KAMA UKO MBALI NA MPENZI WAKO ZINGATIA HAYA
Kama unaishi mbali na mpenzi wako kwanza kabisa unatakiwa kukubali kua mko mbali, huwezi na wala hutakiwi kucontrol kile anachokifanya kule, acha kufuatilia anafanya nini huko, yuko na nani na mambo kama hayo, kwa kfuupi wivu weka pembeni kwani ukiendekeza utachanganyikiwa. Kuna mambo mengi atayafanya mazuri na mabaya lakini kama hakuonyeshei basi huna haja ya kuyafukunyua.
Jambo la pili ni mawasiliano haya ni muhimu na anapokupigia simu au unapompigia tumieni muda wenu vizuri kwa kuongelea kuhusu mapenzi na si kila siku “Mbona hukupokea simu yangu? Mbona nilikuona online hukujibu SMS zangu? Kulalamika sijui nimesikia hivi? Nimesikia vile!” Atakuvumilia kwa muda kisha itaboa na atakua anakwepa kuzungumza nawe na mwisho mapenzi yatakufa.
Hata kama mnaongea dakika tano zifanyeni ziwe tamu zihusu mapenzi na si kuzozana mpaka mtu akitaka kupiga simu anawaza hivi nikiongea naye si kelele tu, hakuna mtu anapenda kupigia simu mtu aliyenuna. Lakini mnapotembeleana hembu dili na mambo yako, sio unafika na kuanza kuchunguza majirani, kuchunguza nani anaingia nani anatoka.
Kuanza kutafuta umbea na vitu kama hivyo, labda kama unataka kumuacha lakini kama bado unampenda basi hayakuhusu sanasana kama humuamini sana muambie mkapime kabla ya chochote ila tofauti na hapo ukitaka kuchunguza utakuta unawachukia majirani, wafanyakazi wenzake na hata marafiki kwani watakua na ukaribu ambao watu watadhani ni wapenzi.
Hata kama mtu anakupenda vipi, hata kama ni muaminifu namna gani lakini kama ukitilia shaka kila kitu basi jua kuwa ndiyo mwanzo wa kuharibu mapenzi yenu. Mnapokua mbali mnakua hamna muda wa kuonana kila saa hivyo zile dakika mnazoongea na zile siku mbili tatu mnazokutana ukizitumia vizuri basi hata kama alikua na madudu yake atakua akifurahia kuongea na kukutana na wewe.
PIA ZINGATIA HAYA HASA KWA WANAWAKE NA MABINTI
Kama wewe ni mwanamke na unampigia simu mpenzi wako mara tatu kwa siku halafu yeye hapigi hata mara moja kwa siku basi punguza, piga mara moja au hata usipige kabisa, muache yeye ndiyo akupigie mara nyingi, muache yeye ndiyo akumiss zaidi. Jinsi unavyozidi kuonyesha kuwa umechanganyikiwa zaidi kwa mwanaume ndiyo jinsi ambavyo anazidi kukuchoka, simu zako zinatoka kuwa “Baby nimekumiss” mpaka kuwa “Kwanini hupokei simu zangu”
Najua wanawake wengi hudhani kua kwa kumpigia simu mwanaume mara kwa mara, kwa kumtumia meseji nyingi ndiyo kuonyesha kuwa unamjali. Hapana vichwani mwa wanaume ukimtafuta sana ni kama unamuambia kuwa sina kazi nyingine ya kufanya zaidi ya kukupenda wewe na unaacha kuwa mpenzi na kuwa “Yule mwanamke msumbufu” najua wengi mnaogopa na kuwaza kuwa usipomtafuta atatafutwa na wanawake wengine!
Inawezekana kuwa kweli lakini kama mwanaume hawezi kukutafuta hata mara moja kwa siku, hawezi kukumiss hata kwa bahati mbaya inawezekana unahitaji mwingine na huyo anapaswa kubaki kwa hao wengine. Najua huwezi kumuacha lakini hembu acha kujipendekeza wewe, acha kuchanganyikiwa wewe na mpe nafasi ya kutambua thamani yako, mwanaume akishajua huendi popote anaanza kuyaona mapenzi yako kama kero.
