bado hataki watu Nyumbani,  yaani urafiki wake na mtu ni upite tu na sio uende kwake ulale,  Hawapendi mawifi mpaka wengine anapigana nao,  mama mkwe ndio kabisa yaani Alikuwa ni mwanamke ambaye hajui thamani ya mama mzaa chema ni nini?  Mume akawa anaendelea kusikitika na kuumia Moyoni  lakini afanyeje mke wake anampenda na wakati mwingine ndugu walikuwa wanakaa kimya kuondoa migogoro Nyumbani, mume wake Alikuwa akisafiri anarudi na vyakula vya kila aina ila Alikuwa chakula cha wengine ni maharage kila siku vitu vingine ni kwa ajili ya watoto wake na kwa sababu mume Alikuwa anamfahamu mkewe kuwa ni Mchoyov Alikuwa akirudi ana tabia ya kuuliza kama walikuwa wanakula ndugu Zake anagundua walikuwa Hawapewi zaidi ya maharage, akiisikia mume wake anarudi safari anatoa Nyama zote,  samaki anawaambia haraka sana wale ndugu aliokuwa anaishi nao kuwa wawapikie mbwa wale na ole wake atakayemkuta anakula Hizo nyama au samaki na ole wako useme kama mlikuwa mnakula maharage tu .

SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI YA WANANDOA WAWILI JOSEPH NA MERRY

Mkasa wa kweli wa wanandoa Joseph na marry  Je nini kiliendea Kati yao

JE NANI ALAUMIWE?

Sehemu ya pili

Mume aaamua Kumpeleka shule mke wake kujiendeleza  aanza Chuo akasoma akamaliza mpaka degree na baadaye  masters atafutiwa Kazi na kutoka kuwa mama wa Nyumbani ,  mume aaamua kumnunulia mke Gari ya kuendea Kaziini na mambo yake mwenyewe ili asipate shida na wakati mwingine mpaka ampeleke, Pamoja na yote ndio jeuri ikazidi maana utamuambia nini tena na shule kaenda na ana hela na yeye
Vitimbi vya mke vikawa vinazidi mke siyo tu Uchoyo,  Bali mkali kama Pilipili,  hataki mume asaidie ndugu Zake ikafika mahali mume ambaye ndio Joseph akaanza kutoa msaada kwao kimya kimya na kwa siri  Bila kumshirikisha mkewe marry kama alivyokuwa anafanya mwanzo maana akimwambia ugomvi na wakati mwingine kukasirika sasa afanyeje Aache kuwasaidia ili Hali wanahitaji msaada wao na ndio mume wake tegemeo La familia, inabidi atumie Hekima ya kufanya siri ili aepushe vurugu,  mume aanza kuona Nyumbani siyo sehemu ya amani tena maana kutwa vituko na hela ipo tena ya kutosha na kubaki, akaanza kuchelewa kutoka ofisini na wakati mwingine kutafuta kampani za marafiki na Kuanza kukaa mahali ili Muda uende afike Nyumbani usiku ale tu na kuoga alale, mke wakati mwingine  akiwa na kampani mpya Wenzake wa Kaanza kumlengeshea watoto wa mujini maana walikuwa wakimuona na mawazo wakajua ana matatizo Nyumbani kwake hivyo wacha apate wa kumtoa stress. Kumbe ndio wanamuongezea tu baadaye
Mambo yakakolea yakawa moto moto mchepuko ukawa mchepuko mpaka mume akazaa na huyo mchepuko, mke akajua ndio Kwanza akawa anataka kushindana na mume wake na  mke ndio akazidi kuwa mbogo mume hata akisafiri anamwambia anatamani hata huko njiani apate ajali afe,  akaacha kupika,  kufua na kufanya vyote akawa housegirl ndio anafanya vyote. Mume akajikuta kaangukia, mkononi mwa housegirl mke baadaye akajua akaamua kumfukuza housegirl.

