Skip to main content

KUJITAMBUA KATIKA WAKATI SAHIHI

Kujitambua katika maisha ni moja ya hatua kubwa ambayo humtofautisha mtu na mtu katika swala zima la mafanikio.
Nini maana ya kujitambua?
Ukizungumzia neno kujitambua kwa mtu yeyote ni  kuwa mtu sahihi, mahali sahihi, kwa muda sahihi.   Kuwa mtu sahihi maana yake ni kuwa mtu ambaye unajisimamia na kutekeleza kile ambacho unatakiwa kufanya wewe kama mwanadamu.
Mahali sahihi inamanisha kwamba upo kwenye kiwango ambacho ulistahiri kuwepo kimaisha kwa maana ya kwamba kiuchumi, kijamii na hata kisiasa.
 Asilimia kubwa ya vijana waliowengi hupoteza uelekeo wao wa maisha kwa kushindwa kujitambua katika umuri nyeti ambao bado vijana hawa wanakuwepo na nguvu za kutosha za kuwawezesha kushughulika na ndoto zao katika maisha.
 Tunapaswa kujitambua na kutambua kwamba chochote ambacho kinaonekana sasa katika Macho yetu ni mamzi mugumu yaliofanywa na watu kama sisi.  Vijana wengi tumekuwa na tabia furani ya kuiambia dunia tunachokifahamu badala ya kuonyesha Dunia unacho kifahamu kwa vitendo.
Maneno pekee hayawezi kukusukuma mbele katika kufikia ndoto zako. Unapaswa kujielekeza katika vitendo zaidi juu ya kile unachozungumzia kuliko nadharia.
Ili kugundua kwamba umejitambua lazima uwe na uwezo wa kujibu haya maswali
1. Kwanini upo hapa duniani?
2. Wewe ni nani hapa Duniani?
3. Kwanini upo katika hali hiyo ulionayo kimaisha?
4. Ni nani anapaswa kulaumiwa katika wewe kuwa hivyo ulivyo kimaisha?
5. Ni nani anathirika kupitia wewe kuwa hivyo?
6. Je anawajibu wowote wa kukutoa katika hali hiyo kwa sasa?
7. Akishindwa kukutoa katika hapo ulipomtegea kuchukua mamzi mugumu kuna madhara yoyote ya moja kwa moja yatakayompata?
8. Kwa nini afikirie kwa ajili ya maisha yako
9. Ikitokea leo akasimamisha tabia ya kufikiri kwa niaba yako utaweza kujimudu?
 Majibu yatakayotokana na kujiuliza hayo maswali yatakusaidia kujijenga na kuchukua jukumu la kufanya mamzi magumu kuyatumikia maisha yako.

UMUHIMU WA KUJITAMBUA KAMA KIJANA.

kujitambua kama kijana katika muda sahihi,  mazingira sahihi na umuri sahihi kuna faida na umuhimu mkubwa katika kubadili maisha yako.  Hakuna aliefanikiwa na kutimiza ndoto zake pasipo kujitambua.  Hiyo ndio mbegu pekee ambayo ilipandwa na watu ambao sasahivi tumekuwa tukiwa shabikia kwa manufaa binafsi.
1.kujitambua husaidia mtu kuwa tofauti na kufikiria vitu chanya ambavyo ni tofauti kabisa na wengine katika jamii inayo mzunguka.  Kumbuka kwamba huwezi kuwa mtu tofauti katika jamii kwa kufikiria vitu sawia na wengine.
2. Husaidia kufikia ndoto zako kirahisi
3. Husaidia kujenga uaminifu na watu katika jamii.  Ikumbukwe kwamba mafanikio yoyote huletwa na watu wanao kuzunguka katika muda sahihi.
4. Husaidia kujenga saikolojia

MAMBO YANAYOWEZA KUSADIA KUJITAMBUA KWA HARAKA NA KUWA MTU SAHIHI KATIKA MAISHA YAKO:

1: Kwepa mazingira hasi
2: Wekeza kwenye utafutaji wa maarifa sahihi na endelevu
3: penda kujitegemea hata kwa kidogo ulicho nacho
4: Jifunze kuwa mtu sahihi muda wote katika maisha yako.
4: fuatilia na kuyajua mapungufu ili uweze kuwepuka kurudia rudia udhaifu muda mwingi.
5: Chagua mahali sahihi pa kuelekeza maisha yako  ( Driven power )
6: Epuka ukusanyaji wa taarifa zisizo za lazima.  Chagua taarifa sahihi na zifanyie utafiti kabla hujaruhusu zianze kuendesha maisha yako.
7: Tathimini mamzi unayofanya kabla ya matumizi yake katika maisha.
8: Chagua mtu sahihi wa kukuongoza katika kufikia unakotaka kufika kimafanikio.
9: Jenga tabia ya kushinda mambo hasi
10. Jenga utamaduni wa kujisemesha semesha katika mtazamo chanya ili ukae kichwani mwako. ... nk

Makala hii itaendelea hapo badaye  . Tunakushauri usiwe mbali na tujenganemedia.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...