Kiasilia wanaume sisi ndiyo tunatongoza na sisi ndiyo tunataka kutaka na si kutakwa, unapomtaka mwanaume zaidi ya anavyokutaka wewe basi jua ni tatizo na hapo ndiyo ambavyo maumivu huanzia hivyo hata kama ni kweli unampenda zaidi lakini hembu vumilia na jifunze kuacha kua wewe ndiyo mtu wa kumtafuta. Acha kuonyesha kwamba maisha yako hayawezi kwenda au huwezi kuwa na furaha bila yeye, kama umemtafuta mara mbili hajakutafuta ya tatu kaa kimya hata kama itachukua mwezi.
Acha kuwa tambara lake la deki,
Mara nyingi hii hutokea kwa wanawake, kwamba umekutana na kijana, kakutongoza vizuri, umeeneda alikua anakusumbukia, anahangaika na wewe lakini akishakupata tu, ukampa mwili wako na kipande cha moyo wako ghafla anabadilika. Hakutafti tena kama awali, hakupigii simu, hafanyi chochote.
Badala ya kuka akujiuliza kilichotokea basi unaanza wewe kuhangaika naye kana kwamba unamtongoza, unampigia simu mara mia, meseji mia mbili na hata hajibu. Lakini hiyo si ishu ishu nikuwa akikuhitaji ana uchafu wake wewe unaenda kuusafisha, yaani akiwa na ashida zake wewe ndiyo unaitwa na unajipeleka.
Anakudanganya na ujinga ujinga kuwa sasa hivi niko bize kana kwamba eti kabadilisha kazi, kwani wakati akikutongoza alikua Diwani na sasa kawa Raisi tuseme amekua bize sana. Mbona alikua anakutumia meseji kila siku, anakupigia simu kila siku anahangaika na wewe lakini ghafla sasa hakuhitaji tena
Iko hivi mwanzoni alikua anakuthamini kwani ulikua kama T-Shirt ambayo anaivaa kila akitoka lakini sasa kashakutumia kakufanya gunia lake la deki anakutafuta tu pale akitaka kufuta miguu na kuondoa uchafu. Hembu amua na sema hapana mimi si gunia la deki, jithamini na kama asipokuthamini basi muambie kwa heri.
Halafu Dada zangu acheni haka kakitu kuwa wanaume wote wako hivyo, nani katembea na wote. Kama hakujali hakuthamini jua hakupendi kuna mtu anamjali na anamthamini, acha kumuendekeza na kama hakufai ukimhitaji na wewe akikuhitaji usimfate uone kama hatabadilika na asipobadilika kwaajili yako basi huyo hakua riziki yako acha kuwa tambara la deki.
DALILI KUMI KWAMBA MWANAUME ULIYENAYE ANAKARIBIA KUKUACHA/ASHAKUCHOKA
Mabadiliko katika mapenzi ni kitu cha kawaida sana, wakati mwingine mtu anahitaji muda wa peke yake, muda wa kutafakari mambo. Lakini kuna mambo mengine yakitokea unapaswa kuamka na kujua kua kuna kitu.
Mara nyingi wanawake ni vipofu katika mabadiliko, wanaachwa na kuonyeshwa dalili zote za kuachwa lakini bado wanang’angania hawaoni, zifuatazo ni dalili kumi kuwa mwanaume wako hakutaki tena kashakuchoka na anakaribia kukuacha.
(1) Anawasiliana, anatamani na kuongea kimahaba na wanawake wengine mbele yako. Wala hajli upo, hajali kuwa anakuumiza, hajali kama unahisia, atawasilina na wanawake wengine, ataongea nao na kuongea maneno ya kukuumiza huku akikudharau mbele yao. Dada Unaachwa!
(2) Hakuchukulii siriasi tena; Yaani unaweza kuongea kitu wala hajali, mnaahadi hatokei na wala haombi msamaha, kuna kitu cha muhimu kinachokuhusu wewe wala hajali na haumizi kichwa, ukiongea hakuchukulii siriasi atakebehi na kukashifu kila unachoongea. Dada Unaachwa!
