Skip to main content

Kwa Nini Uichunguze Biblia?

Je, wewe unaifahamu Biblia? Hakuna kitabu kingine chochote katika historia ambacho kimesambazwa sana kama Biblia. Ujumbe wake umewafariji na kuwapa tumaini watu wa tamaduni zote, nao wamefaidika na mashauri yake maishani. Hata hivyo, watu wengi leo hawaijui Biblia vizuri. Iwe wewe ni mfuasi wa dini fulani au sivyo, huenda kuna mambo fulani ambayo ungependa kujua kuhusu Biblia.
KABLA ya kuchukua Biblia na kuanza kuisoma, ingefaa kujua mpangilio wake. Biblia, ambayo pia huitwa Maandiko Matakatifu, ni mkusanyo wa vitabu au sehemu 66, kuanzia Mwanzo mpaka Ufunuo.
Biblia ilitungwa na nani? Hilo ni swali ambalo limewasumbua watu wengi. Ukweli ni kwamba Maandiko hayo yaliandikwa na wanaume wapatao 40 katika kipindi cha miaka 1,600 hivi. Hata hivyo, wanaume hao hawakudai kamwe kuwa watungaji wa Biblia. Mmoja wao aliandika: “Andiko lote limeongozwa na roho ya Mungu.” (2 Timotheo 3:16) Mwandikaji mwingine alisema: “Roho ya Yehova ndiyo iliyosema kupitia mimi, na neno lake lilikuwa kwenye ulimi wangu.” (2 Samweli 23:2) Kulingana na waandikaji hao, Yehova Mungu ndiye Mtungaji wa Biblia naye anataka kuwa na uhusiano wa karibu na wanadamu.
Kuna jambo lingine muhimu linalohitajika ili kuielewa Biblia. Biblia ina ujumbe mmoja wa msingi: kutetewa kwa haki ya Mungu ya kuwatawala wanadamu kupitia Ufalme wa mbinguni. Katika broshua hii, utaona jinsi ujumbe huo unavyojitokeza kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo.
Ukiwa na hayo akilini, sasa chunguza ujumbe ulio katika kitabu maarufu zaidi ulimwenguni, Biblia.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...