Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2018

MANENO YA LEO NA TUJENGANE MEDIA 2018

Katika maisha unapaswa kukubaliana na mapungufu amabayo unayo katika nyakati amabazo unapiatia kwenye maisha yako. Wapo watu mbalimbali ambao wanakumbana na changamoto nyingi sana katka maisha yao kutokana na kushindwa kukubaliana na mpungufu ama yake binafsi au ya watu wanao mzunguka. Jifunze kuwa mwepesi wa kukubaliana na vitu kama hivyo kwenye maisha yako na baada ya hapo uchukue hatua mapema kukabiliana na hiyo hali. Kuendelea kulaumu hakukupi wewe daraja la kuvukia kuelekea kwenye nafasi ya wateule wanaokubali kushindana na changamoto katika maisha yao na sio kusindwa kizembe na chanagamoto. Ikunbukwe kwamba mtu pekee mwenye dhamana ya kunusuru malengo yako ni wewe mwenyewe. Unapaswa kujibidisha katika kufikiria mambo yalio chanya na kuachana na vitu hasi kama vile kuendelea kushindana na watu ambao wana mapungufu yalio kinyume kabisa na mlengo yako. Jijengee mfumo wa kusamehe, kuikubali na kukbaliana na mapungufu yako pamoja na mapungufu ya wenzio, jisamehe mwenyewe pale ...

VITU VYA MSINGI VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUDUMISHA UPENDO KATIKA MAHUSIANO

Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.” Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi. Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea, yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana. 1. Uaminifu Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote. Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako. Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano. Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli...

MAMBO YANAYOVUNJA UHUSIANO KATIKA MAPENZI NA NDOA ZETU

HAYA NDIO MAMBO MAKUU YANAYOVUNJA UHUSIANO WETU NA WEZI WETU. 1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako. 2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako. 3. Ubishi usiokuwa na maana. 4. Kupenda kujihesabia haki. 5. Kutokubali makosa. 6. Kutokuwa na roho ya msamaha. 7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako. 8. Usaliti wa mapenzi. 9. Kuigiza kupenda. 10. Kutomheshimu mwenzi wako. 11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua. 12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako. 13. Kuwa na jeuri. 14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani. [chumbani] 15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako [ndugu,watoto n.k] 16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja. 17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako [kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako] 18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi. 19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika                maisha yenu. 20. Ugomvi wa muda mrefu usiok...
MBINU 13 ZA KUWA JASIRI NA KUFANIKIWA KIMAISHA Mbinu 13 na rahisi za kupata ujasiri ujasiri kimafanikio. 1. Kutoshindana na waliofanikiwa. Daima mtu ahakikishe anawafanya waliofanikiwa wajione wapo juu. Kama mtu anataka kuwashangaza basi asionyeshe ujuzi wake wote. Kuwapa waliofanikiwa heshima yao kutamfanya mtu apate msaada na hatimaye afikie kiwango cha juu bila ya kupata tabu nyingi. Mfano, mtu asishindane na mwajiri wake ili kuonekana anajua sana; asishindane na tajiri katika matumizi hususani mazingira ya kijamii kama baa, misiba n.k. Waliofanikiwa hutafsiri kitendo cha kushindana kama kuonyesha kiburi au maskini jeuri. 2. Kutoamini sana marafiki. Mtu awe makini 'anapojamiiana' na marafiki au watu wa karibu. Watu wa karibu huwa wasaliti na huvujisha siri kwa wapinzani. Mtu aogope marafiki zaidi ya maadui, ikibidi awape nafasi wale anaohisi ni wapinzani. Ilkiwa mtu hana wapinzani, ajitahidi kuwatafuta. Mtu ajifunze jinsi ya kutumia wapinzani kimafanikio, si kuwaam...