(3) Hakupigii tena simu wala kujibu meseji zako; Zamani ukibeep tu anapiga, lakini sasa wala hata hajali na ukipiga atakuambia nitakucheki ila ndiyo nitolee. Meseji ndiyo hajibu, yuko online au kwenye group, anacomment post ila wewe wala nikama vile haupo. Dada Unaachwa!
(4) Hakuonyeshi Tena Mahaba; Mambo ya kushikana mikono kama zamani hakuna, hataki hata kuongozana na wewe na wala kukushika sehemu lizokua anakushika awali, anakukwepa kwepa na mbele ya marafiki anajifanya kama vile si mtu wake. Kama alikua anafanya hayo mambo awali na sasa hafanyi… Dada unaachwa!
(5) Hataki tena kufanya mapenzi na wewe; Yaani imekua kama adhabu, mnaonana lakini wala hakutaki tena. Zamani alikua akikuona tu mziki wake unchanganyikiwa ila sasa ni kama unalazimisha. Hata kama ukiomba mechi ukifika hakuna rommnce wala kushikana kama analima vile kanyaga twende anakucha anaendelea na mambo yake. Dada Unaachwa!
(6) Anakuambia nataka kuwa peke yake “More Space” Kuna mambo anafikiria msionana. Mkipanga anakuambia atakutafuta na wiki inaisha hakutafuti. Dada kama una mwezi hujaonana na mpenzi wako mko sehemu moja anakupiga chenga wewe ndiyo ushaahwa. Mwanaume anamkwepa mwanamke akiwa na mwingine anampa huduma zote na si vinginevyo hivyo kama anataka space Dada Unaachwa!
(7) Hataki kuongelea tena mambo ya mapenzi; Zamani mlikua mkikaa kidogo anazungumzia maisha, watoto, sijui mapenzi yenu, mahusiano yenu na mahaba. Ila sasa wala hataki, ukiongelea hayo mambo anabadilisha mada, kukasirika na hata kuongea. Dada unaachwa!
(8) Hakusifii tena; Kuna wale wanaume ambao hata hawana hayo mambo, ila kama alikua anajua umevaa nguo mpya, umesuka ana kusifia umefanya kitu kizuri anakusifia ila sasa hata ukipendeza vipi hasifii ni kama vile hata hakuoni na hata ukimuambia wala hajali anajifanya yuko bize na mambo yake. Dada Unaachwa!
(9) Hakuheshimu tena; Zamani alikua akikuheshimu wewe kama mwanamke, anaheshimu kazi yako na ndugu zako, lakini sasa wala hajali, anakudharau anaweza kukudhalilisha mbele za watu na asijali, akakuona unadhalilika na wala hajali na kila wakati ni kutafuta neno hata moja la kukuudhi. Dada Unaachwa!
(10) Ameacha kuongele amambo ya ndoa: Ndiyo kuna ambao wala hawakua wakizungumzia hayo awali achana na hao. Ila kuna yule ambaye kila siku alikua ni namna akikuoa, namna sijui mkifanya hivi, mipango yake yote ilikua inakuhusiha na wewe.
Ila sasa daa hazungumzii tena mambo ya ndoa, yaani ukigusa hayo anakasirika na hata kukutukana. Au utasikia anasema mimi suala la ndoa sasa hivi bado, nataka nijinge kwanza, siwezi kuoa mpaka lini, sijui nataka mwanamke wa namna flani wakati upo na vitu kama hivyo. Dada ukiona hivyo jua Unaachwa.
Nimalizie kwa kusema kuwa hizi ni dalili tu kuwa huyu mtu kakuchoka na anataka kukuacha au kichwani kwake ashakuacha na ana mtu mwingine. Sasa kama anakufanyia yote haya wewe ushaachwa kabisa na ni wakati wakuwaza maisha mapya.
Lakini si wakati wa kukata tamaa, niwakati wa kuanza kujipenda na kujifanyia mambo yote ambayo unaona yatakupafuraha. Kuacha kujipendekeza na kumsujudia na kuanza kujipenda wewe kwa kujifanyia mambo yanayokupa furaha.
SOMA USHUHUDA HUU KWA MAKINI.
