Skip to main content

NUKUU YA LEO

Kuishi na wanadamu kuna hitaji akili na uwezo mpana wa kutambua tabia za kila mmoja anayekuzunguka. kwa kufanya hivyo itakurahisishia wewe kujipapmbanua na kwendana na tabia zao. siyo kwa kufuata kile wanacho kiishi( ndoto zao) bali kwa kuzingatia zile tabia zao ambazo umezijifunza kutoka kwao il wasiwe sehemu ya kukwamisha mipango yako na malengo ambayo umejiwekea.
 usiogope kiwango cha maneno utakayo nenewa wakati wa kuwasoma hao bali jidhatiti vya kutosha kwa kuangalia mzigo wa malengo yako uliyo nayo. kusemwa ni sehemu ndogo sana katika maisha ya mwanadamu inategemea unasemwa juu ya nini na ni kwa namna gani unaujua ukweli juu ya kile knachosemwa juu yako.
lazima utambue kwamba umekuja hapa duniani kutimiza makusudi maalimu na wala siyo kwa bahati mbaya bali ni kwa mipango na maona makubwa toka kwa mwenyezi mungu aliyekupendelea uwepo hapa duniani na amekujalia uhai wa kuendelea utimiza makusudi yake hapa duniani.
unaweza kuwatumia wanadamu kama sehemu ya kunufaika kwa kutumia maneno yao na masengenyo yao kama sehemu ya ujuzi  wa maisha na kukuimarisha vya kutosha kwa manufaa ya  malengo yako mbeleni.  acha kujihukumu kwa kushindwa katika maeneo machache kwenye maisha yako bali kuna nanafasi kubwa unayo ya kuhakikisha  kuna jambo linatimia kama ulivyo taka litimie. kuwa wa kwanza kutoa ushuhuda wa maisha yako juu ya yale unayopitia katika kipindi chote utakachokuwa unaishi na wanadamu wenzio wakati wa maisha yako.
fikiri kabla ya kuamua  na pia amua kabla ya kufiria. sentensi hiyo kidogo ningumu kuelewa lakini ni rahisi kuitumia na ndio inatumika mpaka sasa kwenye maisha yetu ya kila siku.
kwa nini ninasema hivyo kwa sababu kuna wakati ambao itakubidi uamue kabla ya kufikiria na hatimaye kuangukia kwenye wakati mugumu kwenye utatuzi wa mamzi hayo, pia kuna wakati unafikiri kuwa ni sahihi kuamua kumbe ndio unaharibu juu ya kile ulichofikiri kuwa ni sahihi kukiamulia.
FIKIRI KALA YA KUAMUA NA AMUA KABLA YA' KUFIKIRI
     imeandaliwa na bahati magweiga 
       mwandishi wa makala na vitabu 
          simu namba 075747 2165

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...