Skip to main content

MAFANIKIO HUANZA NA FIKIRA.



                 
                         


MAFANIKIO HUANZA NA FIKIRA
Nimependa kushare nanyi kidogo baada ya kufanya utafiti ambao sio rasmi saana, hasa tukizungumzia mada ya Mafanikio. Watu wengi hasa sisi vijana tumekuwa tukichukulia mafanikio kama tukio....(Success as an event) lakini ukweli ni kwamba mafanikio au Kufanikiwa katika jambo lolote ni Mchakato(a process) ambao unakuwa na Mkakati Fulani/ Maalumu (strategy). Mchakato huo maalumu lazima uanzie akilini kwanza. Tunapoongelea Mafanikio katika chochote ni lazima kwanza kuamini katika kufanikiwa ndipo tuandae mkakati ambao utakusaidia au ambao utakuwa ndio njia ya kukufikisha kwenye Mafanikio. Ukweli ni kwamba Huwezi yafikia Mafanikio Makubwa yoyote halali yenye Thamani Bila Kuamini kwanza katika Mafanikio na kujenga mtazamo Chanya juu ya kile unachokiendea. Lakini Kwa Kumalizia Unaweza kuamini katika Mafanikio na ukawa na Mkakati bila Matendo Nazi (Plan of Action) bado inakuwa haina maana. Lazima kupanga matendo kazi yatakayokupitisha kwenye huo Mkakati ili kuyafikia Mafanikio hayo......Wengi huwa tunaamini kuwa IPO  SIKU nami nitafanikiwa....Kibaya ni pale unapoamini hivyo huku ukiwa huna mkakati wowote, that's wrong(ni mbaya saana, wala sio sahihi). So anza kuamini Kuhusu Mafanikio kisha weka mkakati na Matendo kazi.....Kisha twende tukapige kazi....Always Utakatishwa Tamaa katika mpango huo au Malengo hayo...Don't look back...Fight Fight Fight wengine wanasema. Do it and Do it and Do it and Do it and Do it again and again and again Until the Job get done.....Hapo lazima ukifikie kile unachokitaka. Nawaasa vijana wenzangu twendeni Tukafanye kazi.....Tuache Kuamini kwenye Bahati.

USIPOTEZE NDOTO ZAKO KWA VITU VIDOGO VIDOGO  (TAMAA )

Nirahisi kila mtu kuweka malengo na mipango yake mizuri ndani ya muda fulani,
Lakini kufikia mipango hiyo imekuwa ngumu kwa watu wengi sana na hivyo kujikuta wamesha jipoteza na kupoteza mipango yao.

Kujipoteza na kupoteza mwelekeo kwenye maisha yenye malengo kunatokana na tamaa za muda mfupi hasa unapo kuwa na malengo ya mda mrefu na hapo ndipo akili inakuwa rahisi kuhamia kwenye mambo yaliyo ya kawaida na sio yale mtu alipanga kukamilisha kwa muda alio jipangia.

Tamaa ya vitu vidogo vidogo na vilivyo rahisi kupatikana ndio kizuizi cha watu wengi kufikia malengo yao makubwa,
Mambo madogo madogo ndiyo yanayo ongozwa na hisia za tamaa na hivyo watu kujikuta kupata vitu hivyo badala ya malengo yao yaliyo makubwa.

Malengo Makubwa na ya mda mrefu mala nyingi hayafikiwi kwa sababu ya vitu vidogo ambavyo havikuwepo kwenye mipango yoyote ya awali,
Mfano:Watu wengi wamekuwa na mipango mikubwa na ya mda mrefu lakini wanapo kuwa katikati ya utekelezaji wa mipango hiyo kunajitokeza vitu vidogo vidogo vinavyo kuwa rahisi kuvipata kutokana na urahisi wa kuvipata basi akili huanza kufikiri na kutorokea kwenye vitu hivyo badala ya mipango yao na pindi muda wao unapo kuwa umeisha ambao walijipangia kwenye lengo lao hujikuta wana vitu ambavyo hawa kutegemea wala kupanga na hivyo kuongeza muda wa mipango yao.

Rafiki kuepuka kuathiriwa na tamaa zinazo weza kuwa kuzuizi kwako kufikia mipango yako ni Wewe kutambua umuhimu wa mpango wako,Kujiwekea nidhamu binafsi na kuhakikisha hutoki nje ya mpango wako,Kujikumbusha mala kwa mala na kuona ukubwa wa mpango wako,Uking'ang'anizi  na mengine mengi.

Hakikisha hutoki nje ya chaki au mpango wako huo,
Hakikisha mambo mengine yote yanasimama hasa yanayo hitaji fedha zako hata kama ni kidogo,
Hakikisha usiku na mchana unapata muda wa kutafakari mpango wako na kupanga mbinu zaidi kuufanikisha kwa kila namna.
Mwisho kabisa Epuka kutembea na fedha zisizo kuwa na mpango wowote kwenye ratiba yako ya siku,
Epuka tamaa ya aina yoyote inayo
 chochewa na uwepo wa fedha zako.

 MWISHO KABISA KUMBUKA HIKI :

unapotazama mwenzako kafanikiwa ukamuwekea mashaka, ujue ndivyo hivyo na wenzio wanakuwekea mashaka ya kwanini siyo wewe ufanikiwe??. mungu siku zote hawezi kuelekeza mafanikio kwa watu wenye roho wa kwanini katika maendeleo. ukiona mwenzio kapiga hatua furani katika maisha unapaswa kumpongeza na kumtia moyo kwa sababu baada ya huyo ni zamu yako inayofuata katika kufanikiwa....
 kadiri unavyozidi kujitenga na watu ndivyo hivyo unajitenga  na ujio wa mafanikio , kumbuka kwamba mafanikio yako yako mikononi mwa watu wengine. hata waliofanikiwa walikuwa na watu waliokuwa wanawaunga mkono katika biashara zao kwa kununua bidhaa zao na kama wangesusiwa na wanadamu kamwe wasingefikia mafanikio hayo.Muhimu ni kwamba ishi na watu upate vitu na ukiamua kujitenga na watu shariti uyasahau mafanikio


Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...