 Lakini mke Akaendelea na vitimbi,  Alikuwa akimmendea mume wake akiwa anaoga au akiwa amelala ndio anaanza kufukunyua vitu kwenye simu ya mumewe baadaye Akikuta vitu visivyoeleweka ni matusi na wakati mwingine kupigana na kuhama chumba cha kulala anaweza lala cha wageni au watoto mumewe kalala mwenyewe chumbani kwao. Maisha yakaendelea hivyo kwa miaka kadhaaa ya ndoa kutokuwa na amani na furaha. Familia ya Joseph na marry walikuwa na family friend wao ambaye Alikuwa na Binti yao jane aliyekuwa ameolewa lakini kwa bahati mbaya hawakufanukiwa kupata watoto na mume wake John kwa Muda wa miaka tisa waliokaa kwenye ndoa yao na walikuwa ni vijana waliookoka na Wanasali kanisa fulani,  Basi huyo Jane Alikuwa akipata manyanyaso mengi toka kwa mawifi na mkwee kuwa ananenepeana tu na kujaza chooo,  lakini uzuri Pamoja na yote mume wake huyo John Alikuwa akimpenda sana mke wake Jane hivyo hakupenda ndugu Zake walipokuwa wakimnyanyasa hivyo Alikuwa akimwambia Usijali ipo siku Mungu atatupa watoto maana mke hakuwa na matatizo yeyote kutokana na Majibu ya wataalam, mke baada ya kuchoka na manyanyaso Jane siku moja akiwa na baba yake    wakakutana na Joseph wakabadilishana mawili matatu na kupeana namba za simu,  Joseph mume wa marry akawa anawasiliiana na Jane mke wa John na baadaye wakaanza mahusiano yao.

SEHEMU YA TATU

Mkasa wa kweli wa wanandoa Joseph na marry nini kilifuata baada ya Joseph na Jane  Kuanza mahusiano ya siri?

JE NANI ALAUMIWE?

Joseph na Jane walianza mahusiano yao kwa siri sana baada ya Jane kuchoka manyanyaso toka kwa mawifi na wakwe baada ya mumewe  John pia kutompa ushirikiano wa kwenda hospital kufanya vipimo na kujua tatizo lipo kwa nani na wanalitatuaje ili waweze kupata suluhisho na hata kama wanamuomba Mungu wajue Wanaombea nini hasa. Mahusiano yakakolea Kati ya Joseph mume wa marry na na Jane mke wa John,  wakiwa kwenye mahusiano Jane aliyekuwa anatukanwa kuwa hazai akapata mimba Wakaamua kuwa ikabaki kuwa siri yao mpaka mimba ikakua na Hatimae mtoto akazaliwa mume akafurahi na mawifi na mama mkwe aibu zikawashika wakiwa hawajui waanzie wapi kwenda maana walikuwa hawapatani na Wifi yao, mahusiano  Kati ya Jane na Joseph yaliendelea mpaka siku moja marry mke wa Joseph alipogundua mahusiano ya Joseph na Jane mke wa John, mke wa Joseph akamtafuta mume wa Jane  ambaye ni John na kumwambia kuwa mtoto wao anayehisi kuwa ni wake siyo wake maana mke wake yaani Jane  anatembea na mume wake na ndio huyo mtoto aliyepatana,  mume wa Jane akampuuza,

 marry akaona haijafanya Kazi akaamua kuwatafuta mawifi na wakwe wa Jane na kwenda kuwaambia kuwa mtoto wa kaka yao
 sio wao ni wa mume wake, akawaonyesha na na meseji wanazowasilianaga hivyo wa mwambie kaka yao  akampime mtoto wake DNA kama hawamuamini halafu wamfukuze Jane ili kumkomoa Jane,  mume wa Jane na mawifi na wakwe   wakapotezea,

