Skip to main content

Ripoti mpya za shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa ugonjwa wa shinikizo la damu ndio  ugonjwa ambao unaathiri watu wengi zaidi barani Afrika huku ikionesha asilimia zaidi ya 10 ya Waafrika wameshapata na ugonjwa huo.



Kwa mujibu ripoti hiyo imeeleza sababu kubwa za kuzidi kuongezeka kwa ugonjwa huo kuwa ni watu kupuuza kufanya mazoezi, kupunguza au kutotumia kabisa matunda angalau matano na mboga kwa siku, matumizi ya tumbaku au sigara na pombe zimetajwa kama njia kuu za kushindwa kupambana na yote yasiyoambukiza ikiwemo Moyo, Kisukari na Kansa.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), imeonesha pia robo ya watu wazima kutoka nusu ya nchi za Afrika zilizofanyiwa utafiti wameathiriwa na sababu tatu za hatari zinazoongeza uwezekano wa kuwa na moja au zaidi ya magonjwa mengine hatarishi wakati wa maisha yao.
WHO inaonyesha kuwa wanawake wa Afrika wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa haya.
Wakati ambapo matumizi ya tumbaku au sigara na pombe yako kiwango cha chini barani Afrika kuliko sehemu zingine duniani, shinikizo la damu liko katika kiwango cha juu zaidi duniani, na kuathiri karibu nusu ya ya watu wazima barani Afrika.
Kwa mujibu wa WHO, kiwango hicho kinatisha kwa sababu ugonjwa huo unaathiri pole pole na mara nyingi unagunduliwa baada ya miaka kadhaa ukiwa umeshafanya madhara makubwa kwa mgonjwa. Pia ripoti hiyo imeonesha kuwa bara la Afrika ni sehemu pekee watu wanakabiliwa na utapiamlo na fetma.
WHO imeeleza kuwa matatizo haya yanaweza kuzuiwa kwa watu kula vizuri, kunywa kwa kiasi na kufanya mazoezi na endapo tahadhari hizi hazizingatiwi, hali hii inaweza kupelekea kuzigharimu serikali mabilioni ya pesa kwenye matibabu ya wagonjwa wake.




Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...

ZINGATIA HAYA UNAPOKUWA MBALI NA MWENZI WAKO

KAMA UKO MBALI NA MPENZI WAKO ZINGATIA HAYA Kama unaishi mbali na mpenzi wako kwanza kabisa unatakiwa kukubali kua mko mbali, huwezi na wala hutakiwi kucontrol kile anachokifanya kule, acha kufuatilia anafanya nini huko, yuko na nani na mambo kama hayo, kwa kfuupi wivu weka pembeni kwani ukiendekeza utachanganyikiwa. Kuna mambo mengi atayafanya mazuri na mabaya lakini kama hakuonyeshei basi huna haja ya kuyafukunyua. Jambo la pili ni mawasiliano haya ni muhimu na anapokupigia simu au unapompigia tumieni muda wenu vizuri kwa kuongelea kuhusu mapenzi na si kila siku “Mbona hukupokea simu yangu? Mbona nilikuona online hukujibu SMS zangu? Kulalamika sijui nimesikia hivi? Nimesikia vile!” Atakuvumilia kwa muda kisha itaboa na atakua anakwepa kuzungumza nawe na mwisho mapenzi yatakufa. Hata kama mnaongea dakika tano zifanyeni ziwe tamu zihusu mapenzi na si kuzozana mpaka mtu akitaka kupiga simu anawaza hivi nikiongea naye si kelele tu, hakuna mtu anapenda kupigia simu mtu aliyenuna....