Skip to main content

sulemani mwana wa daudi

    Methali za Sulemani+ mwana wa Daudi,+ mfalme wa Israeli:+  Ili mtu ajifunze* hekima+ na nidhamu;Ili aelewe maneno ya hekima;  Ili apate nidhamu+ inayoleta ufahamu,Uadilifu,+ busara,*+ na unyoofu;*  Ili kumfanya mjinga awe mwerevu;+Ili kumpa kijana ujuzi na uwezo wa kufikiri.+  Mtu mwenye hekima husikiliza na kujifunza zaidi;+Mtu mwenye uelewaji hupata mwelekezo stadi*+  Ili kuelewa methali na fumbo,*Maneno ya wenye hekima na vitendawili vyao.+  Kumwogopa* Yehova ndio mwanzo wa ujuzi.+Ni wapumbavu tu wanaodharau hekima na nidhamu.+  Mwanangu, sikiliza nidhamu ya baba yako,+Wala usiyaache mafundisho* ya mama yako.+  Ni shada linalovutia kwenye kichwa chako+Na pambo maridadi shingoni mwako.+10  Mwanangu, watenda dhambi wakijaribu kukushawishi, usikubali.+11  Wakisema: “Njoo twende.Acha tuvizie ili kumwaga damu.Tutajificha na kuwashambulia bila sababu watu wasio na hatia.12  Tutawameza wakiwa hai kama Kaburi*linavyomeza,Wazima-wazima, kama wale wanaoshuka shimoni.13  Na tunyakue mali zao zote zenye thamani;Nyumba zetu tutazijaza nyara.14  Unapaswa kujiunga nasi,*Nasi sote tutagawana sawasawa vitu tunavyoiba.”*15  Mwanangu, usiwafuate.Iepushe miguu yako na njia yao.+16  Kwa maana miguu yao hukimbilia kutenda uovu;Wanaenda haraka kumwaga damu.+17  Kwa kweli ni kazi bure kutandaza wavu huku ndege akitazama.18  Ndio sababu wanavizia ili kumwaga damu;Wanajificha ili wawaue* wengine.19  Hizo ndizo njia za wale wanaotafuta faida isiyo ya haki,Ambayo itawaangamiza wale wanaoipata.+20  Hekima ya kweli+ hupaza sauti kubwa barabarani.+Huendelea kuinua sauti yake katika viwanja vya jiji.+21  Hupaza sauti kwenye makutano ya barabara zenye watu wengi.Nayo husema hivi kwenye malango ya jiji:+22  “Ninyi wajinga mtaendelea kuupenda ujinga mpaka lini?Nanyi wadhihaki mtaendelea kufurahia dhihaka mpaka lini?Nanyi wapumbavu mtaendelea kuchukia ujuzi mpaka lini?+23  Sikilizeni karipio langu.*+Ndipo nitakapowamiminia roho yangu;Nitawajulisha maneno yangu.+24  Kwa sababu niliwaita, lakini mkaendelea kukataa,Niliunyoosha mkono wangu, lakini hakuna yeyote aliyejali,+25  Mliendelea kupuuza ushauri wangu woteNa kukataa karipio langu,26  Mimi pia nitawacheka mtakapopatwa na msiba;Nitawadhihaki jambo mnaloogopa litakapokuja,+27  Jambo mnaloogopa litakapokuja kama dhoruba,Na msiba wenu utakapofika kama upepo wa dhoruba,Wakati dhiki na taabu zitakapowapata.28  Wakati huo wataendelea kuniita, lakini sitajibu;Watanitafuta kwa bidii, lakini hawatanipata,+29  Kwa sababu walichukia ujuzi,+Nao hawakuchagua kumwogopa Yehova.+30  Walikataa ushauri wangu;Waliyadharau makaripio yangu yote.31  Basi watapata matokeo* ya njia yao,+Nao watashiba kabisa mashauri yao* wenyewe.32  Kwa maana upotovu wa wajinga utawaua,Na kutojali kwa wapumbavu kutawaangamiza.33  Lakini yule anayenisikiliza ataishi kwa usalama+Naye hatahangaishwa na woga wa msiba.”+

Comments