UCHUMBA NA MAHUSIANO

                                     MAANA YA UCHUMBA I ngawa neno “uchumba” halipatikani katika Bibilia, tumepewa kanuni kwamba Wakristo wanastahili kupitia kabla ya ndoa. Kanuni ya kwanza ni kwamba ni lazima tutafautishe mtazamo wa dunia kuhusu uchumba kwa sababu mtazamo wa Mungu wahitilafiana na ule wa dunia (2 Petero 2:20). Huku ikiwa mtazamo wa dunia juu ya uchumba huenda usiwe na jinsi tunavyo taka, cha muimu ni kutambua tabia ya mtu kabla tufanye ahadi naye. Lazima tujue ikiwa huyu mtu ameokoka katika roho wa kristo (Yohana 3:3-8) na kama huyo mtu ako na nia ile kama ya kristo (Wafilipi 2:5). Lengo kuu la uchumba ni kumtafuta mpenzi wa maisha. Bibilia inatuambia kwamba, kama Wakristo tusioe wasio Wakristo (2 Wakorintho 6:14-15) kwa sababu hii itafanya uhusiano wetu na Kristo na tuaibishe tabia zetu na kanuni zetu ziwe hafifu. Wakati mtu amejitoa kw uhusiano, hata kama ni wa uchumba,...

NGUVU ZA VITA YA KIMAWAZO

Leo ningependa tuangalie kidogo kuhusu vita ya kimawazo Siku moja nikiwa nimelala, naliota ufalme wa Mungu na ule wa Shetani upo katika vita. Kila upande ulikuwa unafanya bidii kuhakikisha mawazo/matakwa yake yanatekelezwa kupitia mtu. Naam niliota kuna kitu Mungu anataka kizaliwe duniani kupitia mtu na Shetani naye akawa akipinga kile cha Mungu kwa kuleta cha kwake kizaliwe kupitia mtu huyo huyo. Baada ya kutafakari ndoto ile ndipo nikapata ujumbe huu, sasa endelea kujifunza. Kwanza ni vizuri ukafahamu kwamba, ikiwa Mungu ana mawazo ya amani juu yako(Yeremia 29:11), basi, Shetani pia ana mawazo ya uharibifu juu yako. Na hii ina maana kila siku mwanadamu atakutana na vita ya nini atekeleze katika ufahamu wake, naam hii ndiyo vita ya mawazo. Mungu atapigana kuhakikisha mawazo yake juu yako yanafanikiwa na Shetani naye atapigana kuhakikisha mawazo yake kupitia wewe yanafanikiwa. Kumbuka kwamba Mungu anapotaka kufanya jambo lolote chini ya jua anatumia njia ya kuweka wazo ndani y...

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHUMBA

Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba; Jambo la kwanza –    Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu 2Wakorinto 3:17  ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’. Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya. Kum...
Bwana Yesu asifiwe nipende kukukaribisha tena katika somo langu jipya la jinsi ya kutambua kusudi la Mungu ndani yako. Moja ya maswali yanayowatatiza watu wengi duniani na wameshindwa kujua ni wao kutambua makusudi ya wao kuishi katika dunia hii. Wengi wamekua wakiishi katika maisha ambayo sio yao halisi bali wamekua wakiishi kwa kuiga iga maisha ya wengine jambo ambalo ni janga kubwa kwa mkristo kua hivyo. Ila nipende kukutia moyo usikate tamaa kwa maswali uliyonayo hebu fatana nami katika somo hili mwanzo hadi mwisho na nina Imani kua utapata kitu kikubwa cha kukusaidia. NINI MAANA YA KUSUDI?? Watu wengi wameshindwa kuelewa maana halisi ya maisha yao jambo liliwapekea kuishi maisha ya wengine. Ngoja nikupe maana halisi ya kusudi KUSUDI  ~ Ni wazo au lengo lililowekwa ndani ya akili yako ili liwe kama malengo ambayo kwa hayo yataweza kuongoza maishani ili kutimiza lile ambalo Mungu ameweka katika maisha yako. Hebu tuangalie Zaidi katika Biblia inasema nini juu ...