Skip to main content

Hekima inayotuongoza Maishani

, Yehova ni Mtawala mwenye hekima? Njia moja yenye kuridhisha ya kujibu swali hilo ni kuchunguza mashauri anayotoa. Je, yanafanya kazi? Je, kuyatumia kunafanya maisha yawe mazuri zaidi na yenye kusudi? Mfalme Sulemani mwenye hekima aliandika mamia ya methali. Methali hizo zinazungumzia nyanja zote za maisha. Fikiria mifano kadhaa.
Kumtegemea Mungu. Ili kuwa na uhusiano mzuri pamoja na Yehova, lazima tumtegemee. Sulemani aliandika: “Mtegemee Yehova kwa moyo wako wote wala usitegemee uelewaji wako mwenyewe. Mtambue yeye katika njia zako zote, naye atanyoosha mapito yako.” (Methali 3:5, 6) Kumtegemea Mungu kwa kufuata mwongozo wake na kumtii hufanya maisha yawe na kusudi. Mtu anayefanya hivyo huufurahisha moyo wa Mungu na kumpa Yehova jibu la masuala yaliyozushwa na mpinzani Wake, Shetani.—Methali 27:11.
Kushughulika na watu wengine kwa hekima. Leo, kuliko wakati mwingine wowote, tunafaidika na shauri la Mungu kwa waume, wake, na watoto. “Ushangilie pamoja na mke wa ujana wako,” Mungu awashauri waume, akiwaagiza wawe waaminifu kwa wake zao. (Methali 5:18-20) Wanawake walioolewa wanaweza kufaidika na ufafanuzi wenye kupendeza ulio katika kitabu cha Methali kuhusu mke mwenye uwezo anayejipatia sifa kutoka kwa mumewe na watoto wake. (Methali, sura ya 31) Nao watoto wanaagizwa wawatii wazazi wao. (Methali 6:20) Kitabu hicho kinaonyesha kwamba urafiki ni muhimu, kwa kuwa kujitenga hutokeza ubinafsi. (Methali 18:1) Marafiki wanaweza kuwa na uvutano mzuri au mbaya, kwa hiyo tunapaswa kuwachagua kwa uangalifu.—Methali 13:20;17:17.
Kujitunza kwa hekima. Kitabu cha Methali kina mashauri mazuri kuhusu kuepuka matumizi yasiyofaa ya vileo, kusitawisha hisia zinazofaa na kuondolea mbali zisizofaa, na kuwa mfanyakazi mwenye bidii. (Methali 6:6; 14:30;20:1) Kitabu hicho kinaonya kwamba kutegemea akili ya mwanadamu na kupuuza shauri la Mungu hutokeza msiba. (Methali 14:12) Kinatuhimiza tumlinde yule mtu wa ndani, moyo wetu, dhidi ya uvutano mbalimbali usiofaa, na kutukumbusha kwamba katika moyo “ndiko zinakotoka chemchemi za uzima.”—Methali 4:23.
Mamilioni ya watu ulimwenguni wamejionea kwamba kuishi kupatana na mashauri hayo hufanya maisha yawe mazuri zaidi. Kwa sababu hiyo, wana sababu nzuri ya kumkubali Yehova kuwa Mtawala wao.
—Inatoka kwenye Kitabu cha Methali.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...