Skip to main content

NUKUU YA LEO NA TUJENGANE MEDIA

moja kati ya nyakati ngumu ambazo mwanadamu hukumbana nazo ni ule wakati ambao wanadamu wenzio hujinua katika maisha yako wewe. hasa katika wakati ambao  unaamini kwamba upo sahihi katika mtazamo fulani wa kitu amabacho unatazama wazi kwamba kinaweza kuwa na faida kubwa kiuchumi  na maendeleo yako kiujumla.
 kwa mfano unafanya mamzi sahihi ya kuwa na mwenzi wako ambaye umetafakari kwa mapana kabisa na ukaona kwamba  huyu anasitahili kuwa na mimi kulingana na tabia zake pamoja na mipango yake ya kimaisha ila kutokana na imani za kwenu ukunapingwa na kuogopeshwa juu ya mwenzi wako. mira na desturi hukwamisha vikali maendeleo ya mtu na kumfanya kutmia nguvu kubwa kuishi na mtu ambaye hakutarajia kuwa naye . hii ni kutokana na mitazamo ya watu waliotulea huku wakiamininkatika ukabira kuwa ndio chachu ya uvumilivu katika ndoa. wanashindwa kutambua kwamba ndoa inamisingi  yake na pia kuna madhara makubwa ya kuchaguliwa ni mtu wa aina gani ungepaswa kuishi naye katika ndoa.

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UCHUMBA

Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba; Jambo la kwanza –    Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu 2Wakorinto 3:17  ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’. Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya. Kum...

VITU VYA MSINGI VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUDUMISHA UPENDO KATIKA MAHUSIANO

Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.” Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi. Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea, yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana. 1. Uaminifu Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote. Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako. Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano. Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli...

ZINGATIA HAYA UNAPOKUWA MBALI NA MWENZI WAKO

KAMA UKO MBALI NA MPENZI WAKO ZINGATIA HAYA Kama unaishi mbali na mpenzi wako kwanza kabisa unatakiwa kukubali kua mko mbali, huwezi na wala hutakiwi kucontrol kile anachokifanya kule, acha kufuatilia anafanya nini huko, yuko na nani na mambo kama hayo, kwa kfuupi wivu weka pembeni kwani ukiendekeza utachanganyikiwa. Kuna mambo mengi atayafanya mazuri na mabaya lakini kama hakuonyeshei basi huna haja ya kuyafukunyua. Jambo la pili ni mawasiliano haya ni muhimu na anapokupigia simu au unapompigia tumieni muda wenu vizuri kwa kuongelea kuhusu mapenzi na si kila siku “Mbona hukupokea simu yangu? Mbona nilikuona online hukujibu SMS zangu? Kulalamika sijui nimesikia hivi? Nimesikia vile!” Atakuvumilia kwa muda kisha itaboa na atakua anakwepa kuzungumza nawe na mwisho mapenzi yatakufa. Hata kama mnaongea dakika tano zifanyeni ziwe tamu zihusu mapenzi na si kuzozana mpaka mtu akitaka kupiga simu anawaza hivi nikiongea naye si kelele tu, hakuna mtu anapenda kupigia simu mtu aliyenuna....