 akaona isiwe shida akaenda kuomba appointment kuonana na mchungaji wa kanisa La kilokole walilokuwa Wanasali jane na mumewe John na kumwambia mchungaji kuwa  muumini wake wamtenge kanisani kwa sababu ametenda Dhambi kwa kuzaa na mume wake, lengo La marry ni kumharibia ili Aachwe na mumewe na mume wake pia amuache then aanze kuhangaika
Mume wake alimkataza kuyafanya yote hayo lakini mke akawa hasikii  anaishindana na mume wake,  na  kumwambia kuwa atamuonyesha kuwa yeye ni nani,? Ikabidi kiitishwe kikao cha ndugu na mume wa Jane akathibitisha kwa baba yake kuwa ni kweli hana uwezo wa kumzalisha na siku nyingi alishalitambua kwa kwenda hospital kwa siri Bila hata mke wake kujua, baada ya ushahidi kupatikana na mchungaji kuchunguza na kujiridhisha na ushahidi wa mahusiano yao Hatimae kanisa likamtenga Jane  na wakwe wakamwambia John amfukuze Jane Nyumbani kwake baada ya kugundulika kuwa ni kweli John hana uwezo wa kumzalisha mwanamke na Alikuwa anajua siku nyingi ndio maana Alikuwa hataki kwenda na mkewe Jane kupata solution,  hivyo mtoto kweli hakuwa wake.

Itaendelea. ..........

Nini kiliendelea baada ya Jane kufukuzwa na mume wake?  Usikose sehemu ijayo

Mkasa wa kweli wa wanandoa Joseph na marry,  Je nini kiliendelea baada ya Jane kufukuzwa na mume,  mawifi na wakwe Nyumbani.

JE NANI ALAUMIWE?

Sehemu ya nne

Mke wa Joseph baada ya kusikia Majibu ya DNA ya metoka na Jane amefukuzwa na mume wake Nyumbani alifurahi sana,  ingawa kwa upande wa Jane mambo yalibadilika alichanganyikiwa akawa hajui itakuwaje  akiangalia Kazi hana akaamua kurudi Nyumbani kwao kwa mama yake.  Kama ilivyo kawaida mama ni mama akampokea mwanaye Maisha yakaanza upya,  mume wake marry kwa kuwa Alikuwa anampenda huyo Jane na ukizingatia tayari ana damu yake na ni kigogo akamwambia wala Usijali nitakuhudumia kwa sasa kaa Kwanza kwa mama. Marry akawa amefurahi sana kuwa amemuharibia ndoa yake mwenzie sasa anaishi kwa shida.

Kweli baada ya miezi kadhaaa akamchukua Jane na mtoto wake akawapangishia Nyumba nzima na kuwawekea furniture zote ndani Maisha yakaendelea kwa siri marry akijua kuwa Jane anaishi kwa shida Kumbe Jamaa Kamfata mtoto anamuhudumia maana Jane Alikuwa ni mzuri wa aina yake halafu ukimlinganisha na marry kwake Alikuwa bado mdogo ukichanganya na matunzo  hivyo Alikuwa analipa kuliko bimkubwa marry. Mahusiano yakaendelea kuwa ya siri maana Joseph Aliapa kutokumuacha Jane kwa kuwa tayari ana damu yake na yeye ndio kamsababishia hayo matatizo

