Skip to main content

TAMBUA HILI MWANAMKE KATIKA NDOA YAKO

Wewe ni mwanamke mkuu wa familia yako. Uwe na hekima na uweledi. Panga vizuri matumizi yako. Panga bajeti ya matumizi yako kwa njia ambayo haitasababisha hasara kwa utajiri na hekima yako.
Usishindane na wengine na uwaonee wivu. Kama unaona nguo nzuri imevaliwa na mwanamke, au kama unavutiwa na fanicha na vyombo ambavyo umeviona kwenye nyumba ya rafiki, usimlazimishe mumeo kununua vitu kama hivyo ambavyo vinazidi uwezo wake wa kifedha na pengine atalazimika kukopa. Je, si vema zaidi kungoja hadi hapo ambapo hali ya kipato itaruhusu au itakapopatikana akiba ya ziada ya kuwezesha kununua vitu visivyo vya muhimu?
Mara nyingi ni wale wanawake wajinga na wanaojipendelea ambao hushindwa, na kuwa wabadhirifu na kutaka kushindana. Wanawake wa aina hii huwalazimisha waume zao kuingia kwenye madeni na huchoshwa na kukasirishwa na kujaribu kuridhisha matakwa yao yasiyo weza kutoshelezwa. Wakati mwingine, ufumbuzi wa aina moja tu uliopo kwa wanaume wa kutatua matatizo haya ni uamuzi wa kumtaliki mke au kujiua.
Wanawake ambao hawatambui madhumuni ya kweli na maana ya ndoa na badala yake wanaifikiria kama utumwa ambapo mwanamume anapatikana kwa lengo la kutimiza matamanio yao ya kitoto na mahitaji ya kiulimwengu.
Wanawake wa namna hii wanataka mume ambaye atawahudumia kama mtumwa na hawatapinga njia zao za matumizi. Wanawake wa aina hii mara nyingine huenda mbali zaidi. Wanawafanya waume zao watumie zaidi ya uwezo wao hali ambayo inaweza kuwafilisi, wanaweza kufanya mauaji au matokeo yoyote ya msiba.
Wanawake wa aina hii ni aibu kwa wanawake wenzao. Endapo matarajio yake makubwa yanasababishwa kutalikiana, mwanamke atanyang’anywa mapenzi ya watoto wake na ataishi maisha ya upweke.
Kwa wanawake wa aina hii si rahisi kuolewa tena kwa urahisi. Hata kama inatokea, hakuna uhakika wa ndoa ya pili kama itadumu, kwani binadamu wengi hawapendi kuwekwa katika utumwa. Na mume mpya inawezekana naye asiwe na uwezo wa kutimiza mahitaji yao kabisa kuliko hata wa mwanzo.


Mwanamke hii ni muhimu kwako,Badala ya kuwa mwenye tamaa sana, jaribu kuwa mwenye busara. Tumia muda mwingi na juhudi kwa ajili ya ustawi wa familia yako na mumeo badala ya kujaribu kuiga mambo ya kila mtu. Kama mumeo anaumia kupita kiasi, mzuie na udhibiti matumizi yake yasiyo ya muhimu. Badala ya kununua bidhaa zisizo za muhimu, ni vema kuweka kiasi fulani cha akiba kwa ajili ya matatizo ya siku za usoni.
Ikumbukwe kwamba “Mwanamke yeyote ambaye halingani na mume wake na humshawishi afanye mambo zaidi ya uwezo wake, basi matendo yake hayatakubaliwa na Mwenyezi Mungu, ataonja ghadhabu ya Mwenyezi Mungu mnamo Siku ya Ufufuo.”
Pia “Mwanamke yeyote asiyelingana na mumewe, haridhiki na kile ambacho Mwenyezi Mungu amewajaalia na humtendea mume wake ubaya kwa kudai ampe zaidi ya uwezo wake, basi matendo yake (au ibada ya mke) hayakubaliki kwa Mwenyezi Mungu na Atamkasirikia mwanamke huyo.”
kumbuka hili  “Baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu, hapana neema iliyo kubwa zaidi ya kuwa na mume au mke mnayeelewana naye.
                       
  JITAHIDI KUWA FARAJA KWA MUMEO
Uzito wa mzigo wa maisha huchukuliwa na wanaume kwa sababu wao wanao wajibu wa kutunza na kusaidia familia zao. Katika kutimiza wajibu huu, mwamaume wa familia lazima akabiliane na matatizo mengi na vikwazo vingi nje ya familia yake. Baadhi ya matatizo haya yanaweza kuwa ukubwa wa kazi, mizozo kwenye msongamano wa magari na usumbufu wa kungoja na kupanda mabasi kutoka nyumbani kwenda ofisini na kurudi nyumbani, wasiwasi kuhusiana na masuala ya marafiki nawafanyakazi wenzake na wasiwasi wa kiuchumi na kisiasa ya siku hiyo, wasi wasi wa marafiki na wafanya kazi wenzake, na wasiwasi wa kujaribu kuboresha hali ya maisha ya familia yake. Kiasi cha mishughuliko na wasiwasi wa mtu mwenye kuwajibika ni mikubwa na yenye sehemu nyingi. Si jambo la kushangaza kwamba wastani wa umri wa mwanaume ni mdogo zaidi ya ule wa mwanamke.

Ili mwanadamu aweze kwenda sambamba na mizigo ya maisha ni muhimu kuwa na mtu ambaye atakusikiliza na kukuhurumia. Mumeo ni mmoja wapo wa watu hao. Anaweza akahisi yu mpweke na akahitaji kupata kimbilio na faraja akiwa katikati ya misukumo hii. Ni kawaida kwamba mwanaume hutarajia kupata faraja na utulivu kutoka kwa mke wake na familia yake. Kwa hiyo, tazamia matarajio na mahitaji yake.
Uwe mkunjufu na mchangamfu wakati ambapo kwanza ndio anarudi nyumbani kutoka katika kazi zake, na apate viburudisho au umfanye ahisi kwamba wewe upo tayari kusikiliza mahitaji yake. Jaribu kutokumwingiza kwenye shari kwa kuanza kumlaumu mara tu umuonapo.
Ngoja apumzike na apate nguvu upya kabla ya kumweleza madai binafsi ya watu wa familia.
Mumeo anapokuja nyumbani, jaribu kutabasamu na kumsalimia kwa uchangamfu. Mtimizie mahitaji yake ya kimwili ya uchovu, njaa na kiu. Halafu muulize kuhusu matatizo yake. Kama hayupo tayari kusema uwe msikilizaji mzuri na umhurumie. Jaribu kuonesha kuhusika kwako kwa dhati na halafu umsaidie kutambua kwamba matatizo si kwamba hayawezekani, na makubwa kama anavyodhani. Mpe moyo wa kumuunga mkono na kumsaidia aweze kukabiliana na masuala ipasavyo. Unaweza kusema kitu kama: “Matatizo haya yanawapata watu wengi. Kwa utashi na uvumilivu, inawezekana kuyatatua matatizo almuradi mtu asiruhusu yamshinde. Matatizo haya, kwa kweli ni mitihani na pia hujenga tabia ya kweli ya mtu. Usikate tamaa. Unaweza kuyatatua kwa kuazimia na ustahamilivu

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...