Skip to main content

USHUHUDA WA YOHANA MBATIZAJI

Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji
19 Lk 3:15,16 Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? 20Mdo 13:25 Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. 21Kum 18:15,18; Mal 4:5; Mt 17:10; Yn 6:14; 7:40 Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. 22Basi wakamwambia, U nani? Na tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wanenaje juu yako mwenyewe? 23Isa 40:3; Mt 3:3; Mk 1:3; Lk 3:4Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya. 24Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo. 25Mt 21:25 Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule? 26Mt 3:11; Mk 1:7,8 Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. 27Yn 3:26; Mdo 13:25 Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza kamba ya kiatu chake. 28Mt 3:6,13 Hayo yalifanyika huko Bethania ng'ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.
Mwana-kondoo wa Mungu
29 Yn 1:36; Isa 53:7 Kesho yake alimwona Yesu akija kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30Yn 15:27 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 31Wala mimi sikumjua; lakini ili adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nilikuja nikibatiza kwa maji. 32Mt 3:16; Mk 1:10; Lk 3:22 Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. 33Lk 3:2; Mt 3:16Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenituma kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. 34Mt 3:17Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.



Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...