 Baada ya miaka kazaa kupita Joseph  akaamua Kumpeleka shule naye Nyumba ndogo ili awe na yeye na Kazi ya kufanya ili kesho kesho kutwa ikitokea amekufa mtoto wake asipate shida,  Nyumba ndogo  akasoma na kumaliza chuo na baadaye kutafutiwa Kazi,  Maisha yakaendelea ya utumishi,  Nyumba ndogo akatambulishwa rasmi kwa baadhi ya ndugu Pamoja na mtoto wake ili kesho kesho kutwa wasije mkataa kuwa hawamjui,  Nyumba ndogo Jane Alikuwa mkarimu,  mpole, Mwenye heshima na kuwapenda ndugu wa mume wote kitu ambacho mke halali ili kuwa ni ndoto,  ndugu wote wakaanza kumpenda Nyumba ndogo,  mke halali wa Joseph akasikia kuwa Nyumba ndogo akatambulishwa na anajulikana  basi chaki ikazidi kwa ndugu wa mume na wote walio karibu na huyo Nyumba ndogo, but mume wake akamuambia ukweli kuwa ni kweli alikosea lakini hawezi  kumtelekeza huyo Nyumba ndogo  kwa sasa ataendelea kumhudumia yeye na mtoto mpaka pale ambapo labda mume wa Jane aamue kumsamehe na kuamua kuwa arudi Nyumbani,  lakini miaka Itaendelea kwenda hakuna dalili za Jane kurudi kwa mumewe, marry akaanza kutafuta alipopangishiwa Jane Nyumba na mume wake ili akamfanyie fujo na kumpiga Kwamba kwanini hataki kuachana na mume wake,  jitihada  za kupajua kwake zikagonga mwamba kwani kila aliyekuwa anamuuliza akawa anamuambia hajui Kumbe wanapajua ila wanaanzaje kumharibia ndugu yao ambaye ni Joseph?

Miaka Ikaenda kama ilivyo adha ya kulipa kodi kila wakati ilivyo Joseph akaamua kumnunulia Kiwanja kwa ajili ya maandalizi ya Nyumba,  baadaye akamjengea Nyumba nzuri ya kuishi ili   mtoto wake asipate shida,  Maisha yakaendelea Nyumba ndogo akiwa tayari ni mfanyakazi na ana Nyumba yake pia na Gari akanunuliwa La kutembelea, miaka ikasogea mbele Nyumba ndogo akapata ujauzito mwingine baadaye mtoto wa Pili akazaliwa na kama ilivyo kawaida wambea hawakosekani  taarifa zikamfikia bi mkubwa,  ikawa balaa ndani hapakaliki tena mke ugomvi mkubwa mpaka akaahidi kuondoka Nyumbani.

Je nini kilifuatia marry ataondoka kweli Nyumbani kwa mumewe kwenye lijumba La kifahari na kuziacha luxury zote?

Itaendelea..........
www.tujenganemedia. blogspot.Com



Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHUMBA

Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba; Jambo la kwanza –    Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu 2Wakorinto 3:17  ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’. Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya. Kum...

ZINGATIA HAYA UNAPOKUWA MBALI NA MWENZI WAKO

KAMA UKO MBALI NA MPENZI WAKO ZINGATIA HAYA Kama unaishi mbali na mpenzi wako kwanza kabisa unatakiwa kukubali kua mko mbali, huwezi na wala hutakiwi kucontrol kile anachokifanya kule, acha kufuatilia anafanya nini huko, yuko na nani na mambo kama hayo, kwa kfuupi wivu weka pembeni kwani ukiendekeza utachanganyikiwa. Kuna mambo mengi atayafanya mazuri na mabaya lakini kama hakuonyeshei basi huna haja ya kuyafukunyua. Jambo la pili ni mawasiliano haya ni muhimu na anapokupigia simu au unapompigia tumieni muda wenu vizuri kwa kuongelea kuhusu mapenzi na si kila siku “Mbona hukupokea simu yangu? Mbona nilikuona online hukujibu SMS zangu? Kulalamika sijui nimesikia hivi? Nimesikia vile!” Atakuvumilia kwa muda kisha itaboa na atakua anakwepa kuzungumza nawe na mwisho mapenzi yatakufa. Hata kama mnaongea dakika tano zifanyeni ziwe tamu zihusu mapenzi na si kuzozana mpaka mtu akitaka kupiga simu anawaza hivi nikiongea naye si kelele tu, hakuna mtu anapenda kupigia simu mtu aliyenuna....

VITU VYA MSINGI VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUDUMISHA UPENDO KATIKA MAHUSIANO

Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.” Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi. Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea, yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana. 1. Uaminifu Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote. Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako. Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano. Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli...