Skip to main content

ULEAJI WA VIFARANGA NDANI YA SUKU 30 ZA MWANZO

 MAANDALIZI KWAJILI YA  VIFARANGA  NA MAMBO  MUHIMU SIKU 30 ZA MWANZO.

         By Magweiga  bahati

bahatichacha698@gmail.com

📞+255757472165

📞+255786155188

ukitaka kuwa mfugaji mzuri na mwenye kujenga uzoefu mzuri katika ufugaji huna budi kuanza na vifaranga.  Changamoto mbalimbali za uleaji wa vifaranga ndio uhalisia wa kuku katika magonjwa, ukuaji na mambo mengine yanayo mhusu.  Upo utofauti mkubwa wa uelewa kati ya mtu ambaye ameanza kumfuga kuku tangu kufaranga hadi kutaga kisha kuuzwa  na yule ambaye ameuziwa kuku wakiwa wakubwa.  

Aliyeuziwa kuku wakubwa anakuwa na changamoto chache za kutatua kuliko yule mkuzaji wa huyo kuku tangu kufaranga.  Hata katika uchambuzi wa changamoto zinazohusiana na kuku Anakuwa na uwanja mdogo wa kuzungumzia kuku kiundani. 

Asilimia kubwa ya watu hupenda kuwa wafugaji lakini hawataki kupita katika mchakato wa kulea vifaranga.  Wengi huamini kukuza vifaranga ni kazi ngumu bora kununua wakubwa.  Dhana hi kitaalamu tunaita upungufu wa maarifa /kukosa uvumilivu au uhitaji wa maendeleo ya haraka yasio na tija. 

Sasa Tuangazie mambo muhimu katika maandalizi ya kuwapokea vifaranga. 

  1. Hakikisha banda limejengwa kwa kufuata kanuni bora za ujenzi wa mabanda kama vile uelekeo wa upepo, mkondo wa maji au lisiwe katika sehemu yanakopita maji, uwezekaji sahihi wa paa, nk. 
  2. Hakikisha unaweka oda kulingana na idadi sahihi ya vifaranga ambao wanatakiwa kukaa kwenye banda hilo kulingana na square meters  pendekezwa.  Epuka kauli za kusema kwamba naagiza 250 kisha unajianda kwamba hata wakifa 50 utabaki na 200.  Ukweli ni kwamba siku wakianza kufa utabaki na 50.  Agiza vifaranga ukiwa na imani kwamba wote watakuwa vyema.  Usijipangie idadi ya vifoo kabla hata ya kuanza kufuga. ( Mungu wetu halali wala hasinzii )
  3. Kama banda ni kubwa tengeneza  bruda ndani yake ili kuzuia upotevu wa joto bandani au kuchukua muda mrefu joto kusambaa bandani . Kitendo hiki kitawafanya vifaranga wakue taratibu na pia ulaji hautakuwa sawia kwa sababu hutumia muda mrefu kujikunyata . Joto ni muhimu sana Kwa vifaranga ndani ya siku 30 za mwanzo.  Huwasaidia vifaranga kuota manyoa Kwa haraka na kukua vyema.  Zingatia kiwango cha joto kulingana na majuma sahihi ya vifaranga.  Joto hupunguzwa kadiri majuma yanavyo ongezeka pamoja na ukuaji wa vifaranga.  Epuka mkaa unaotoa moshi kwani huongeza hewa chafu bandani.  
  4. baada ya kuandaa vitaru na kuviwekea vyanzo vya joto,  hatua inayofuata ni kuandaa vyombo vya maji kwa idadi sahihi ya vifaranga. Kagua vyombo na kuvisafisha kwa maji na sabuni hata kama vipya.  Hakikisha vyombo vya chakula na Maji vina vibanio ili kuepusha kumwaga maji bandani.  
  5. wape vifaranga maji ya dawa ya kufunga vitovu  neoxychic formula baada ya kuwapokea.  Ikiwa vifaranga wametoka umbali mrefu wapewe glucose kwa masaa mawili kisha waendelee na maji ya dawa.  Epuka kujichanganyia dawa hovyo kama vile Neochick na oxyfarm nk. 
  6. Hakikisha wewe mwenyewe upo safi wakati wa kupokea vifaranga.  Epuka kutumia nguo za kuhudumia kuku wakubwa au ulizokuwa ulizunguka nazo wakati wa kuwapokea vifaranga.  Wakague vifaranga vizur na kuwaingiza bandani. 
  7.  Mabokisi yaliotumika kubeba vifaranga yasiingizwe bandani bali yaishie njee kwani yanaweza kukuachia vimelea bandani na kukuletea magonjwa. Kadharika usiruhusu aliyekuletea vifaranga kuingia bandani kwako hata kama unamfahamu

Siku 1-5.... Neochick

Siku 6……maji ya kawaida

Siku ya 7.....  Chanjo ya Newcastle

siku ya 8 ….maji ya kawaida

Siku ya 9-12… Maji yenye vitamini

Siku ya 13 maji ya kawaida

Siku ya 14 . Chanjo ya gombolo

Siku ya 15 maji ya kawaida

Siku ya 16-19 maji ye Vitamini

Siku ya 21  chanjo ya gombolo

Siku ya 22 maji ya kawaida 

Siku ya 23-26 wape vifaranga maji ya vitamini 

siku 27  wape maji ya kawaida siku ya 28    wape  chanjo ya Newcastle. 

