Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2018
Jilazimishe kusamehe ili iwe rahisi kwako kusamehewa mbele za mungu.  Kuna badhi ya watu wanashindwa kusamehe kabisa hata pale wenzao wanapojishusha kwa kuwaomba msamaha . Jambo la kujiuliza ni moja,  Ni kwanini wao wasisamehe kama yesu mwenyewe awasamehe? . Lazima tubadilike na kuyafuata maandiko matakatifu.

NUKUU YA LEO NA TUJENGANE MEDIA

moja kati ya nyakati ngumu ambazo mwanadamu hukumbana nazo ni ule wakati ambao wanadamu wenzio hujinua katika maisha yako wewe. hasa katika wakati ambao  unaamini kwamba upo sahihi katika mtazamo fulani wa kitu amabacho unatazama wazi kwamba kinaweza kuwa na faida kubwa kiuchumi  na maendeleo yako kiujumla.  kwa mfano unafanya mamzi sahihi ya kuwa na mwenzi wako ambaye umetafakari kwa mapana kabisa na ukaona kwamba  huyu anasitahili kuwa na mimi kulingana na tabia zake pamoja na mipango yake ya kimaisha ila kutokana na imani za kwenu ukunapingwa na kuogopeshwa juu ya mwenzi wako. mira na desturi hukwamisha vikali maendeleo ya mtu na kumfanya kutmia nguvu kubwa kuishi na mtu ambaye hakutarajia kuwa naye . hii ni kutokana na mitazamo ya watu waliotulea huku wakiamininkatika ukabira kuwa ndio chachu ya uvumilivu katika ndoa. wanashindwa kutambua kwamba ndoa inamisingi  yake na pia kuna madhara makubwa ya kuchaguliwa ni mtu wa aina gani ungepaswa kuishi naye katika...

MANENO YA MUNGU NA TUJENGANE MEDIA

“Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; nao waupendao watakula matunda yake.” (Mith.18:21) Naomba kuwasilisha ujumbe maalum kuhusu matumizi ya vinywa vyetu kwa nia ya kujifunza faida na athari zake. Ni muhimu kutambua ya kwamba maneno yatokayo katika vinywa vyetu ya nguvu. Maneno mazuri yana “nguvu za uumbaji” na maneno mabaya ni kama “silaha za maangamizi”. Maandiko tuliyosoma hapa juu yanatujulisha jinsi ambavyo, nguvu za ulimi zimebeba mauti na uzima. Hebu tujihoji kwa kifupi hapa. Hivi kweli maneno yanayotoka vinywani mwetu yanazalisha matunda gani? Je! tunatumia maneno ya ndimi zetu kujenga au kuangamiza wengine? Maneno yatokayo vinywani mwetu ni ya namna gani? Yamejaa sumu ya chuki au ladha ya upendo? Yamejaa sumu ya uchungu au dawa ya baraka? Ni maneno ya lawama au kutia moyo? Ni maneno yanayotabiri ushindi au kushindwa? Maneno ni kama vifaa vya matumizi ya kutusaidia kufikia malengo ya kimaendeleo au kushusha moyo na kusababisha mkandamizo wa moyo na msongo wa mawa...

NUKUU YA LEO

katiaka maisha usisahau kuacha nafasi ya wanadamu kukumbusha juu ya matendo yako maovu unayopitia kuelekea kwenye mwisho wako. kikubwa hupaswi kulalamika na kusononeka kwa hayo unayopitia. kumbuka nyakati na siku zaja ambazo hutapata nafasi ya kuambiwa kwamba haupo sahihi kwenye maisha yako.  Tambua kwamba maneno yao hayana  madhara yoyote kwenye maisha yako bali yanakuongezea nguvu ya kusonga mbele na kufikia mwisho wako uliomwema . Moja ya vitu ambavyo ungepaswa kuomba kwa mungu ni hekima na maarifa thabiti ili uweze kufika kule unakotazamia bila mahangaiko na magumu  yoyote.