Binti mmoja alikua amekaa kibarazani analia, simu yake bado alikua ameishikilia mkononi anatetemeka. Alitokea Bibi mmoja ambaye hata hawakua wakifahamiana, yule Bibi alikaa pembeni yake na kumuuliza ni kwanini binti mzuri kama yule alikua analia mchana wote ule. Huku akiendelea kulia, binti alianza kumlaumu Mungu, akisema haamini kweli kama Mungu yupo.
Alisema yeye anamuomba Mungu kila siku, anatoa sadaka, anasaidia masikini na anafunga lakini Mungu amemdanganya kwa muda mrefu na sasa kamuacha analia. Bibi alimuuliza ni nini kimetokea lakini binti aliendelea kulia huku akilalamika akisema, mimi nimempa Mungu maisha yangu yote lakini ameshindwa kunipa kitu kimoja tu nilichokua namuomba kila siku. Bibi alimuuliza kitu gani binti akamuambia ndoa.
Alimuambia mpenzi wangu wa miaka saba ameniacha na kumuoa rafiki yangu kupenzi, niliwafumania na kumuomba msamaha lakini pamoja na mimi kutokukosea amenitumia meseji kuwa hanitaki na sasa anamuoa rafiki yangu, kweli Mungu yupo? Kweli ananipenda? Angekua ananipenda angenifanyia yote haya, angeniumiza hivi?
Bibi alimuangalia na kutabasamu, kisha akamuambia Mungu anakupenda na ndiyo maana aliruhusu umfumania rafiki yako na mpenzi wako kabla ya kukuoa! Asingekua anakupenda asingekufungua macho! Binti alikasirika na kuanza kutukana tena akidhani Mungu hampendi. Yule Bibi alimsogelea akamshika macho kisha yule Binti alilala palepale na kupata usingizi mzito, akiwa amelala Binti alianza kuota.
Aliota harusi kubwa ya yeye na mpenzi wake, watu wengi wamehudhuria na kila mtu anafuraha, rafiki zake wote wapo hata yule aliyemfumania yupo na anafurahia ndoa yao. Baada ya harusi alipata ujauzito, yeye na mume wake walikua wanaishi ndoa ya raha sana, alichukua mkopo Ofisini kwao na kumalizia kujenga nyumba yao, baada ya kumaliza tu kujenga alishangaa ghafla mume wake kabadilika, hampendi tena na hamhudumii kwa chochote.
Siku moja akiwa ametoka kazini na mimba yake, alimfumania mumewe akiwa na yule rafiki yake katika nyumba aliyojenga na mume wake, tena katika chumba kilekile anacholala na mumewe. Alipoongea mume wake alimpiga sana wakimchangia pamoja na rafiki yake, baada ya hapo akiwa maepoteza fahamu waliondoka na kumuacha. Asubuhi alizinduka na kupata msaada kutoka kwa majirani ambao walimsaidia kumpeleka Hospitalini, mimba ilitoka.
Kwa bahati mbaya wakati anasafishwa alitolewa kizazi na kuambiwa hatapata mtoto tena, alirudi nyumbani akiwa hana matumaini ya kuishi na mumewe liporejea na kusikia tena zile taarifa alimuacha akimuambia hawezi kukaa na mwanamke ambaye hazai. Palepale alistuka huku akitetemeka, hakumuona yule Bibi lakini alikuta kiratasi kilichokua pembeni yake, alikifungua na kukisoma, kilikua kimeandikwa.
“Unaona namna Mungu anavyokupenda, hakutaka upitie yote hayo ndiyo maana akakufungua macho sasa. Usiachae kumuombe kwani yeye hatendi kama tunavyotaka sisi bali hutenda kwa namna yake.” Binti alijikuta analia, sasa hivi hayakua machozi ya huzuni bali machozi ya shukurani kwani Mungu alikua amemuepushia mambo mengi. Siku iliyofuata alienda kutoa sadaka nyingine na kumshukuru Mungu kwa wema wake.
Asante sana na Endelea kufuatilia makala zetu za kila siku katika blog yako ya tujengane media.

Comments
Post a Comment
asante kwa kuichagua tujengane media kuwa sehemu yako ya kujifunza