Siku ya 35 mpaka 42 wape chanjo ya ndui.

9. Hakikisha unachakula chao cha kutosha ndani ya siku 30.  Vifaranga wapewe chakula bora chenye virutubisho ili kuwasaidia kuimarisha mifupa pamoja na Kinga ya mwili kwa haraka ndani ya siku 30.  Epuka uchanganyaji holela wa chakula cha vifaranga kwani utakuletea matatizo mkubwa kama vile 

✔️ulemavu wa muguu 

✔️kudumaa kwa vifaranga 

✔️kuvimba macho na kupofuka kabisa 

✔️magonjwa ya Mara kwa Mara bandani 

✔️kudonoana na kulana hovyo kwa sababu ya upungufu wa vini rishe katika chakula chao. Vifaranga waanze kuchanganyiwa chakula baada ya siku 30 mpaka 60

Fuatilia maendeleo ya vifaranga wako kwa ukaribu ili kubaini kama 

✔️ wanakula wote 

✔️wanatawanyika na kusambaa vyema katika banda au bruda.  Ikiwa wanajikusanya kwenye pembe za banda jua kwamba joto halipo sawia.  Hakikisha unauwa hizo kona za banda kwa kutumia kitu chochote kwani asilimia kubwa ya vifaranga hujikusanya kwenye kona na kulalina kisha kukosa hewa na kupelekea vifoo. 

✔️ Wana dalili za ugonjwa wowote ili iwe rahisi kwako kutubu mapema kabla haujawa mkubwa.  

✔️ Fuatilia sana vinyesi vyao na muonekano wao bandani.  Hi itakusaidia kujua kama kuna magonjwa nyemerezi kama vile 

    Prolium

   Salmonella

    Coccidiosis

 Flow chorela nk 

Kukiwa kuna mambukizi yoyote yanayo kutatiza muone dakitar aliopo karibu na wewe kwa msaada na ushauri Zaid. 

🍇Hakikisha vifaranga wanapewa chanjo zote kwa wakati. Vifaranga wagonjwa wasipewe chanjo mpaka watakapo kuwa wamepona. Tibu kwanza vifaranga wako wapone ndio uwape chanjo. Hapa inatakiwa umakini sana.  Unatakiwa kujiridhisha siku Tatu kabla kuwa vifaranga wako Hawa magonjwa yoyote kisha ndio uchukue hatua ya kuwapa chanjo. Zingatia uhifadhi wa chanjo kutoka dukani hadi kwako . Chanjo dhaifu haifai kwani badaye inaweza kusababisha changamoto kwa vifaranga.

🍇Hakikisha vyombo vya chakula na maji vinatosheleza kwa idadi ya vifaranga. Hii itakusaidia kupata ukuaji ulio sawia( uniform) kwa vifaranga.  Vyombo vikiwa vichache kuna badhi ya vifaranga watakula wa mwisho na chakula kichache. 

🍇Hakikisha vifaranga ambao wana dalili za magonjwa wanatengwa na wenzao kisha kuhudumiwa wa mwisho.  Fuatilia vyema na kubaini aina ya ugonjwa, chanzo chake na tiba sahihi kulingana na ukubwa wa tatizo. 

🍇Epuka utoaji dozi kiholela kwa vifaranga kwani badhi ya dawa zinakuwa nzito kwa vifaranga na kupelekea stress pia jambo hili linaweza kusababisha usugu wa madawa katika vifaranga.  Onana na dakitari wa mifugo kwa ushauri zaidi. 

🍇Unapo changanya dawa mbili hadi Tatu kutibu ugonjwa hakikisha unafahamu kiundani zinatibu nini na chemical concentration zake zinahusiana vipi. pia kuna muhimu wowote kufanya hivyo. Kuna badhi ya dawa hazitakiwi kuchanganywa na yoyote. 

Kwa uhitaji wa vifaranga bora vya kroila wasiliana nasi kupitia namba zilizopo katika makala hi.  Bei ya kifaranga ni shilingi 1500/=

Tupo kibaha pwani na mikoani tunakufikia kwa uwaminifu mkubwa.  0786155188

Magweight poultry investment.  Wafugaji, wazalishaji  na wauzaji wa kuku rika tofauti.  Pia  mayai ya layers  na kroila yanapatikana 

  Asante niwatakie ufugaji mwema

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...